Mkuu wataalamu wa TRA sio mbumbumbu kama unavyosema. Tatizo wanafanya kazi wakiwa na shinikizo fulani nyuma.Sasa hawana namna zaidi ya kufanya kibabe.Kwani wewe mkuu! Huu ukimya haukufanyi ujihoji!? Honestly!
Mie tangu Jana nimetoa angalizo waliosoma Jude waje Watueleze what's what!
Kwa ajili ya uzi huu nimejua zaidi ya Kodi.. na diagnosis inabidi iendelee.. kupata fursa ya kujua zaidi sio kitu kibaya.. mie si mtaalam wa Kodi na katu siwezi kuingilia ninachopinga ni kuaminishwa kamba hawa wataalamu wetu (TRA) ni mambumbumbu kiasi kwamba haya yanayojadiliwa hapa na wataalamu wa JF wao hawayajui kabisa.. hilo tuu
Kama unakumbuka,mkutano wa wafanyabiashara na Rais malalamiko mengi yalikuwa juu yao. Wanaua biashara sana hawa watu.
Hebu fikiria kampuni kubwa kama Vodacom licha ya kuwa na wataalam wa kodi wa kila Idara,bado wanapigwa fine kila siku na hawa TRA.
Mtu ambaye hajawahi kufanya biashara ya level fulani hawezi kuwajua TRA. Ila amini wanaua sana biashara.