Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Siamini kama Serikali inaweza tu kufanya uonevu wa kuwalipisha hiyo kodi bila kuchunguza,shule nyingi za private za kidini zipo business oriented Ila hujificha kupitia kivuli cha misaada wanayoitoa kwa baadhi ya wanafunzi
MimI naamini wanaweza kufanya hivyo hasa ukizingatia mzee anawachukia sana watu wa kaskazini
Inawezekana sana ingekuwa hiyo shule ipo kanda ya ziwa "kwa wapiga kura wake" isingefungwa.

Hapa ishu ni kukataa kuwavalisha wanafunzi kijani na kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya CCM.
 
Hauna akili..
 
Hii post nitaisoma tena kesho... Naona kuna vitu kadhaa muhimu kwa taaluma yangu
 
Hapa kuna ujaujanja wa kukwepa kodi ya serikali kwa kisingizio cha kusomesha watoto bure na ndio maana hataki kueleza mkasa mzima, TRA sio Machizi
 
Hakuna utaratibu kama huo katika sera za elimu ya tanzania, afuate miongozo ya elimu.
 
Ilikuwaje TRA walikanusha kuchota pesa kutoka kwenye akaunti bila idhini ya mwenye akaunti, benki husika lazima ieleze.
Kwa sasa TRA wanayo mamlaka ya kufunga akauti ya mfanyabiashara yeyote anayedaiwa na TRA wala benki haihusiki.
 
Ingekuwa vyema haya mambo yakashuhulikiwa bila kumuathiti mwanafunzi mtoto wa mtanzania maskini
 
Inasikitisha sana, 2000+ ni wanafunzi wengi sana hii inaadhiri moja kwa moja familia nyingi za watanzania na TRA na wamekosea kwenye timing n at least wangefanya hivi wakat wa likizo ili isiathiri moja kwa moja masomo ya wanafunzi waliowengi
 

Sema shule ingekuwa kanda pendwa isingefungwa.
 
TRA kuchukua pesa kuna jambo ambalo haliko sawa. Shule iweke ukweli nini kinaendelea pale shuleni, haiwezekani TRA wafumuke tu na kujitwalia pesa wana sababu nzuri tu kama sikosei, kama hazipo mleta mada pamoja na shule waende mahakamani wakawashitaki TRA. Tena watalipwa na fidia juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…