Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Mkuu,Watanzania wengi ni maskini.Hawa mabwana wanafanya physical means testing,yani wanakuja nyumbani kuona mazingira ya mtoto ila awe na vigezo vya kuwa maskini.Wanawachukua toka shule za serikali on the second year.These people are doing a good job mkuu wakiondokoa.Tutakuwa wajinga sana kwa kiwango chao cha uwekezaji na huduma bora wanazowapa watoto ambao hawaweza kulipa ada za FEZA na IST
Watanzania tuna hila mkuu usijidai umekulia uingereza,Compassion ilikuwaje?Watu wenye kazi walijaza watoto wao na wanakazi,hata rafiki yangu Tom Baba Toby,boss wangu alikuwa mtoto wake analipiwa na compassion.Alikuwa na kazi na mkewe ana kazi.Wanaenda ghafla au wanawataarifu siku ya visitation?Lengo ni zuri sana lakini fuatilia sio wazazi wote ni masikini.
 
Wewe jamaa bado akili zako hazijakaa sawa.Cha kufanya ni kukwambia tu kwamba.Kama roho inakuuma wenzako kutendewa wema basi fanya tu kujitambua kwamba wewe ni binamu yake ni Ibilisi.Hayo mengine tuachie watu wa Arusha
Jamaa akili zake mbona zimekaa SAWA....

Amekuuliza ni kwanini mna hulka ya kujaza watoto WASIOSTAHILI kusomeshwa bure katika hizo shule?!!

Jamaa yuko sahihi...

TRA imeingia vyema tu....taifa kuachwa liende KIHOLELA Wala hakuna afya...

Sasa CORPORATE TAX hiyooooo........
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Watadaiwaje kodi wakati hawafanyi biashara na wanafadhiliwa 100%! muwe mnasoma kabla ya kucomment!
 
Wewe jamaa bado akili zako hazijakaa sawa.Cha kufanya ni kukwambia tu kwamba.Kama roho inakuuma wenzako kutendewa wema basi fanya tu kujitambua kwamba wewe ni binamu yake ni Ibilisi.Hayo mengine tuachie watu wa Arusha
Acha vya bure nenda kalipe ada watoto wasome.Una post humu huo sio umasikini.Masikini wa Tanzania hata smart phone hana.Kalipe ada za watoto acha ujinga.
 
Hicho ndio kiini chenyewe.
Watu wengi Arusha wanajua kisa kilianzia siku Magufuli alipokuja Arusha kwenye kampeni na waendeshaji wa shule ya St. Jude wakagoma kuswaga wanafunzi wake kwenda Sheikh Amri Abeid kuongeza idadi ya wahudhuriaji kwenye mkutano wa CCM.

Wamiliki wa shule waliweka wazi kuwa, shule yao haina itikadi yoyote ya vyama vya siasa, uongozi wa shule haukuwa na mamlaka ya kuwahusisha kwa lazima wanafunzi wake kwenye itikadi za vyama na mwisho uongozi wa shule hauwezi kuhahakisha usalama wa wanafunzi wake kwenda uwanjani.

Yote kwa yote, chuki ya serikali ya Magu dhidi ya ukanda wa Kaskazini ni kubwa mnoo, St. Jude huenda ni miongoni mwa taasisi za Elimu zilizokuwa zinawindwa kuangamizwa kwa muda mrefu sana, maana ni miongoni mwa taasisi za mtaji wa kimaendeleo ya kijamii kwa kizazi cha watoto na vijana waliopo kanda ya Kaskazini.
Usilete chuki kwa jamii dhidi ya serikali bila uthibitisho au ushahidi wowote! Acheni hizo tabia
 
Hii shule ni Non Profir Business, najiukiza kodi inatokana na nini? Labda kama kuna ane ewa kiundani upande wa pili atujuze maana huu ni mkanganyiko
Uko sahihi,ndio maana ni lazima sana kupata madai ya upande wa TRA ili Kuweza kusema ni uonevu ama la
 
Kuna siku nilikuwa naona graduation ya wahitimu wa kozi ya kodi. Nikajiuliza how is that possible (labda tuna mbinu nyingine na dunia) maana hiyo sio conundrum ya kuku na yai kipi kimetangulia.

In practice you need to be an accountant first (which cover aspects of taxation) tools you need for everyday working and then you can specialise into taxation (this is why tax accountants earn big bucks).

Ndio hayo sasa anakuja afisa wa TRA kukudai kodi (he is not a qualified, accountant) wakati shule yenyewe ukiona hiyo report income yote ni kwa sababu ya operations costs tu na hakuna faida.

Unachukua 500m baada ya kuona faida ipi or how do you even justify that.

Apatikane mtu wa ku sort TRA kuna issues za taxation Tanzania. Nilikuwa naangalia vipindi vyao vya elimu ya kodi kwa raia nikajisemea these ppl are at their mercy siku afisa akienda kumkadiria mtu kodi.

Halafu awajali yaani unaaribu uchumi bila ya kufikiria mara mbili.
 
Kwa juujuu ni RAHISI kukataa....

Ila.....

Ziko SHULE ZA MAYATIMA ambazo zinapata FEDHA ZA WAFADHILI ambazo haziko liable to tax....lakini ndani mwake WANASOMESHWA WATOTO WENGI MNO kwa ada ya WAZAZI NA NDUGU ZAO....
👆👆👆

Hapo huipati harufu ya MONEY LAUNDERING?!!!
Kuna kitu kinaitwa cross subsidisation. Unachukua wanafunzi wachache wenye uwezo halafu unatumia ada wanayolipa kuwalipia wale wasio na uwezo. Aidha, ninavyojua mimi ni kuwa kodi inatakiwa kutozwa kwenye faida na sio mapato. Hata kwenye shule ambazo za kibiashara hauwezi kudai kodi kubwa kwa sababu tu ada yao ni shilingi milioni tano kwa kila mwanafunzi bila kuangalia gharama zao za uendeshaji kama mishahara ya walimu, vifaa vya masomo, usafiri, umeme, maji n.k. Kwa hiyo kabla ya kuwa shuku hawa kwa kosa la money laundering unatakiwa kupitia vitabu vyao. Na ukikuta kuwa wanapaswa kukulipa basi unakaa nao kuangalia namna gani wanaweza kukulipa bila kuathiri utoaji wao wa huduma hii muhimu. Ni vigumu sana kufidia siku ambazo wanafunzi watapoteza ikiwa shule itaendelea kufungwa. Busara ilitakiwa kutumika kabla ya kuwafungia account yao.

Amandla...
 
Uko sahihi,ndio maana ni lazima sana kupata madai ya upande wa TRA ili Kuweza kusema ni uonevu ama la
Huu uonevu mkuu, tangu lini shule inayosomesha watoto bure that means ni charitable entity, swala la kodi linatoka wapi??? and why now,?
 
Kama mahakamani wameshindwa kuna uwezekano hawana facts za kutosha kuhalalisha kutokulipa kodi.
Mbona hakuna sehemu inaonyesha walienda mahakamani? Ili sakata mimi nilianza kuliona kwenye YouTube channels sijasikia kwenda mahakamani

Hiyo brief report ya shule inaonyesha breakdown ya expenses zao (hawana msamaha wa kila kodi wanalipa paye) na hakuna income zaidi ya ufadhili na wenyewe una cover operation costs tu; TRA wamechukua hiyo hela shule aiwezi jiendesha.

Kuna tatizo TRA hapo sio tu wanafunzi kukosa elimu, unapoteza ajira, paye za serikali, unaaribu supply chain, huko nako kuna ajira na kodi za serikali.

TRA needs sorting out
 
Sijui hii roho ya kishetani ya huyu Mhutu ni ya Shetani yupi...Wasukuma huyu Ibilisi mkataeni siyo ndugu yenu, jitu lifashisti na lijambazi kabisa lisione taasisi yoyote ina hela linavamia
 
Mbona hata juzi taarifa ya shule hii ilikuwemo kwenye magazeti ya TZ na ilielezwa vizuri tu imeanza lini mpaka shule ikafungua kesi Mahakama ya Rufaa na mara tu baada ga kushindwa kesi hiyo TRA wakachukua kodi zao kutoka kwenye akaunti zao za Benki. Kasome gazeti la Mwananchi la Jumanne mkuu utapata habari kamili.
OK ngoja nitafute upande wa pili labda kuna mzozo mwingine.

Hila it doesn’t look good kwa TRA kwenye ili so far maana niliona mkurugenzi wa Arusha yeye mwenyewe kapigwa na butwaa hajui ajibu nini wakati kazungukwa na wazazi.
 
Kuna kitu kinaitwa cross subsidisation. Unachukua wanafunzi wachache wenye uwezo halafu unatumia ada wanayolipa kuwalipia wale wasio na uwezo. Aidha, ninavyojua mimi ni kuwa kodi inatakiwa kutozwa kwenye faida na sio mapato. Hata kwenye shule ambazo za kibiashara hauwezi kudai kodi kubwa kwa sababu tu ada yao ni shilingi milioni tano kwa kila mwanafunzi bila kuangalia gharama zao za uendeshaji kama mishahara ya walimu, vifaa vya masomo, usafiri, umeme, maji n.k. Kwa hiyo kabla ya kuwa shuku hawa kwa kosa la money laundering unatakiwa kupitia vitabu vyao. Na ukikuta kuwa wanapaswa kukulipa basi unakaa nao kuangalia namna gani wanaweza kukulipa bila kuathiri utoaji wao wa huduma hii muhimu. Ni vigumu sana kufidia siku ambazo wanafunzi watapoteza ikiwa shule itaendelea kufungwa. Busara ilitakiwa kutumika kabla ya kuwafungia account yao.

Amandla...
Hiyo cross subsidisation haipo hapo....kwani SHULE INAFADHILIWA NA WAAUSTRALIA...watoto hawatakiwi kulipa SUMNI KIPANDE.......

Ada inayolipwa "kinyemela" ndiyo INAYOULIZWA...na hapa ndipo ilipo HOJA mkuu....
 
Back
Top Bottom