Kimei alaani mauaji ya kijana Octavian, ataka haki itendeke na kuwatuliza wananchi

Ifikie mahali familia ziamue kuwasusia polisi miili wakae nayo huku taratibu nyingine zikiendelea

Kisheria Halmashauri wana mamlaka ya kuuzika mwili ambao umekaa zaidi ya siku tano bila ndugu kuufata na au kuutambua.

Watanzania wote wapo chini ya Himaya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Sitetei hili lakini alikuwa anakata ndani ya hifadhi kitu ambacho walishapigwa marufuku kisheria, according tu habari ni katika purukushani za ukamataji sidhan kama askari alidhamiria
Hoja yako haina mashiko,huko walikosomea kozi zao za askari hawajafundishwa jinsi ya kumkamata mvunja sheria na kumpeleka sehemu stahiki?Yaani maaskari wote watatu washindwe kumkamata mtu mmoja tu ambaye hana silaha yoyote hadi option iwe ni kumuua tu?Tusitetee uovu hapo mfumo ni mbovu na vitengo vimeshikiliwa na watu wenye uono mdogo haiwezekani wanyama wathaminiwe kuliko uhai wa binadamu.
 
Sorry kukwambia maybe siijui kozi yao kiundani but niliyopita mimi tulifundishwa, na uzuri mmoja kozi za askari almost wote tz zimefanana mitaala kwa 60%, 40% ni mafunzo separate inategemea na jeshi au taasisi.

Kuna taarifa nyingi sana zinatoka eneo husika, wapo wanaosema ni accidental firearm discharge (huwa inatokea, kwa wale waliopitia) wakat wa mikurupushano, wengine mshukiwa alitaka kumdhuru askari kwa panga, wengine wanasema askari wametumia nguvu kupitiliza.

Until then mm nasema tungoje uchunguzi zaidi ili kupata picha halisi nini kilitokea
 
Watanzania tumezidi upole hadi tumekuwa wajinga,ccm na serikali yake wanatutesa na kutuua kadri wapendavyo lakini tunawachekea tu,
Leo anaweza kutokea muuaji mmoja akajifanya yeye ni muungwana na mtetezi wa watu(wenyewe wanatuita wanyonge)tunampigia makofi na kumpa sifa za kila aina kumbe ni usanii tu kwa sababu nyuma ya pazia kuna maelfu ya Watanzania wanadhulumiwa haki zao na hao hao wanaojifanya watetezi wa hao wanaowaita "wanyonge".
Inatia uchungu sana.
 
Umenena,kwa nchi zingine itokee tukio kama hilo panakuwa hapatoshi aisee,uhai wa mtu sio jambo la masihara
 
Polisi wa nchi hii ni mashetani kabisa. Yaani Mtu wa kawaida anakwenda kuona maiti anasema huyu kapigwa risasi ya kichwa lakini wao waliona kajinyonga? Na bado OCD Yuko ofisini na dhamira yake ya kuficha uhalifu?
 
Dola inayolinda watawala waovu, nayo ina kinga ya kutochukuliwa hatua dhidi ya maovu wanayoifanyia nchi hususani wananchi.

Haki ni adimu Tanzania
 
Sitetei hili lakini alikuwa anakata ndani ya hifadhi kitu ambacho walishapigwa marufuku kisheria, according tu habari ni katika purukushani za ukamataji sidhan kama askari alidhamiria
Ni sawa ila majani tu yamtoe mtu uhai, kila siku yanaota? Wanajeshi tu ndio rafiki wa wananchi
 
Majani yemyewe mwisho wa siku lazima yaote tena na kua kichaka!!
Kabisaa, mtu ametolewa uhai kisa majani, ninachojua damu ya mtu huwa inalia maana imwagika isivyo halali, kumtoa mtu uhai ni kujitafutia laana pamoja na kizazi chako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…