Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kwa kweli awaachie shule waendeshe wenyewe wakusanye kodi.
 
Mkuu umepangilia hoja zako vizuri tena kwa reference hongera sana.
 
Non profit organization inalipaje kodi.? Kwanza Kodi maana yake nini tuanzie hapo
1. Je kamishina wa kodi alishawapa certificate ya kutolipa kodi?
2. Kuna kodi zinazotokana na mishahara, je ilikuwa inapelekwa ipasavyo na complience za SDL na PAYE returns
3. Wafadhili wanapotoa pesa na St. Jude hainufaiki na chochote tofauti na elimu inayotoa
4. Hakuna wanafunzi wengine wanaolipa ada?
kuna maswali mengi lazima uyapatie majibu ndiyo utajua status ya hiyo NGO
 
Great inputs!
 
Mzee tunaomba utusaidie kujibu hizi HOJA za TRA toka mlipo anza kupambana nao katika hili jambo Mwaka 2012.

Inawezekana Mahakama imewaonea, tunaomba mjibu hapa HOJA za TRA katika hii kesi yenu ya malimbikizi ya KODI.View attachment 1641914
Nikiwa mwanasheria wa shirika la kiserikali niliwahi kuandika barua kwa waziri na kamishna wa kodi kuhusu kupunguziwa na kusamehewa kodi (VAT) kwenye baadhi ya miradi mikubwa lakini kila siku tulikuwa tunapigwa kalenda. Mara nyingine nilikuwa nashinda mahakamani kwenye kesi ambazo mamalaka za kiserikali kama TRA, TTCL au LAPF imelishitaki shirika letu ambalo ni la kiserikali. Sasa jiulize kama mti mbichi (taasisi za kiserikali) tulikuwa tunapelekwa hadi mahakamani kisa kodi, unadhani mti mkavu (taasisi binafsi) watapona kweli ???

Mashirika mengi ya kiserikali yamepona kuanzia mwaka 2018 baada ya kupitisha sheria za mabadiliko zilizotenganisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka na Ofisi ya Wakili Mkuu: Ambapo ilitolewa amri kwamba taasisi za kiserikali hazitakiwi kupelekana mahakamani. Hivyo hii kesi ya St. Jude naielewa vizuri kwasababu mimi binafsi nimeshuhudia kinachoendelea huko serikali kabla ya kuamua kuachana nako kabisa(There's a structural Rot).

Sasa nimeiosoma vizuri hii kesi na kuelewa kitu kimoja cha kisheria ambacho mahakama imekitilia maanani lakini nadhani siyo sahihi sana: Kusema kwamba Bank Interests, Surplus and other Profits are taxable. Binafsi ninavyofahama unaposema Public Trust Fund/Charitable Work/Endowment haimaanishi kwamba ni lazima iendeshwe tu kwa pesa za misaada na zawadi.

Ukisoma vizuri sheria za Uingereza hasa The Laws of Trusts & Equity utatambua kitu muhimu kwamba hii misaada inaweza kufanyiwa biashara na msimamizi (Trustee) kisha kuzalisha faida ambayo itakuwa kwa ajili ya walengwa (Beneficiaries). Hivyo kiiingereza naweza kusema A Trust/ A Charitable Organisation/ An Endowment can engage in a business inorder to develop profit than can be solely used to advance the cause of a beneficiary.

Mtu anaweza akatoa msaada wa pesa kusaidia watoto masikini kusoma, aidha akaanzisha shirika ambalo bodi yake ikaamua kufanya biashara kama kununua hisa au kuanzisha viwanda. Lengo hapa siyo kupata faida binafsi (Personal Benefit), lakini lengo hapa kupata faida kwa maslahi ya walengwa (Beneficiaries) ambao ni watoto masikini. Hichi kisheria kinaitwa Reinvestment of Endowment Fund. Hili husaidia kuwezesha hizi taasisi zijiendeshe vizuri hata pale ambapo kuna siku wafadhali wanashindwa kutoa fedha, basi taasisi haifi.

Sasa nikupe mfano hai kabisa: Vyuo Vikuu vya Marekani na Uingereza vinatumia huu mfumo wa Endowment Funds kujiendesha. Kuna watu walitoa pesa kama msaada, lakini bodi za vyuo zikaamua kufanya biashara ili kutengeneza faida ambazo zitatumika kusaidia wanafunzi wanaosoma hapo vyuoni. Hii ni biashara ndiyo lakini haifanywi kwa faida ya mtu binafsi bali mlengwa (Beneficiary). Marekani Harvard University ina miradi mingi inayoingiza fedha, lakini fedha hizo kazi yake ni kuendelea kusaidia chuo kiwepo: Hawa kodi walikuwa hawakatwi kabisa mpaka alipokuja Donald Trump na Steve Mnuchin kutaka kuanzisha Endowmnent Tax mwaka 2019.

Umetokea ugomvi mkubwa mpaka sasa kule Marekani baada ya Serikali ya Donald Trump kutaka kauanza kukata kodi hizi Endowment Funds kwasababu eti kwenye hivyo vyuo kuna biashara zinafanywa na kuna baadhi ya wanafunzi wanalipa kodi. Mswada wa Trump na Mnuchin umesema kwamba vyuo vyote ambavyo walau kuna wanafunzi zaidi ya 500 wanaolipa ada binafsi basi lazima vikatwe kodi. Hili siyo sahihi, maana lengo kuu ni kuzalisha fedha kwa ajili ya faida binafsi, bali kuhakikisha wamarekani wanasomesha watoto wenye uwezo na wanafanya tafiti kubwa za kisayansi.

Bahati mbaya sana nadhani Tanzania yetu kwenye suala zima la The Law of Trusts & Equity bado tuko nyuma sana hivyo kuona watu mnashangalia hichi kinachoendelea na kukomaa kwamba ni biashara binafsi sishangai. Lakini wewe kama msomi inabidi ujiongeze, fanya tafiti na kuangalia wenzetu wanafanyaje. Kama kuna utakatishaji na ukwepaji kodi basi wahusika wakamatwe na siyo kuumiza watoto wetu ambao taifa linatagemea waje kuwa viongozi wa kesho.

NB 1: Kuna kesi ya ajabu sana ya Coca-Cola Kwanza Ltd ambayo ilitolewa maamuzi na Jaji Kyando mnamo miaka ya 90 mwishoni. Aliwapigisha faina ya ajabu Coco-Cola kampuni ambalo lilikuwa ndiyo changa nchini Tanzania, hadi wasomi wenzake wa sheria walimtukana na kumuita "A Lazy Lawyer", sasa hii ni fedhea kubwa sana kwa mwanasheria yoyote. Hapa inabidi tujiongeze na kuangalia nini hasa lengo la hizo biashara au faida zinazokusanywa na St.Jude, kama zinatumiwa na watu binafsi basi wapewe adhabu mara moja, lakini kama faida hiyo inatumika kutimiza malengo ya msaada ambayo ni elimu basi nadhani sisi kama wasomi tunatakiwa tujiongeze haraka na kuwafunga speed-governor TRA.

NB 2: The Law of Trusts & Equity inaruhusu Endowments/ Charitable Organisations/Trust Funds kufanya biashara na kupata faida, ikiwa tu faida hizo zinalenga kutimiza matakwa ya hiyo Charity/Endowment, ambapo lengo kuu ni Advancement of Education. Tanzania sisi kwenye Law of Trusts & Equity bado tuko nyuma na hakuna sheria za kutosha ambazo zimezungumzia hili. Hivyo wanasheria inabidi tujiongeze, maana nikisomea kesi naona hadi Mzee wangu Jaji Mziray ameamua kuwa A Positivist na kusoma sheria kama ilivyo bila kutafuta tafasiri za kifalsafa ambazo zingesaidia kufahamu ni faida gani ambayo inaongelewa hapa na nini haswa ni lengo ya hiyo faida.


CC: Chige , Sophist
 
Wahenga walisema "Jogoo La Shamba Haliwiki Mjini "

- mtu wa kijijini aletwapo mjini shida kubwa sana hutokea !

- Just imagine ndege 11 cash money ?? Kama ni Utalii, kwa nini hoteli zinageuzwa Hostel ?

- Ushamba ni Shida Ya Zama Zote Ndugu Watanzania !
 
Wawasomeshe ili waje wasumbue mtaani. Jukumu la kutoa Elimu ni la serikali na Wala haijashindwa.wanatakatisha fedha hao

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
 
Wewe jamaa, mimi na wewe tutakuwa ni Distant Relatives........
 
Mimi nadhani watanzania hawakosei.. yote haya ndio kukua na kupanuka kitaasisi na kimifumo. Ni changamoto kama hizi zinatusaidia kuboresha sheria zetu..

Sasa TRA wanakwama wapi au Shule kutumika kufanya fraud hilo ni swala la kitaasisi... TRA wanaibaka shule ..na shule inawabana watumishi...kwa fraud.

Ukisema hapana tusiibane shule kwa makosa ya mtu mmoja mmoja ndani ya taasisi.. basi hautakuja kumkamata na kumuwajibisha yeyote kwenye makosa ya kampuni..

After all, kampuni haili, wala haina mikono ni Watu ndani yake ndio walaghai na wezi.. lazima ibebe responsibility.

Swala la wao kutaka kuchangisha ni swala la.kurelejea sheria za uanzishwaji wao.. ambayo si kazi ya TRA.. waende waseme hatutatoa ufadhili wa masomo kwa asilimia mia.. wanafunzi watachangia.. huenda ikawa inaangukia category nyingine kabisa kwenye usajili.. hilo inabidi tuwaachie wanasheria watufungulie.

Ila ninachoamini.. TRA sio mazwazwa kama tunavyojaribu kuwachora hapa.. ni wataalamu na wanasimama na sheria tulizozitunga wenyewe.. kama enforcers lazima tuwaelewe.. huwezi kutetereka kisa huruma inaingia katikati... Hautaweza kusimamia chochote na sheria zitakuwa obsolete
 
Serikali yetu ni sikivu;

Jambo hili litafanyiwa kazi;

Watoto wataendelea na elimu.
 
Hii shule ina kitu hakiko sawa mahala...

Nimeangalia bajeti yake ya mishahara kwa mwezi... ni average ya 1.6m kwa mtu kwa mwezi.

Kwa mwaka hii shule ilikuwa inaspend 12b kutoa elimu kwa wanafunzi 2000. An average of 6m per child. Hii ni ada za Bablo.. ambako wanaenda elites.

Mfumo wake wa kuwapata wanafunzi unafanyika rigorously kote nchini... na wanarecruit 150 kids per year. Nimehoji hapo juu sinze 2007 kweli hakuna yeyote amesoma hapa uzi huu umefikia aseme kitu roho zetu zitulie!?

If they are truly spending this much per child.. hata mimi ningepambana nipeleke mwanangu huko.. kwann upeleke mtoto Tusiime wakati huku ni bure!? Sijui kama this makes sense

Na kuwapata vijana walienda TASAF ambao wana database ya walio masikini wa kipato nchini!? Ambao watoto wao bado wanapewa pesa za madaftari na serikali!?

Huenda aliyeanzisha alikuwa na malengo mema... But this has been hijacked na waroho ambao wanaitumia kifamilia na kishkaji. Na huenda kama sio close friend utalipa tu..

Kuna shule tulisoma sisi kila mtu alikuwa ana ada yake.. 🙂 na wengine hawalipi kabisa 🙂
 
Nimekupata, Ahsante kwa nyongeza hii.
 
St Jude wahamie Kenya mbona kazi rahisi!! Hii nchi bila hekima wengi tutaumia shule inatoa ajira kibao,ufadhili kibao,elimu na malezi kwa gharama zao kubwa hatakama wachache wangelipia bado kwa sehemu kubwa inasaidia nasio biashara!! Sasa zinafungwa zigeuzwe hosteli za vyuo kama jirani yake ngurdoto hotel.inaudhi sana. Ama kwakuwa ipo aruxha sio ile kanda yetu pendwa??
 
Tusubiri maelezo ya serikali kwanini wamefunga na wameona nini chenye wasiwasi, kupokea 1.7B kila mwezi constantly kwa miaka yote ile nadhani hata uchumi wa Tanzania unaingia kwenye inflation and as a bonus bado hulipi kodi
Mkuu taasisi inatumia 1.7bil kwa mwezi mil 500 ikiwa ni mishahara.

Tanzania kupiga kwata la Uhuru kwa siku inatumia mil 995. Ndio maana JPM akaona bora zijenge hospital ya Uhuru Dodoma.

Well, ngoja tuone wakubwa watasemaje.
 
Ipo haja ya kufanya cost benefit analysis:-
(i). Hivi kama mtoto anayesomeshwa na jirani ni wako - kuna haja gani kuvutana kwa ajili ya surplus? - hapa TRA mnataka kuvuna msikopanda!

(ii). Hawa watoto wanaposoma faida ziko kwa nani Tanzania au Australia? Kama ni kwetu vikwazo vya nini dhidi ya walezi na kwa watoto wetu?

TRA msimwangushe JPM kwa hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…