Ndugu zangu watz wenzangu nadhan mtakuwa nami juu ya kinachoendelea kwa sasa katika nchi yetu
Wafanyabiashara saiz wanajiamulia bei gan watupige na kila siku wanapandisha bei hasa wakijisikia kitu ambacho ni hatar sn kwa usalama wa nchi
Kibaya zaid pamoja na bei za vitu kupanda kila siku yan ni kama hatuna viongoz yan ni kama nchi inajiendesha yenyewe.....Rais yupo,wazir mkuu yupo,mawazir wapo lkn masikin ya Mungu hakuna hata mmoja mmoja anaeumia na kuumizwa kwa wananchi hawa watz ndio kwanza kila mtu yuko bize kuangalia anavunaje sehem aliyopo
Hali hio sasa imetoka kwenye chakula imeenda had kwenye mawasiliano ya simu yan saiz wanajibadilishia tu vifurushi kila wanapojisikia ....yan kwa kweli hali ni mbaya sn tena sn na masikin ya Mungu watz hawa hatujui hata haki zetu tunasubir wakina CHADEMA au NCCR ndio watusemee bila wao kufanya hivo kila mtu yuko kimya hadi vile vyama vyetu vya kiraia ambavyo sijui viko wapi siku hizi
Hebu imagine unakwenda sokon lkn unakuta kila mtu anauza vitu kwa bei yake na wala hata hawana wasiwas wao wanasema wanafidia kipind kigum cha mwendazake
Hiv kweli Tanzania tumefikia huku kweli jaman,mbona inasikitisha sn jaman
Huyu mwananchi wa kawaida kabisa anaishije kwa hali hii?
Nadhan sasa umefika wakati wa wanachi wa Tanzania kuleta umoja wetu na kureact bila kujali utofaut wa vyama vyetu,dini zetu wala ukanda wetu na kuacha kutegema vyama vya siasa kutusemea katika matatizo yetu
Serikal imeshindwa mapema sn katika hili la mfumuko wa bei hivo ni wakati wetu sisi wananchi kuondoa tofauti na kuwa kitu kimoja katika hali hii mbaya kabisa katika ustawi wa taifa na maendeleo ya wananchi
Naomba kuwasilisha
Ukweli hali ya mfumuko wa bei inatisha ila naomba nikurekebishe kidogo,
Uchumi wa nchi yetu unaendeshwa na soko huria kwa sasa hivyo issue ya bei ya bidhaa inaamuliwa na kanuni za soko huria sio serikali.
Kwenye soko huria bei ya bidhaa inaamuliwa na nguvu ya soko(forces of demand and supply).Katika mfumo wa soko huria ni ngumu sana serikali kupanga bei ya bidhaa sokoni.
Katika mazingira ya sasa tatizo lililopo uhitaji ni mkubwa kuliko usambazaji/uzalishaji hii ni
moja ya sababu ya huu mfumuko wa bei.
Ziko sababu nyingine zinazoweza kuathiri bei ya bidhaa sokoni mfano kupanda na kushuka kwa thamani ya dola kunaweza kuathiri bei ya bidhaa kutoka nje ya nchi.
Ukame na majanga ya asili pia kunaweza pelekea bidhaa fulani ikawa haba sokoni.Mfano mzuri ni nafaka zinavyopanda bei nyakati za ukame ambapo mavuno yanapokuwa haba.
Kupanda kwa Bei ya nishati kama mafuta na umeme kunaongeza gharama za uendeshaji na kupelekea bidhaa kupanda bei.
Sera za nchi pia kwa sasa nazo zinachangia hii hali tunayoiona leo.Sera ya uchumi wa viwanda imesababisha uzuiaji wa bidhaa nyingi kutoka nje kwakuziongezea ushuru ili kulinda viwanda vya ndani ambavyo kwa hali inayoonekana viwanda vya ndani vinazalisha kidogo kuliko mahitaji ya soko hivyo imepelekea bei ya bidhaa kupanda.
Mifano michahche ya bidhaa zilizo ongezewa ushuru kutoka nje ni sukari na Mafuta ya kula ambavyo tunaona hali ilivyo mbaya.Mipakani mfano Tunduma wanatumia sukari kutoka Zambia wananunua tsh 2000 kwa kilo wakati Tanzania hali ya bei ya sukari ni mbaya.
Suluhusho la huu mfumuko ni serikali kutizama sera zake ili kuokoa hii hali.Serikali iruhusu bidhaa kutoka nje kwa utaratibu maalumu ili kulinda viwanda vya ndani lakini pia isiumize wananchi.
Serikali ipunguze tozo kwenye nishati.Ukifuatilia nishati kama mafuta serikali imeweka tozo nyingi mno zote hizi ni tatizo.
Kwakweli hali mtaani ni mbaya sana.
Kwa uchache ni hayo.