Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe huna tofauti na hao kamchape.Hao raia wa kigoma wamezidisha uchawi na kuroga watu ndio maana hata maendeleo huko yanachelewa sana,inafikia hatu raia wakawaida tu wauza mawese wanawatishia watumishi wa uma kama madiwani,polisi,madaktari nawengineo kuwaroga! Huko kigoma hakuna amani kabisa yakukaa hasa kwa wageni wanaoajiriwa au kutafuta maisha! Yaani ni uchawi tu kwenda mbele hakuna haja yakuwatetea hao.
Watu kama wewe kumbe bado wanaishi duniani?Mleta mada nadhani hujawahi kuingia kwenye 18 za wachawi, acha waendelee kuchapwa. Ile Sungusungu ya Usukumani miaka ya 1980s - 1990s ilifanya kazi njema sana.
Juzi juzi kulikuwa na scandal moja ya hao wapumbavu. Bado tu wanaendelea? Hebu elezea wanawatesaje na wananachi? Tukijua tunaweza kutoa mchango wa mawazo na hali...Kuna raia wa Kongo kwa kushirikiana na Watanzania wanatesa wananchi kwa kuwapiga, kuwapora pesa, mifugo, mazao kwa kisingizio cha uchawi. Ni kama vile serikali ya mkoa na wabunge wako uhamishoni.
Ni mateso makubwa sana kiasi kwamba ingefaa serikali yote ya mkoa ya ccm ingejiuzuru kwa kushindwa kuwalinda raia na mali zao.
Uhuni huu umefanyika kwa kipindi kirefu sasa na police wanajua lakini wanachukua rushwa na kuwaacha matapeli waendelee kutesa wananchi.
Hayo nimeyaona wilaya za Uvinza na Buhigwe.
Serikali kwa maana ya waziri mwenye dhamana (waziri wa mambo ya ndani) ichukue hatua haraka sana au Waziri ajiuzuru.
Nawasilisha
Scandal ipi mkuuJuzi juzi kulikuwa na scandal moja ya hao wapumbavu. Bado tu wanaendelea? Hebu elezea wanawatesaje na wananachi? Tukijua tunaweza kutoa mchango wa mawazo na hali...
Siamini katika ujumbe huu KALINZI ninayoijuwa kwa Kina hlf uniambie eti kila familia inalipa elfu 5 kumlipia kamchape huo ni UONGO UONGO UONGO UONGO.Narudia tena ni Udhalilishaji, Upuuzi, Ushenzi, Uchonganishi na Utapeli.
Nimefika mkoa wa Kigoma Tokea Majuzi nilicho Kikuta huku Sielewi Huku ninchi Nyingine au ni Tanzania hii hii !
Kuna kitu kinaitwa KAMCHAPE, hawa wapuuzi nani kawaleta, Hili kweli nani kalipa Baraka kufanyika karibu mkoa mzima wa Kigoma?
Kinachofanyika Ni Udhalilishaji na Uchonganishi kwa jamii.
Kwanza Wanachangisha Tsh 5,000 kila kaya kwa lazima sio ombi.
Kisha Wanapita kila nyumba Eti wanatoa Uchawi na wachawi! Tena utake usitake lazima.
Wakifika kwako wanasema hapa kuna uchawi Lazima uchapwe kisha unanyolewa Nywele Mbele ya umati wa watu kisha kunyweshwa Kile wanachoKiita Dawa hautakuwa mchawi tena!
Nimefuatilia kinachofanyika pale ni Mazinga Ombwe na Kujipatia Pesa kwa Utapeli!
Wakati Yakifanyika hayo Kijiji Jirani, Nyie mnaanza jiandaa na kama mwenyekiti hata Wakaribisha hao watu au kuchangisha hizo pesha kila kaya naye Anajumuishwa kwenye Kundi moja la Wachawi !
Kuna vitu vya Ajabu sana Vinafanyika mpaka nimeshikwa na Butwaa. Nimeuliza nikaambiwa Serikali Ndio Imeruhusu hili Lifanyike Mkoa mzima kweli?
Mbona Sioni Dodoma na Mbeya Kwanini Kigoma?
Kwasasa zoezi limepamba Moto Vijiji vya Nyarubanda, Kalinzi, Mukigo, Muhinda, Nyaruboza, Rukoma, Igalula, Mgambo, Katumbi, Kalya Nk.
Huko kumechafukwa hali ni mbaya na lisipofanyiwa kazi na kuacha litaleta shida kwa watu
======================
UPDATE: 13/09/2023
Hatimaye Jeshi la Polisi limeingilia Kati jambo Hili
View attachment 2749733
Pia soma
- Mfahamu 'Kamchape' mkamata wachawi na shughuli zake kwa ujumla kutokea hapa Mkoani Kigoma
Scandal ipi mkuu