Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Ok tunaamu kuamini tunachoamini.Mimi najua kwamba tunahitaji shule nyingi sana kama za ST.Jude ila taifa letu liinuke.Kama wewe huamni basi lazima utakuwa una matatizo yako mengine.
Yupo kwenye system hyo, anakula mema ya nchi watoto anasomesha feza.
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana.

2. Shule hii inategemea misaada ya wahisani kwa asilimia 100 amabpo aslimia 90 inatoka kwa wahisani wa Australia.

3. Shule ina usajili wa wa shirika lisilo la kiserikali na ina jumla ya shule tatu zilizosajiliwa; Shule ya msingi (Na. AR. 02/7011), Shule ya Sekondari ya Wasichana (Na. S. 5243) and shule ya sekondari ya Bweni wavulana wa O-level na mchanganyiko A-level (Na. S. 4262). Shule ilipewa tamko kuwa ni shule ya ufadhili kupitia cheti S/Na. 53.

4. Shule inatoa ajira kwa zaidi ya watanzania 300 na wageni waajiriwa nane. Zaidi ya asilimia 60 ya uongozi wa Shule ni watanzania.

5. Shule pia inawasaidia wahitimu 326 kusoma elimu ya juu kwenye vyuo vikuu na vyuo vya kati vinginevyo.

6. Tarehe 3 Novemba 2020, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliondoa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 500,000,000 kwenye akaunti za Shule.

7. Tarehe 4 Novemba, Mwenyekiti wa Bodi wa wafadhili wa Australia (amabao ndio wanaifadhili bajeti ya mwaka ya shule kwa asilimia 90) aliandika kutujulisha kuwa Bodi haitaweza tena kutuma fedha zozote kwenye shule maana hawawezi kutoa ufadhili kulipa kodi za TRA. Badala yake wanataka kufadhili elimu tu ya wanafunzi wa Kitanzania.

8. Kwa sababu hiyo, St Jude ina uwezo mdogo sana wa kifedha na haiwezi kujiendesha kama kawaida.

9. Bajeti ya shule kwa mwaka 2020 ni Shillingi za Kitanzania 12,682,710,722. Kila mwaka, shule inarudisha bajeti nzima kwenye uchumi wa Tanzania kwa kutumia asilimia 100 ya matumizi ndani ya Nchi. Kwa ufupi jedwali linatoa picha ya matumizi kwa baadhi ya maeneo muhimu sana kama ifuatavyo:

Matumizi ya Kila Siku TZS 35,229,752
Matumizi ya Mwezi TZS 1,056,892,560
Matumizi ya Chakula kwa Mwezi TZS 74,167,771
Matumizu ya Usafiri kwa Mwezi TZS 26,133,418
Mishahara ya Wafanyakazi na kodi za msingi kwa mwezi TZS 550,674,024

10. Shule kwa sasa ina kiasi cha TZS 5,777,658.40 kilichobaki kwenye akaunti ambayo ni sawa na tone dogo la maji katika bahari kwa matumizi ya siku moja ikiwa shule ingekuwa inajiendesha kama kawaida.

11. Tarehe 10 Novemba shule ilitoa mpango wa malipo kama ilivyoombwa na Kamishana Mkuu wa TRA, kwa ajili ya kuainisha namna ambavyo deni litalipwa. Katika mpango huo, shule iliatoa uwezekano wa kuchangisha familia zenye watoto shuleni, mpango ambao ungeondoa dhana ya kwamba tunatoa elimu bure kwa asilimia 100. Hata hivyo hadi hivi leo, shule haijapokea majibu kutoka ofisi ya Kamishina wa Mapato ya Ndani ya TRA.

12. Bodi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Tanzania, Bodi tatu za shule na Afisa Elimu- Arusha walikutana tarehe 13 Novemba na kwa pamoja waliamua kutoa kipaumbele kwa pesa zilizobaki kwa wanafunzi wanaotakiwa kufanya Mitihani yao ya Taifa. Wanafunzi wote ambao hawana mitihani walirudishwa nyumbani tarehe 18 Novemba.

13. Katibu Tawala na Afisa Elimu – Arusha wamekuwa wakipewa taarifa kila mara kadiri mambo yanavyokuwa.

HADI KUFIKIA TAREHE 1 DISEMBA 2020:

1. Wanafunzi wote kuanzia shule ya msingi (Na. AR. 02/7011) wapo nyumbani. Wanafunzi wa Kidato cha nne wa shule ya sekondari ya wasichana (Na. S 5243) na shule ya sekondari (Na. S 4459) wanamalizia mitihani yao ya Taifa na watarudi majumbani siku ya tarehe 8 Disemba. Wanafunzi wa kidato cha 6 kwenye shule ya sekondari (Na. S 4262) wanategemea kufanya mitihani yao ya Mock na watarudi majumbani tarehe 14 Disemba mpaka hapo watakapojulishwa.

2. Wanafuzi watakosa siku 40 za masomo kwa Muhula wa pili na Ripoti za mwisho wa Muhula hazijatolewa bado.

3. Kutokana na ukosefu wa fedha, shule inajiendesha katika upungufu mkubwa kama ilivyoainishwa hapo chini:

Hali ya KawaidaUpungufu wa kujiendesha kwa Mwezi December
Jumla ya wafanyakazi30762 wanao fanya kazi sasa, upungufu wa asilimia 80 ya uendeshwaji katika hali ya kawaida
Mishahara na malipo ya Msingi ya mweziTZS 550,674,024Wafanyakazi 199 wapo kwenye likizo bila malipo kwa sababu shule haina fedha ya kulipa mishara ya mwezi wa Disemba
Kodi za wafanyakazi (PAYE) na michango mingineTZS 163,766,559 (Oktoba) TZS 171,588,427 (November)Tumeshindwa kulipa TZS 335,354,986 ambayo ni jumla ya kodi za Oktoba na Novemba
Wafanyakazi waliopunguzwa/ Mikataba iliyoshindwa kuhuishwa0 staffWafanyakazi 101 wamepunguzwa/ kunyimwa mikataba mipya (sawa na 1/3 ya wafanyakazi wote)


4. Shule pia inaatoa misaada kwa wanafunzi 326 walio kwenye vyuo 53 ambavyo asilimia 95 vipo Tanzania. Tumeweza kulipia asilimia 5% tu (TZS 76,459,000) ya bajeti nzima ya elimu kwa wanafunzi hawa. Jumla ya bajeti kwa mwaka 2020-2021 ni TZS 1,786,671,100 ambayo inajumuisha ada, malazi, chakula, vifaa muhimu, usafiri, na vitabu. Kati ya wanafunzi hawa, wanafunzi 23 wanategemea kuhitimu shahada na astashada za Afya, mwaka 2021.

Gharama za Mwaka kwa Wanafunzi 326Malipo yalihitajika Tarehe 16 Novemba
AdaTZS 490,006,100
Fedha ya kujikimuTZS 892,425,000
MalaziTZS 293,400,000
UsafiriTZS 45,640,000
Vifaa muhimuTZS 65,200,000
Jumla ya gharama:TZS 1,786,671,100
Kiasi kilicholipwa (Asilimia 5%):TZS 76,459,000
Gharama iliyobaki ikiwa haijalipwa:TZS 1,710,212,100


5. Shule imefanikiwa kuchagua wanafunzi 340 kutoka kwenye shule za serikali kujiunga na shule zetu mnamo Januari 2021. Hata hivyo, wanafunzi hawa hawataweza kupewa ufadhili huu wa kimasomo kama hali itabakia hivi ilivyo sasa.

6. Shule ina wahitimu 116 waliomaliza Kidato cha 6 wanaojitolea kufundisha masomo mbalimbai kwa mwaka mmoja kwenye shule 34 za serikali. Wahitimu wote 116 pia wamepewa likizo bila malipo hivyo hawajaweza kupata fedha ya kujikimu ya Shillingi 170,000 kila mmoja, fedha inayowasaidia kugharimu chakula na usafiri kwa mwezi.

7. Shule imeshindwa kulipa zaidi ya watoa huduma 50 kwa mwezi wa Oktoba na Novemba 2020 kiasi cha shilingi 68,997,205.

8. Wanafunzi 90 wanaohitaji msaada zaidi ya elimu hawatapokea msaada wa mwisho wa mwaka wa chakula, sabuni na vifaa vingine vya muhimu vya nyumbani.

9. Wafanyakazi wote 101 waliopunguzwa au kunyimwa mikataba mipya wana haki ya kulipwa mishahara na marupurupu ya mwisho, lakini shule haijajua bado fedha hizi zitatoka wapi.

10. Walinzi 25 wanatakiwa kuendelea kufanya kazi ili kuhakikisha ulinzi wa shule zote tatu, hivyo kupaswa kulipwa mishahara yao, hata hivyo, shule haijajua bado fedha hizi zitatoka wapi.

11. Shule haina fedha kulipa deni linalotajwa kwakuwa haina kipato wala njia ya mapato, zaidi ya zawadi na misaada inayotolewa na wafadhili ili kuendesha shule. Wahisani hawako tayari kutoa fedha ili kulipa deni hili maana kufanya hivyo kunakinzana na sababu ya kujitolea kwao.

12. Ikitokea TRA hawatarudisha fedha waliyochukuwa na kuendelea kuidai shule kodi iliyobaki, shule haitakuwa na chaguo lingine isipokuwa kuifunga kabisa na wanafunzi wote wa vyuoni watalazimika kurudishwa nyumbani.


Wacha kufanya conclusion kwa kutmia hisia zako. Ni vema ukaskiliza maelezo ya serikali then ukaskiliza na St.Jude then ukabalance! Mpaka hii decision imefikika its obvious ni kitu kimefuatiliwa muda mrefu, who knows kuna watu wanaitumia St. Jude kama njia ya kusafisha pesa zao walizoiba? Busara ni kuskiliza kote kote kama acacia walivopandwa kichwani kumbe walikua wezi wakubwa
 
Hivi kuna Charity hadi zinalamba billions kuendesha mambo yao ! Hapo lazima kuna kitu hatukijui
Kama umewahi kuandika proposals za donor funding fuatilia sources za funds kwa watu kama Policy Forum, LHRC (kituo cha sheria na haki za binadamu,
Twaweza,
Haki elimu,
Mtandao wa haki za binadamu (Human rights defence coalition)
TGNP,
Foundation for Civil Society
Media Council of Tanzania
Hao wote wanapokea billions of cash toka nje au ofisi za kibalozi kwa non-profit activities.

Issue ya shule kupokei bil 1.7 is a peanut;
Nadhani TRA kwa kuwa inataka PAYE; sio sawa kuchukua fedha operations ya shule juu kwa juu bila kujua namna shule itajiendesha.
 
Wakati Mwingine tunapenda kulaumu mno bila kujua UNDANI WA MAMBO....

Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia watanzania...kwani na hao wanaoiendesha ni watanzania hawahawa....

Si kila wakati serikali inafanya mambo KUKIFAIDISHA CHAMA TAWALA......
 
Kama umewahi kuandika proposals za donor funding fuatilia sources za funds kwa watu kama Policy Forum, LHRC (kituo cha sheria na haki za binadamu,
Twaweza,
Haki elimu,
Mtandao wa haki za binadamu (Human rights defence coalition)
TGNP,
Foundation for Civil Society
Media Council of Tanzania
Hao wote wanapokea billions of cash toka nje au ofisi za kibalozi kwa non-profit activities.

Issue ya shule kupokei bil 1.7 is a peanut;
Nadhani TRA kwa kuwa inataka PAYE; sio sawa kuchukua fedha operations ya shule juu kwa juu bila kujua namna shule itajiendesha.

Tusubiri maelezo ya serikali kwanini wamefunga na wameona nini chenye wasiwasi, kupokea 1.7B kila mwezi constantly kwa miaka yote ile nadhani hata uchumi wa Tanzania unaingia kwenye inflation and as a bonus bado hulipi kodi
 
Hicho ndio kiini chenyewe.
Watu wengi Arusha wanajua kisa kilianzia siku Magufuli alipokuja Arusha kwenye kampeni na waendeshaji wa shule ya St. Jude wakagoma kuswaga wanafunzi wake kwenda Sheikh Amri Abeid kuongeza idadi ya wahudhuriaji kwenye mkutano wa CCM.

Wamiliki wa shule waliweka wazi kuwa, shule yao haina itikadi yoyote ya vyama vya siasa, uongozi wa shule haukuwa na mamlaka ya kuwahusisha kwa lazima wanafunzi wake kwenye itikadi za vyama na mwisho uongozi wa shule hauwezi kuhahakisha usalama wa wanafunzi wake kwenda uwanjani.

Yote kwa yote, chuki ya serikali ya Magu dhidi ya ukanda wa Kaskazini ni kubwa mnoo, St. Jude huenda ni miongoni mwa taasisi za Elimu zilizokuwa zinawindwa kuangamizwa kwa muda mrefu sana, maana ni miongoni mwa taasisi za mtaji wa kimaendeleo ya kijamii kwa kizazi cha watoto na vijana waliopo kanda ya Kaskazini.
Basi sawa shule ifungwe na kodi ilipwe haiwezekani shule ikawa na ubinafsi wa namna hii , inaonyesha wazi kabisa shule ipo kwa ajili ya Watu wa ukanda huo ,Kama ingekuwa ni ya watanzania wote wasingekutwa na ili jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa taasisi kubwa kama hii Tena inayotoa huduma bure bila faida hao TRA walipaswa watoe maelezo ya kutosha kwanini wamefreeze hizo pesa. Lakini kuchukua tu kimya kimya haijengi picha nzuri kwa wadau wa maendeleo nchini.
Haya shule haina uwezo wa kujiendesha na mfadhili amesema hawezi kufadhili TRA Bali anafadhili elimu kwa wasiojiweza. Je mkuu tunapata picha gani kwa statement hiyo ya mfadhili?
Picha tunayoipata hapo kwa mfadhili ni kuwa mfadhili ameshtuka kuwa uongozi wa shule ulikuwa unakula pesa za kodi halafu kwenye mahesabu wanaripoti kuwa kodi imepelekwa serikalini.
 
Ndg kuwaabia watu mazezeta ni kutokuwa na elimu ya kodi ,tofauti kati ya shule hii na shule zingine ni source of revenue (chanzo cha mapato),shule zingine wazazi/walezi wanalipa ada ,kwenye shule hiyo gharama zipo wazi kabisa ,serikali inachotaka ni asilimia kadhaa ya faida wanayopata ,mapato ukitoa matumizi ,ndg serikali kwa hili haijamuonea MTU
Kuna watu au kikundi cha watu kinachofaidika na ziada kama ipo? Mfano kama ziada ni 1,000,000 serikali ikichukua 300,000 inayobaki 700,000 nani anaifaidi?

Kama jibu lako ni HAKUNA maana yake hiyo shule haifanyi biashara.
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Umenena Vyema Naona Kama inatafutwa huruma ya Umma.

Maelezo hayatoshelezi Non Profit Organisation inadaiwaje kodi?
Ikiwa ni kweli inadaiwa ni kiasi Gani? Na ilikuwaje hadi malimbikizo ya kodi yakawa makubwa Hivyo?
 
Mbona naona kama sinema tu; ni kama aliyokuwa anaongea Lissu kwenye kampeni juu ya TRA kukusanya fedha moja kwa moja toka benki
 
Back
Top Bottom