Kinachoendelea Tanzania kuhusu mfumuko wa bei ni hatari kwa ustawi wa maendeleo ya wananchi na usalama wa nchi

asante ndugu mchumi. Sasa rais aliahid kupandisha viwango vya mishahara , je kwa mtizamo mfumko wa bei utakuaje ? Na nn mapendekezo yako kuhusu nyongeza hiyo. Kwamba aongeze au isubiliwe miaka mingine hadi tuikamate the so called natural growth of economy ?
 
Hatukuona Bakhresa akifunga biashara hata alipoambia alikwepa kodi na kudaiwa bil 10, alilipa na akaendelea na biashara, Mengi hakufunga biashara, MO aliendelea, Manji na GSM chini ya mwamvuli wao ule wakakimbia, TIN zilipounganisha biashara zote zimilikiwazo na mtu mmoja kwa majina tofauti ili kukwepa kodi, wakafunga zile zisizo halisi.

Mtumishi mwenye mshahara wa tzs 800,000 anakatwa kodi kubwa kuliko mfanyabiashara anayeingiza faida ya tzs 800,000 kwa wiki 1 kwakuwa mfanyabiashara ana mianya ya kukwepa kodi. Uliwahi sikia mtumishi akaacha kazi kwakuwa kodi ni kubwa?

Kama $2.29bn alizokopa zimeingia mtaani kweli kujenga madarasa, vituo vya afya na ZNZ, tozo za kila mwezi zilizotangazwa mara moja zinaingia kwenye madarasa pia, unahitaji miaka 3 ya nini kuona impact yake?

Au ndo kupunguza paye ambapo ni kama ongezeko la kati ya tzs 8,000 mpaka 50,000 kwa mshahara na kisha kuanzisha tozo za zaidi ya 100,000?

Na huo utaalamu wenu, tofauti yetu sisi na wake weupe ni nini basi kama tuna prof wa uchumi, wana prof wa uchumi, wao wanasogea, sisi tunabaki kumlaumu JPM? Kabla yake, uchumi ulikuaje? Mlifanya nini?
 
Kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ni useless kama inflation au mfumko wa bei haujadhibitiwa, value ya Tz shilling intaendelea kushuka dhidi ya $.....ndomaana unaona Raisi hajagusia kuongeza mishahara paka pale economy itakavo recover to normality kwa kupata real economic growth sio economic development ya mwendazake, alitupumbaza sana alilazimasha economic development wakati disposable income ya Wtz iko chini, ndo madhara hayo tunao pata sasa hivi wasio jua uchumi wanamlaumi Raisi wa miezi tisa kwenye utawala, wakati hili bomu alilitegenezwa na jpm.
 
Jinga sana, akili yako matope tu! Mimi ningekuwa Rais wa nchi hii watu wa aina yako mngekuwa chakula cha mamba na si vinginevyo...
 
Wafanya biashara wa kubwa kama bhakresa au GSM, sio lahisi kufrisika, ni gharama kubwa kwa wao kufunga kuliko ku operate kwa minimum loss,.......tena serikali inakusanya direct na indirect taxes nyingi kwao watu kuliko mtumishi anae lipwa 800,000 paye yake ni 14% baada ya kukata basic ya 300k.......ila huyu GSM analipa excise duty property tax income tax Paye tena bidhaa zake zinalipishwa Vat wafanya kazi wake wote wanakatwa Paye gari zake zinalipiwa ushuru na kodi za mafuta. Muekezaji moja kama Bakhresa ni zaidi ya watanzania 1m wakawaida, tungekua na Bakhresa kama 100, nchi yetu ingekua katika kiwango kingine, sasa mwendazake alikua anapambana nao ili wafirisike uko anakopa kimya kimya ndo maana tuko kwenye hi economic stack.
 
Hivi tajiri gani aliyetimuliwa aliesababisha kilo ya nyama kufikia 12 elfu?

Naona sasa hata waume zenu wakishindwa kusimamisha wawapnd mtamsingizia mwenda zake.
 
Kama wafanyabiashara wanajiamulia bei za vitu bas ina maana Tz hatuna wizara ya fedha wala vyombo vya fedha kama vile T.R.A na benk kuu...ndugu mwandish je huoni kama huu ulio andika ni upotoshaji
 
Hivyo vyote ni sehemu ya gharama ya biashara na usiniambia kwamba hujui gharama zote hizo zinaingizwa kwenye bei ya end product kwa mteja! Si yeye anayeingia mfukoni kulipia hivyo, mlaji wa mwisho ndio analipa! Na zaidi yeye anayo Tax return, vipi kuhusu end user?

Anapambana nao ili wafirisike? Kama una billions of tzs kwenye account, ukashindwa kuzitolea maelezo jinsi ulivyozipata, kisha ukapewa hesabu za jinsi unavyodhaniwa kuingiza kipato chako kulingana na records zako ulizoandikisha na mtiririko wako wa ulipaji kodi, na kuambia, hizi usizojua umezipataje SIO zako, tunazichukua au tunaenda mbele ya sheria, ukachagua zichukuliwe ili ubakiwe na UHURU wako, utamlaumu mtu kuwa KAKUFIRISI?

MANJI alirudi kipindi hiki cha Miss Utalii, mbona kaondoka tena?

Mnadai kwa sasa kuna utawala unaofuata sheria, na wale wote wafanyabiashara wameachiwa kwakuwa wameonewa, kisheria huyu mtu anaruhusiwa kufungua kesi dhidi ya serikali kudai kusafishwa na kulipwa alichopoteza na fidia juu, sijui ni wangapi wamefungua kesi hizo ili angalau tu kusema kweli kulikua na uonevu?

Tuko busy kurudisha Chunya, ardhi zilizorudishwa serikalini n.k kujaza wazenji bara na kupukutisha bara kwa zenji, wewe umekomaa na uchumi uliosoma vitabuni ambao hauna impact pengine hata kwa mazingira yaliyokuzunguka.
 
Numbers never lie.

Kwa miaka 6 watanzania waliishi kwa uongo na hofu, takwimu nyingi hazikuwa za kweli sababu tu ni kumfurahisha boss.

The moment of egg on face was inevitable .
Kwamba nondo ilikuwa inauzw elfu 28 tukawa tunafichwa?

Kwamba bidhaa zilipanda sana bei tukawa tunafichwa?

Hivi mnafikiri kila mtu ni mjinga na haoni kinachoemdelea?
 
Namfumko wa bei ya vitu na vyakula ulikuwepo kwamba hivihivi wananchi walinunua kwa kudanganywa na takwimu na umeme ulikatika hivihivi? Utetezi mwingine mhhhh
Haya mataahira yanafikirisha sana mkuu
 
Kwani sukari ilipanda kipindi gani na watu wakaambiwaje?

Si waliishia kuwaambia tuko vizuri tuna sukari ya kutosha?

Mafuta ya kupikia yalipanda enzi za nani na why serikali ilikanusha hakuna uhaba uliochangia bei kupanda?
Hiyo ilikuwa ni sukari, vipi sasa hivi mbona kila kitu bei juu
 
Kwanini sasa uchumi wa jk haukusavaivu kipindi cha magu?
 
Mama akilala akiamka anawaza 2025..basi. Huyu anatakiwa asipate kura hata moja
 
Mama akilala akiamka anawaza 2025..basi. Huyu anatakiwa asipate kura hata moja
Kufika 2025 mama atakua amesha nyoosha uchumi wetu, mbona tu tamchagua kwa kupenda wenyewe, japo kura zetu sio determinant wa nani awe Raisi wa nchi hi.
 
Kufika 2025 mama atakua amesha nyoosha uchumi wetu, mbona tu tamchagua kwa kupenda wenyewe, japo kura zetu sio determinant wa nani awe Raisi wa nchi hi.
Usalama wampe kwa nguvu lakin sio sisi
 
Mateja mbona walikuwepo, kuli kua na ombwe kubwa sana la taarifa kwa wananchi ndio maana vitu vingi cya hovyo mlikua hamsikii, sasa kwa kua mna pata taarifa sasa ndio maana mna ona kama ni taharuki
 
Unataka kusema Tanzania hakuna wizara ya fedha wala benk kuu? yaani wafanyabiashara wanajipangia wenyewe bei.Embu fafanua vizuri term “kujiamulia”
 
Hiyo ilikuwa ni sukari, vipi sasa hivi mbona kila kitu bei juu
Serikali ni ile ile ya uongo sasa mnachokipata ni muendelezo tu , mama yenu naye yuko busy kusuka timu yake kuelekea 2025.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…