Mimi binafsi kwa Maoni yangu ni kwamba Jeshi la Tanzania (JWTZ/TPDF) linapaswa lijiondoe kutoka huko Msumbiji, badala yake Jeshi hilo lijikite kwenye Ulinzi wa Mipaka ya nchi yetu ya Tz. Iimarishe ulinzi ktk mipaka ya Tz na Msumbiji, lisijiingize kwenye Migogoro ya ndani ya nchi ya Msumbiji na hata ktk nchi zingine zote ambazo tunapakana nazo, tuache kufanya hivyo kwa sababu kuendelea kujiingiza kwenye hiyo Migogoro ndio chanzo Cha kuhatarisha usalama wa Wananchi wa nchi hii pamoja na mali zao.
Mbaya zaidi kwenye huo Mgogoro wa huko Msumbiji ni kwamba hata baadhi ya Viongozi wakubwa wa Serikali ya Msumbiji nao wapo nyuma ya Mgogoro huo, hao Wapiganaji wa hilo Kundi la RENAMO wamekuwa wakipata taarifa zote muhimu kutoka kwa INFORMERS wao ambao wapo ndani ya Serikali ya Msumbiji.
Je, mmeshawahi kujiuliza ni kwa nini Jeshi la Serikali ya Msumbiji halikuwa na Kambi nyingi za Jeshi ktk maene hayo ya Kaskazini kwa nchi hiyo ya Msumbiji, hususani kwenye hilo Jimbo la Cabo Delgado? Kwa nini kwenye Jimbo hilo kulikuwa na kambi chache sana za Jeshi na badala yake Kambi nyingi sana za Jeshi ziliwekwa upande wa Kusini mwa nchi hiyo?? Je, mnazijua sababu????
Hata pale Kampuni za kutoka Ulaya za Uchimbaji wa Gesi zilipoenda kuchimba Gesi kule Jimboni Cabo Delgado Serikali ya Msumbiji ilizijulisha na kuziruhusu Kampuni hizo kwenda huko wakiwa na Ulinzi wao binafsi, na pia Kampuni hizo ziliruhusiwa kwenda na Jeshi lao binafsi kwa ajili ya Ulinzi wao na hatimaye Kampuni hizo Walikodi Jeshi binafsi la Kujitegemea kutoka kwa Makaburu wa Afrika ya Kusini, Je, mmeshawahi kujiuliza ni kwa nini Serikali ya Msumbiji iliamua kufanya Maamuzi Kama hayo????
I remind you, "No research no right to speak ", Mgogoro wa huko Msumbiji una historia ndefu, haukuibuka tu hivi hivi from nowhere.