Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kama serikali ina uwezo wa kwenda bank na kuchukua fedha kwenye account ya mtu bila idhini, bila shitaka na mahakama kutoa kibali, hapo ni shida kubwa.

Halafu katika mazingira hayo utegemee wawekezaji kuja kweli?
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Mitano tena.
 
What is it to you mbona CCM yenu inakula pesa zenu mnakenua.Acha roho mbaya.Ukweli unabaki kwamba ST Jude ni moja kati mradi bora kabisa tukiuharibu kama taifa kwa sababu ya upuuzi wetu tutakuwa ni wajinga sana.
Tatizo lenu mmekalia kila kitu kupinga pinga tu. Hata serikali ikikupa milioni 100 utapinga pia, kwa sababu ni CCM.

Mimi sizungumzii kwa upenzi wa chama nazungumzia uhalisia wa mambo. Jaribu siku moja na wewe uwe mhalisia utaona raha yake.
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana.

2. Shule hii inategemea misaada ya wahisani kwa asilimia 100 amabpo aslimia 90 inatoka kwa wahisani wa Australia.

3. Shule ina usajili wa wa shirika lisilo la kiserikali na ina jumla ya shule tatu zilizosajiliwa; Shule ya msingi (Na. AR. 02/7011), Shule ya Sekondari ya Wasichana (Na. S. 5243) and shule ya sekondari ya Bweni wavulana wa O-level na mchanganyiko A-level (Na. S. 4262). Shule ilipewa tamko kuwa ni shule ya ufadhili kupitia cheti S/Na. 53.

4. Shule inatoa ajira kwa zaidi ya watanzania 300 na wageni waajiriwa nane. Zaidi ya asilimia 60 ya uongozi wa Shule ni watanzania.

5. Shule pia inawasaidia wahitimu 326 kusoma elimu ya juu kwenye vyuo vikuu na vyuo vya kati vinginevyo.

6. Tarehe 3 Novemba 2020, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliondoa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 500,000,000 kwenye akaunti za Shule.

7. Tarehe 4 Novemba, Mwenyekiti wa Bodi wa wafadhili wa Australia (amabao ndio wanaifadhili bajeti ya mwaka ya shule kwa asilimia 90) aliandika kutujulisha kuwa Bodi haitaweza tena kutuma fedha zozote kwenye shule maana hawawezi kutoa ufadhili kulipa kodi za TRA. Badala yake wanataka kufadhili elimu tu ya wanafunzi wa Kitanzania.

8. Kwa sababu hiyo, St Jude ina uwezo mdogo sana wa kifedha na haiwezi kujiendesha kama kawaida.

9. Bajeti ya shule kwa mwaka 2020 ni Shillingi za Kitanzania 12,682,710,722. Kila mwaka, shule inarudisha bajeti nzima kwenye uchumi wa Tanzania kwa kutumia asilimia 100 ya matumizi ndani ya Nchi. Kwa ufupi jedwali linatoa picha ya matumizi kwa baadhi ya maeneo muhimu sana kama ifuatavyo:

....... see attach for more
Huu ni upande mmoja wa habari
 
Mtoto WA dada keshachungulia mabilioni yanavyoingia kutoka Australia. Mate yanawatoka yeye na mjomba wake.
 
"Kuna NGO za ovyo,mheshimiwa waziri niliyekuteua kashughulikie"- Chattle Boy
Nchi hii imekaa kukamia kamia tuu.
 
Corporate tax kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi wao.

Wako watoto wanaosomeshwa kwa kulipiwa ilihali the school is pure free for have not ...sasa hizo pesa zinazolipwa?!!!

Tungoje tuone wakijibiwa na serikali yao adhimu inayodhamiria ukweli na haki.

Samahani ukipata kichwa chako bas ukitumie kaka kuandika
 
Elimu kwa Watanzania ni jukumu na kazi ya Serikali JMTZ na siyo Mzungu wa sijui Australia, kwani huko kwao hana matatizo ? .
Hujui umuhimu wa NGO hawa ni development partners

Wadau wa maendeleo kwenye huduma za kijamii wapo kila sekta muhimu sana kwa nchi yoyote hasa maskini
 
Labda kashawishiwa na chuki dhidi ya wafadhili wa kizungu bila kuona impact kwa jamii hasa kwenye kutatua kero na changamoto ya Elimu
 
Hayo ni maelezo ya utetezi ya upande mmoja na kiuhalisia hayajitoshelezi kabisa

Tusubiri maelezo au hoja kutoka TRA ili tuweze kuelewa nini kinachoendelea.

Shule ya School of St Jude WanaJambo Lao!
 
Inaelekea umekariri au kukaririshwa kauli za wanasiasa. Hii ni shule iiyoanzishwa na mama raia wa Australia kusaidia watoto maskini kupata elimu. Watoto zaidi ya 2000 wa msingi na sekondari wanasoma, kuvalishwa na kulishwa bure, bila kulipa hata senti moja, vijana zaidi ya 300 kutoka kaya hizo hizo wanalipiwa karo na stipend kusoma vyuo vikuu na vyuo vya kati bila wazazi wao kugharimia. Sasa wewe unazungumza kodi gani. Yaani wananchi wa Australia wajitolee kusomesha Watanzania kupunguzia Serikali/TRA mzigo wa kugharimia elimu halafu Serikali iwatake wahisani wanaoisaidia kugharimia elimu kulipa kodi!

Soma hiyo attachment utaelewa kinachojadiliwa. Tafadhali usikariri wa kukubali kukaririshwa.
Huyo mama ajitoe.

Serikali izibe pengo lake.
 
YANI NYIE ST JUDE RUDINI TU MPATANE NA SERIKALI, HAKUNA MTU MWINGINE WA KUWASAIDIA ....JAMII FORUM, WAZAZI KWA MKUU WA MKOA, BARUA, ETC, ALL THIS WILL NEVER HELP, RUDINI HUKO HUKO MUELEWANE!
Mwenye shida ni mmiliki wa St. Jude au mzazi mwenye mtoto anaesoma?

Manake wamiliki wanaweza kufunga mahesabu na kuhamia Sudani Kusini nyie mbaki na umasikini wenu.
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana...
Mmefanya vizuri sana kuwasaidia Watz.

Lakini je, katika haya yote mlijitahidi kucomply na Sheria za kodi?

Mfano ninyi ni Purely Charitable Organisation, je mlipata Ruling toka kwa Commissioner General-TRA ili kupata hii status ya Charitable Organisation na ninyi kuandaa hesabu zenu kwa mujibu wa taratibu MAALUM ambazo hutumiwa na CHARITABLE ORGANISATION?

Na Je, baada ya kufanyiwa Audit mwaka 2012 na kupewa zile Assessment mbili ambazo zilionyesha mna malimbikizi ya kodi, mlitumia njia gani kutafuta Suluhu na TRA?

Ni jambo gani liliwazuia kufika muafaka na TRA toka Mwaka 2012 mlipo anza vurugana mpaka mkaenda TRAB, TRAT na mwisho CAT ambako kote huko mlikuwa mnashindwa jitetea na mwisho mka amriwa MLIPE KODI?

Nisaide katika hili Mkuu.
 
Kuna Kampuni moja inaitwa simgas ya waholanzi, wao walikuwa wana mradi WA kuwatengenezea gesi Shamba ( biogass) kwa Shule Za vijijini kwa msaada ambapo Shule husika haichangii hata 100 kuanzia Mwanzo na hata marekebisho ikitokea Tatizo kwenye mtambo Kampuni inapeleka fundi kwa gharama zake, nao walifanyiwa hivi wazungu wakafunga mradi mitambo imekufa, wafanyakazi hawana kazi, sasa wamehamia Kenya wanaendelea na maisha, hela yako Utoe msaada Bado usumbuliwe.
 
Wakiwamaliza hao wembe utahamia kwa wale wafanyakazi waliokua wakifanya biadhara then wakazifunga bila kutoa taarifa TRA ili kusimamisha TIN namba zao. Kupitia TIN namba walizo submit watauona moto. Unakuta mtu alifunga biadhara yake tangu 2016 na hakutoa taarifa ya kusitishwa TIN namba yake, kodi atakayo kuta anadaiwa atafurahi na mungu wake na lazima waichukue kwenye account yake atake asitake
Kama ipo sasa hiyo pesa kwenye account, kama hakuna si afadhali watunyonge sasa! Haaaaa anyways ukifunga TIN toa taarifa kwa barua.
 
Back
Top Bottom