Hatukuona Bakhresa akifunga biashara hata alipoambia alikwepa kodi na kudaiwa bil 10, alilipa na akaendelea na biashara, Mengi hakufunga biashara, MO aliendelea, Manji na GSM chini ya mwamvuli wao ule wakakimbia, TIN zilipounganisha biashara zote zimilikiwazo na mtu mmoja kwa majina tofauti ili kukwepa kodi, wakafunga zile zisizo halisi.
Mtumishi mwenye mshahara wa tzs 800,000 anakatwa kodi kubwa kuliko mfanyabiashara anayeingiza faida ya tzs 800,000 kwa wiki 1 kwakuwa mfanyabiashara ana mianya ya kukwepa kodi. Uliwahi sikia mtumishi akaacha kazi kwakuwa kodi ni kubwa?
Kama $2.29bn alizokopa zimeingia mtaani kweli kujenga madarasa, vituo vya afya na ZNZ, tozo za kila mwezi zilizotangazwa mara moja zinaingia kwenye madarasa pia, unahitaji miaka 3 ya nini kuona impact yake?
Au ndo kupunguza paye ambapo ni kama ongezeko la kati ya tzs 8,000 mpaka 50,000 kwa mshahara na kisha kuanzisha tozo za zaidi ya 100,000?
Na huo utaalamu wenu, tofauti yetu sisi na wake weupe ni nini basi kama tuna prof wa uchumi, wana prof wa uchumi, wao wanasogea, sisi tunabaki kumlaumu JPM? Kabla yake, uchumi ulikuaje? Mlifanya nini?