Kinachoendelea Tanzania kuhusu mfumuko wa bei ni hatari kwa ustawi wa maendeleo ya wananchi na usalama wa nchi

Kwa nabii LEMA anasemaje?
 
Ukweli hali ya mfumuko wa bei inatisha ila naomba nikurekebishe kidogo,
Uchumi wa nchi yetu unaendeshwa na soko huria kwa sasa hivyo issue ya bei ya bidhaa inaamuliwa na kanuni za soko huria sio serikali.

Kwenye soko huria bei ya bidhaa inaamuliwa na nguvu ya soko(forces of demand and supply).Katika mfumo wa soko huria ni ngumu sana serikali kupanga bei ya bidhaa sokoni.

Katika mazingira ya sasa tatizo lililopo uhitaji ni mkubwa kuliko usambazaji/uzalishaji hii ni
moja ya sababu ya huu mfumuko wa bei.

Ziko sababu nyingine zinazoweza kuathiri bei ya bidhaa sokoni mfano kupanda na kushuka kwa thamani ya dola kunaweza kuathiri bei ya bidhaa kutoka nje ya nchi.

Ukame na majanga ya asili pia kunaweza pelekea bidhaa fulani ikawa haba sokoni.Mfano mzuri ni nafaka zinavyopanda bei nyakati za ukame ambapo mavuno yanapokuwa haba.

Kupanda kwa Bei ya nishati kama mafuta na umeme kunaongeza gharama za uendeshaji na kupelekea bidhaa kupanda bei.

Sera za nchi pia kwa sasa nazo zinachangia hii hali tunayoiona leo.Sera ya uchumi wa viwanda imesababisha uzuiaji wa bidhaa nyingi kutoka nje kwakuziongezea ushuru ili kulinda viwanda vya ndani ambavyo kwa hali inayoonekana viwanda vya ndani vinazalisha kidogo kuliko mahitaji ya soko hivyo imepelekea bei ya bidhaa kupanda.

Mifano michahche ya bidhaa zilizo ongezewa ushuru kutoka nje ni sukari na Mafuta ya kula ambavyo tunaona hali ilivyo mbaya.Mipakani mfano Tunduma wanatumia sukari kutoka Zambia wananunua tsh 2000 kwa kilo wakati Tanzania hali ya bei ya sukari ni mbaya.

Suluhusho la huu mfumuko ni serikali kutizama sera zake ili kuokoa hii hali.Serikali iruhusu bidhaa kutoka nje kwa utaratibu maalumu ili kulinda viwanda vya ndani lakini pia isiumize wananchi.

Serikali ipunguze tozo kwenye nishati.Ukifuatilia nishati kama mafuta serikali imeweka tozo nyingi mno zote hizi ni tatizo.

Kwakweli hali mtaani ni mbaya sana.

Kwa uchache ni hayo.
 
Jua kwamba watu waliopo ni wale wale ila mwendazake alikua dictator asie penda kukosolewa, anawza kuua mtu wakitofoutiana mtizamo tu, lazima tusubiri probation period ya miaka mitatu kwasabb kubadili sera na sheria ni mchakato sio tukio, sera mbovu za mwendazake fisical and economic policy lazima zipitie bunge, ndo zibadilishwe, naona hili limeanza private sector imeanza kupata nguvu na watu binfsi wameanza kuwekeza mdogo mdogo.
 
Nzuri lipi mkuu? Mwendazake kaua sekita nyingi kwa kutaka sifa na umarufu wa kisiasa, hata vile vizuri alishindwa kuvifanyia business plan, kama ATC hamna anae isema ila inaingiza hasara kila siku.........mazuri yake ni ya kutafuta tu.
Vipi nyinyi na chama chako mmeshafanya zuri gani?
 
Una malalamiko ya msingi ila unaowalalamikia sio watu sahihi kulalamikiwa. Wafanyabiashara sio chanzo cha kupanda kwa bei za vitu, pia hakuna kosa lolote kwenye uchumi wa soko huria wafanyabiashara tofauti kuuza bidhaa kwa bei tofauti ambazo kila mmoja anaona zina faida kwake.

Malalamiko yako yaelekeze wizara ya fedha na uchumi pamoja na benki kuu ya Tanzania (BoT), hao ndip wenye uwezo sahihi wa kurekebisha mfumoko wa bei, sehemu nyingine yoyote ni siasa tupu.
 
Sasa kama ng'ombe wanakufa kwa ajili ya ukame!Unataka nyama uuziweje na ili hali ng'ombe wamepungua?.
Kwa nini wanasubiria hadi wafe? Hao wanaokufa si wauzwe kwa bei ndogo
 
Nyama sio basic kwenye uchumi wa Tanzania wengi hawaitumie ata ingeshuka kwa 5000 kwa kg kwahiyo sio kigezo cha kupimia uchumi wetu
Nyama ni basic na inaweza kuwa chanzo cha pili cha protini baada ya maharage hapa nchini.
 
Matrilioni wanayolipiwa huko Stigler na SGR ni kwa dolari au pesa za madafu?
 
Miaka mitatu mingi sana, Wizara ya fedha na BoT lazima waje na mpango maalum katika kipindi kifupi kurekebisha hali, watu wa kipato cha chini wanaumizwa sana na hii hali.
 
Miaka mitatu mingi sana, Wizara ya fedha na BoT lazima waje na mpango maalum katika kipindi kifupi kurekebisha hali, watu wa kipato cha chini wanaumizwa sana na hii hali.
Mpango kama upi? Bot ikiamua kushusha riba kwenye Bank za biashara ( intrest on Bank rate ) kwahali yasasa tuta pata inflation au mfumko wa bei na kushuka kwa thamani ya shilling ya Tz dhidi ya dollar, tusubiri natural growth of the economy, angalau miaka miwili, ndoturapata hali ya uchumi wa kweli......kwa sasa uzalishaji uko chini sanaa pesa ikiwa nyingi in circulation lazm bei intapanda tu, naona policy ya serikali iko sawa
 
Reactions: Ame

Mfumuko wa bei ni kwa sababu Mama amefungua nchi-Zitto Kabwe!
 

Hebu twambie kimetokea nini ikiwa bei za bidhaa na huduma zimepanda maradufu baada ya budget ya kwanza ya Mama!?Take in note (usisaha ongezeko la kodi na tozo kwenye huduma na bidhaa) hivi mnafikiri watanzania wote ni wajinga hawafatilii na awaoni?
 
mwendazake ndo alievuruga sector binafsi na kutimua wawekezaji binfsi. Tutakuja kupata unafu baada ya miaka kama 3. Ndotutaanza kumlaumu Raisi sio kwa kwasasa
Pamoja na definition uliyoitoa ambapo kimsingi ni yq vitabuni, umevuruga kwa kutoka nje ya vitabu ulivyonukuu kwa kuanza kulaumu bila kuweka facts.

Uhalisia ni tofauti na hayo mavitabu na especially kwa TZ hii inayoongozwa na brainless.

Mfumuko wa bei unaweza tengenezwa na kina Jan + Msoga team
 
Huyu maza ameharibu sn nchi yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…