Hapana mkuu, kama ungejikita kwenye kwenye kuchambua uhalisia kisha ukatuwekea hizo facts za elimu, sisi tungenufaika na kuelewa ILA kwakuwa umeamua ku-side, point zako zinakuwa na uwalakini.
Mfano dogo, mama kafungua nchi kishamba kabisa, Shinyanga, Kahama na maeneo yafananayo huko, kwasasa wamejaa Kenyans, Rwandans, Comorians etc wananunua mchele kwa kutumia TZS moja kwa moja kwa mkulima kwa kiwango kikubwa, wafanyabiashara wazawa walikuwa wananunua kwa tzs 1,100 kwa kilo, wageni wananunua tzs 1,800 kwa kilo, mkulima atachagua kumuuzia nani? Vipi sasa wananchi wa Dsm wanaosubiria, waliozoea kununua kilo kwa hiyo 1,800? Nchi inapataje faida au fedha za kigeni hapa na especially dollars? KES ni stronger, tunafahamu kama hiyo tzs 1,800 inaweza kununua kilo ya mchele Kenya? Kenya hawawezi ku-package mchele wetu na kuurudisha kwa bei kubwa zaidi?
Mtu mmoja asiye hata na $1bn, unamzungumzia nani labda na kwa uhakika gani? Shimbo alisemekana kumiliki Tzs 3trillion alizozificha SA, Nelson Mandela akitoa siri hiyo, ni wakati wa Liase affairs.
Leo mtu mmoja kwa maslahi ya tumbo lake, anaweza kupandisha bei ya mafuta, mfumuko wa bei hautatokea/haujatokea tayari?
Mtu mmoja aliua usafiri wa rei ili malori yake yafanye kazi, kwa bei yake, bei zitabakia pale pale mtaani? Ni mtu mmoja tu, hahitaji mabilioni, mamlaka tu ya kipumbavu na anaweza kutikisa kila kitu, so kama hizo formula zinasema haiwezekano, nadhani si kwa TZ.