Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana...
Tuwakumbushe watawala wa Afrika kuwa kushika hatamu haukufanyi ugeuke kuwa injinia, daktari, mhasibu, mwanasayansi au mtaalam zaidi! Power doesn’t suddenly increase your knowledge or qualify you to be anything more than you were! Waache u-much-know wawe humble!
 
Mgogoro wa hii kodi umeanza Mwaka 2012 siyo Mgogoro wa jana au wa Serikali ya Magufuli.
Hii shule ni ya zamani sana..tangu mwaka 2007 nakumbuka..kwanini iwe leo ndio waangalie suala la kodi mlima hivyo..
 
Inategemea, kuwa NGO hakufanyi uwe EXEMPTED kulipa kodi.

Ni lazima ufuate taratibu za kisheria ili uweze pata KIBALI 'Ruling' toka kwa Commissioner General na utakuwa subject kwenye taratibu za kuandaa mahesabu yako tofauti na Organisation zingine.

Tusikariri jambo hili.
Non-Profit Organization haiko subjected to Tax payments.
 
Wewe umefuatilia huu mgogoro?

Mgogoro huu upo toka 2012 wakati walipofanyiwa Audit na baadaye Audit findings zikaonyesha hawakuwa na sifa ya Charitable Organisation kwa maana ya sheria za kodi.

Tokea hapo wamepelekana kwenye mabaraza ya kodi mpaka Mahakama ya Rufani ambayo maamuzi yake hayajatofautiana na maamuzi ya Bodi ya Rufani za kodi na Baraza la Rufani za Kodi. Inakuwaje leo mnakimbilia ni Magufuli kabana?

Ukitaka kuwa NGO ambayo hailipi KODI fuata TARATIBU ZOTE ZA KISHERIA acheni kutengeneza mabomu ambayo yakiripuka mnatafuta huruma za kisiasa.
Inaelekea umekariri au kukaririshwa kauli za wanasiasa. Hii ni shule iiyoanzishwa na mama raia wa Australia kusaidia watoto maskini kupata elimu. Watoto zaidi ya 2000 wa msingi na sekondari wanasoma, kuvalishwa na kulishwa bure, bila kulipa hata senti moja, vijana zaidi ya 300 kutoka kaya hizo hizo wanalipiwa karo na stipend kusoma vyuo vikuu na vyuo vya kati bila wazazi wao kugharimia. Sasa wewe unazungumza kodi gani. Yaani wananchi wa Australia wajitolee kusomesha Watanzania kupunguzia Serikali/TRA mzigo wa kugharimia elimu halafu Serikali iwatake wahisani wanaoisaidia kugharimia elimu kulipa kodi!

Soma hiyo attachment utaelewa kinachojadiliwa. Tafadhali usikariri wa kukubali kukaririshwa.
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana...
Mzee tunaomba utusaidie kujibu hizi HOJA za TRA toka mlipo anza kupambana nao katika hili jambo Mwaka 2012.

Inawezekana Mahakama imewaonea, tunaomba mjibu hapa HOJA za TRA katika hii kesi yenu ya malimbikizi ya KODI.View attachment THE SCHOOL OF ST. JUDE LTD VS THE COMMISSIONER VGENERAL TRA CIVIL APPEAL NO.21 OF 2018 HON.MWA...pdf
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana...
Hii menejimenti ya St. Jude haijakurupuka kutoa msimamo wake. Hiyo ndio fact. Serikali wataamua kupoteza au kupata lakini TRA wakae na serikali kupima hoja za St. Jude ikionekana faida ni kubwa kuliko hiyo hasara ya 5 bln kwa serikali. Then waifutie shule kodi.
Angalizo

1. Hii shule ni msaada mkubwa kwa kanda ya Kaskazini katika kutoa elimu bure na yenye kiwango cha juu.

2. Wafanyakazi waliajiriwa pale zaidi ya 300 wanachangia pato la taifa kwa kulipa kodi PAYE ambayo ni hela ya kutosha tu kumsaidia serikali kupanga vipaumbele vyake.

3. Account za shule hii ni faida kwa benki husika kwenye transactions shule inazofanya.

4. Watoa huduma kwenye shule ya St Jude mf. Dizeli, vyakula, maji umeme nk nk hunufaika na shule na hivyo kuleta kodi serikalini.

5. St. Jude ni mwekezaji kama alivyo mwekezaji mwingine Tanzania. Serikali impe kila support na kumshauri ili aendelee na uwekezaji huu na sio kusubiri mpaka matatizo yametokea mnaanza kumsumbua na kumletea fitna.

6. Ukweli ni kwamba TRA kama ina hoja za msingi zitolewe kwa umma na Kamishna TRA Taifa au waziri husika kuondoa taharuki na sintofahamu kwa wanafunzi, wazazi, staff na menejimenti ya St Jude.

7. Ninashauri ni vizuri mwenye kuusoma uzi huu atembelee website au tovuti hii kufahamu hii shule kwa undani. www.theschoolofstjude.co.tz

8.Tujenge watanzania wenzangu kuchambua hoja vema na kujaribu kuelewa jambo kabla ya kulaumu au kukashifu.
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara

Hivi sheria zetu zinasemaje kuhusu pale kitu kinapoingia kama zawadi au msaada nacho chatozwa kodi?
 
Mzee tunaomba utusaidie kujibu hizi HOJA za TRA toka mlipo anza kupambana nao katika hili jambo Mwaka 2012.

Inawezekana Mahakama imewaonea, tunaomba mjibu hapa HOJA za TRA katika hii kesi yenu ya malimbikizi ya KODI.View attachment 1641914
Very interesting case, tunatabia ya kufanya copy and paste ya sheria zetu ila tafsiri halisi na implemention zake inakuwa shida.

Binafsi nadhani wakili wa hiyo shule ‘Mr Duhia’ or rather one of its board members appears to know his accounting legal staff.

Kwanza inaonekana kuna issue ya kutokuwa na sheria mahususi (nor case laws) zinayotoa tafsiri ya ‘badges of trade’ kuelezea mipaka yako kabla ujaonekana unafanya biashara, having said that (kwa sheria za nchi za wenzetu hiyo shule bado inaangukia kama charity organisation).

Hatari ni kwamba ukiweka tafsiri ya badges of trade kwa Tanzania kama inavyotumika kwa nchi za wenzetu halafu utake watu wanao qualify walipe kodi kutokana na activities zao kuna watu wengi watalia aijawahi tokea. Mifano kidogo tu umwambie dalali anatakiwa awe na TIN number kwa sababu nyumba na viwanja anavyouza ni more than 2 million kwenye hiyo hela 18% ni VAT ya serikali na faida ya mapato yake 20% ni profit ya serikali anatakiwa alipe kodi as a sole trader; au machinga aonyeshe risiti zake hao watu awawezi kukuelewa kabisa).

Pili asilimia kubwa ya income iliyopata hiyo shule kama bank interest, miscellaneous income etc. Sababu zinazofanya TRA idai kodi falls into capital gain tax, rather than corporate tax kwa nchi za wenzetu ili charity isiathirike.

Ijumaa leo mida hii kidogo akili ipo nusu, ila huyo Mr Duhia arguments zake ndio sahihi sio TRA at least in global view of what a charity is. Inawezekana sheria zetu zina tafsiri nyingine (but then the, Law is the Law) kwa ivyo lazima ziheshimike nonetheless if the purpose of a charity is to help the needy with that line of reasoning amendments are required.

Huu mjadala kama unaendelea kesho ntaweka senti 50 zangu when I am sober, ila TRA needs proper accountants.
 
Swali la msingi Kwanza tangu shule hii imeanza,huwa inalipa Kodi seriklini?imekuaje kukawa na limbikizo la Kodi?
 
Mbona hakuna sehemu inaonyesha walienda mahakamani? Ili sakata mimi nilianza kuliona kwenye YouTube channels sijasikia kwenda mahakamani

Hiyo brief report ya shule inaonyesha breakdown ya expenses zao (hawana msamaha wa kila kodi wanalipa paye) na hakuna income zaidi ya ufadhili na wenyewe una cover operation costs tu; TRA wamechukua hiyo hela shule aiwezi jiendesha.

Kuna tatizo TRA hapo sio tu wanafunzi kukosa elimu, unapoteza ajira, paye za serikali, unaaribu supply chain, huko nako kuna ajira na kodi za serikali.

TRA needs sorting out
Si waache kusomesha watoto bure?mvutano wa nin i?kama wanataka kutusaidia na sisi hatutaki nini kifanyike?Naona humu wengi wenu mnasomeshewa watoto pale bure,concern yenu sio kodi na uonevu,ni kusomeshewa watopto wenu bure!
 
Si waache kusomesha watoto bure?mvutano wa nin i?kama wanataka kutusaidia na sisi hatutaki nini kifanyike?Naona humu wengi wenu mnasomeshewa watoto pale bure,concern yenu sio kodi na uonevu,ni kusomeshewa watopto wenu bure!
It’s an accounting legal issue based on existing laws, come with that line of argument umewekewa mpaka kesi yenyewe.

Kwani sisi tulio zaliwa maskini kwenye hii nchi hatuna haki yakupatiwa elimu bora to enhance our life chances.
 
Jiwe si binadamu kabisa!
Japo jina sio zuri ila yeye anahusika vipi?

Msingi wa mzozo wenyewe ni surplus za 2 billion (roughly) in 2009 and 2.25 billion 2010. Mapato ambayo kutokana na source zake (based on law) shule ilitakiwa kulipa capital gain tax.

Whereas TRA wanataka the same income walipe corporate tax na kuitoa shule as a charity registered because it’s profitable. An argument which isn’t justifiable.

Watu kama nyie siku mkijikwaa mtalaumu serikali ya Magu. Sio kila kitu siasa soma kesi toa mawazo yako proffesionally.
 
Sasa kodi hapo inaingiaje wakati wafadhili wameamua kusomesha watanzania sasa hiyo kodi inatokana na biashara gani inayofanyika hapo hakuna mtu yeyote anayeuziwa huduma. Au huelewi kodi ni kitu gani. Kwanini watanzania tunakuwa mazezeta kiasi hiki. Watu wamejitolea kusomesha watoto wetu bado tunashindwa kushukuru tuna matatizo gani.
Usibabaike na maelezo ya upande mmoja.
 
Kilatha,ukiwa unataka kunisaidia mimi kidekede,mimi sitaki,what do you do?
Sio kilatha tu ata wewe hakuna mtu anaetoa msaada sehemu usiotakiwa (at personal level).

Ila kwenye nchi kutoa msaada sio utashi wa mtu au taasisi. Kuna sheria zinazoelezea watu wanaohitaji huo msaada hizo taasisi zinatakiwa zishiriki vipi.

Ndio maana nchi inaongozwa kwa katiba na sheria kwa wale tuliowapa dhamana, viongozi wetu hawana mamlaka nje ya hapo.

Tanzania kuna sheria za charitable organisations kuwepo and the rules of their engagement.
 
Hivi wafanyakazi wao hawalipi kodi? Suppliers wao wa vyakula, uniform, vifaa vya kufundishia n.k. hawalipi kodi? Je mchango wa hao wanafunzi katika uchumi wetu utakuwaje? Na tutapata faida gani wakikatishwa masomo?

Amandla...
Mfanyakazi anahusiana nini na kodi ya shule! Yeye analipa kodi ya mshahara wake tu. Vitabu! Jipange uandike tena.
 
Sio kilatha tu ata wewe hakuna mtu anaetoa msaada sehemu isiyotakiwa.

Ila kwenye nchi kutoa msaada sio utashi mtu. Ni sheria na watu wanaohitaji huo msaada. Ndio maana nchi inaongozwa kwa katiba na sheria kwa wale tuliowapa dhamana, viongozi wetu hawana mamlaka nje ya hapo.

Tanzania kuna sheria za charitable organisations kuwepo and rules of engagement.
Kilatha kama unataka kunipa laki moja mimi siitaki unafanyaje?wa australia sijui kina nani wanalazimisha kutusaidia,kwa nini?kama hawawezi kulipa kodi waache kutusaidia!!!waende wa kajustify wasilipe kodi kwa vile ni charity kama wanaonewa.ikikinzana na sheria zetu they have two options:
1)Pay Tax
OR
2)Pack and Go back to Australia!
 
Wafadhili wamejitoa sasa serekali inapora fedha za mashirika ya ndani
 
Back
Top Bottom