Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Unatoa comments kutokana na msukumo fulani fulani uliopo nje ya uwezo wako. Isipokuwa tambua tu kwamba Mimi Ninatoa Maoni yangu hapa nikiwa na moyo thabiti kabisa wenye nia njema kwa nchi hii ili tusije kuingia kwenye shimo ambalo hatutaweza kujinasua endapo kama tutatumbukia humo.
Aidha, Mimi siyo Mwislamu Wala sina maslahi yoyote yale huko kwenye dini hiyo ambayo inanasinishwa na hao Wapiganaji wa huko Msumbiji.
Nimetoa Maoni yangu haya nikiwa ni mtu mwenye mitizamo na fikra huru kabisa, ambapo sijaegemea upande wowote usiostahili, Bali ni kueleza ukweli na uhalisia wa mambo jinsi yalivyo.
Usifikiri watu wote ni wajinga wajinga
 
Huyo mhuni anaandika kwa code
I think you have a short-sighted mind.
Je, umeshawahi kujiuliza ni kwa Nini nchi yenye uchumi mkubwa kama Nigeria imeshindwa kulitokomeza kundi la Boko Haram licha ya kwamba nchi hiyo Ina Jeshi Kubwa Sana na lenye nguvu zaidi ukilinganisha na nchi nyingine yoyote ile kwenye ukanda huo wa Magharibi mwa Afrika???Do you know the reasons???
 
Navomfahamu kagame, alikua anatafuta upenyo wa kuibagaza Tanzania kisawasawa na iko wazi chance ya msumbiji kama nchi tuliichezea sana na nyusi alitafuta msaada kwetu tukaleta siasa sasa we will pay the cost, sababu tunahitaji kusini kote mtwara, ruvuma tuwe macho vinginevo tutaingia vitani miaka mitatu au minne mbele kama utani, magaidi watadhibitiwa msumbiji na watahamia Tanzania hili linawezekana
 
Usifikiri watu wote ni wajinga wajinga
Nakupa pole sana.

Inavyoonekana wewe huwa unakurupuka tu na kuandika comments zako humu mitandaoni bila hata kutafiti kwa undani juu ya kile unachoandika.
Watu kama wewe ndio mmekuwa kiini Cha kuibuka kwa matatizo mengi yaliyopo kwenye nchi zetu hizi za Afrika. Migogoro ya kibinadamu imekuwa sugu barani Afrika na haimaliziki kutokana na kuwepo kwa Watu wengi wenye akili kama za kwako.
 
Kuondoka Kwa vikosi vya SADC msumbiji ni ombi la rais Nyusi na mkuu wao wa majeshi waliwaarifu jamaa waondoke na ukumbuke vikosi vya Rwanda wanaishi kama wafalme kule maana hakuna wanachokosa kuanzia posho nono, vifaa vya kisasa yaani hata wakiwa doria mtaani wanajeshi wa Rwanda wanavifaa vya kisasa na bora zaidi kuliko hata wanajeshi wetu, lazima kazi ifanyike kubwa na serikali ya msumbiji Kwa sasa imeshaanza kuwalipa wanajeshi wa Rwanda hadi mishahara Kwa siri, na achilia mbali makampuni hayo ya Rwanda lakini TOTAL wanaomba vikosi zaidi vikalinde uwekezaji wao lakini sharti viwe vikosi kutoka Rwanda tu
 
Tuongeze nguvu kubwa sana huko kusini na usisahau mission za jeshi la Rwanda hua ni hatari wanaweza kupeleka hata kikosi cha siri kikawatrain magaidi au renamo wakapewa na vifaa wakatuvamia mchana kweupe lazima tukae tayari
Hizi akili mnatoaga wapi na Rwanda aivamie Tanzania kwa nini? ndio maana CCM wanajipigia wanavyotaka
 
Ma

Ugadi biashara kama biashara zingine tu hakuna cha ugaidi wala nn jiulize silaha wanapata wapi na nguvu
...hizo agenda zilishapangwa na western leaders kwa ajili ya kudhoofisha Africa walikuwa wanamtumia Mobutu sasa hivi Kagame
Kagame hana akili ya kipuuzi kama nyie na mobutu, anajielewa kuliko hata westerners
 
Jeshi la Tanzania litaendelea kubaki huko hata pale wengine wa SADC watakapokuwa wamejiondoa.
Tutazidi kupoteza makamanda wetu na hakuna faida yoyote tunayoipata. Hii nguvu tuliyopeleka huko tungeipunguza tukaimarisha usalama wa mipaka yetu.

Kwa maoni yangu tungeacha makamanda wa kuzugia tupeleke na Watu wa TISS kwaajili ya udukuzi wa taarifa.
 
Tz kusini haiko salama,vyombo vya habari nafikiri hawaruhudiwi kutangaza sana hili lakini hapako salama haswa mpaka na msumbiji inaniuma sana.

Tunajeshi Bora sana naliamini(JW),wapo Kule wanajitahidi lakini naona Badoo..Cha kufanya waongezwe zaidi,hakuna maana mwanajeshi akae Bariadi,misungwi,Mlowo au Handeni bila jukumu la maana wakati huko kusini panahitaji nguvu zake.Tulinde taifa letu hususani raia wake kwa garama yoyote.
 
Kila tunamtukanaga Kagame, ila in real sense acha jamaa azid kupambania maslahi ya Rwanda kama sisi tumeamua kulala sawa tuendelee nza huu ujinga ujinga maana ndio tunauweza.

Anatumia akil sana. Imagine kama isingekua kongo na Car na sasa Msumbiji, hiv unafikiri idadi yoote hiyo ya wanyarwanda iwalioko huko wangetosha pale Kigali na viunga vyake??

Kwakifupi itakuja siku tutakuja gundua tumezungukwa na wanyarwanda kila kona.

Idara za usalama na majesho ya nchi zote zknazotuzunguka, zitajaa wanyarwanda tu.

Unafikiri mko na raia wa msumbuji kumbe ni mnyarwanda alizamia huko miaka na miaka..

Tanzania inachiweza ni petty issues tu, Jw wanachowaza wao ni ugali tu na ada za watoto wao shule. Hakuna zaidi ya hapo, Sa100 hana hata ajualo kuhusu namna gani Jeshi linapaswa kuwa na mafungamano ya karibu na serikali katika kuhakikisha ustawi wa Taifa
 
Tz kusini haiko salama,vyombo vya habari nafikiri hawaruhudiwi kutangaza sana hili lakini hapako salama haswa mpaka na msumbiji inaniuma sana.

Tunajeshi Bora sana naliamini(JW),wapo Kule wanajitahidi lakini naona Badoo..Cha kufanya waongezwe zaidi,hakuna maana mwanajeshi akae Bariadi,misungwi,Mlowo au Handeni bila jukumu la maana wakati huko kusini panahitaji nguvu zake.Tulinde taifa letu hususani raia wake kwa garama yoyote.
Ni kweli mikoa ya mipakani huko Kusini haiko salama sana kutokana na Mgogoro wa huko Msumbiji. Jeshi letu linapaswa kuongeza nguvu nyingi zaidi kwenye upande huo ili kuimarisha ulinzi.

Aidha, tuondoe wanajeshi wetu waliopo huko Msumbiji, badala yake walinzi hao wajikite kulinda mipaka ya nchi yetu.
 
magaidi watadhibitiwa msumbiji na watahamia Tanzania hili linawezekana
Wakiingia Tanzania magaidi, nina mashaka TZ nayo itakwemda kuomba msaada wa kijeshi Rwanda.
Hii nchi ina viongozi wa ajab sana hujapata kuona. Ukiwatazama sasa kwenye suti zao unaweza dhani ni watu flan wenye akili na hekima kumbe doohh!! 😂
 
Back
Top Bottom