Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Kama ni Wafuatiliaji wazuri wa siasa za nchi hii mtakubaliani nami na ukweli kuwa Dkt. Slaa amekuwa na Udini mkubwa sana ndani ya kifua chake. Amekuwa na chuki binafsi sana kila inapotokea utawala uliopo madarakani ni wa upande wa pili yaani Uislamu. Amekuwa ni mtu mwenye chuki, vurugu na mzushi wa masuala mbalimbali ili kuwachafua viongozi wetu hasa Rais pamoja na kumchonganisha na Wananchi.

Unaweza muangalia Dkt Slaa wa wakati wa Mheshimiwa Kikwete, wakati wa Hayati Dkt Magufuli na wakati huu wa Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan. Utagundua ya kuwa anaongozwa zaidi na Udini pamoja na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais.

Hali hiyo imempa upofu wa akili na macho katika kujadili hoja. Ndio sababu unaona anakuwa akizusha mambo mbalimbali ya uongo na uchonganisha kwa lengo la kutaka kuifanya serikali ichukiwe na wananchi. Jiulize kama umewahi kumuona au kumsikia Dkt Slaa akikosoa kitu chochote kile katika utawala uliopita. Unafikiri ni kwanini? Jibu ni Udini tuu ndio muongozo wake. Ndio maana kwa Udini wake yupo tayari kuzusha lolote na kusema uongo wowote ule ili serikali ichukiwe na kuleta taharuki pale inapokuwa ikiongozwa na muislamu.

Lakini ni huo huo Udini wa Dkt Slaa anaweza kufumbia macho kitu chochote kile na kutetea kila jambo ikiwa tu ni wa upande wa Dini yake. Ndio maana katika uzushi anaoongea huwezi ukaona akiweka ushahidi wa aina yoyote ile mezani kuthibitisha madai yake ya uzushi na uongo. Hawezi akaweka nyaraka yoyote ile kuthibitisha maneno yake.

Watanzania tunapaswa kumpuuza na kukataa kabisa kuingia katika mtego wa Dkt Slaa wenye lengo na ajenda ya chuki binafsi na Udini kwa kutunga vitu vya kizushi na uongo. Tumkatalie zidi ya ajenda zake chafu za kumchafua Mheshimiwa Rais na tumkemee kwa nguvu zote. Tumwambie kama ana ushahidi wa lolote lile anapokuwa akizungumza hadharani basi atuwekee kwanza ushahidi.

Napenda kumalizia kwa kusema kuwa dkt Slaa hata fanikisha ajenda zake za Udini na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais, na wala hatafanikiwa kumchafua kwa namna yoyote ile kama ambavyo amekuwa akifanya jitihada za kutaka kumchafua Rais wetu na kumjengea taswira mbaya kwa wananchi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Lukasi hebu jaribu mara moja moja kutumia kichwa kwa kufikiri we jamaa. Kazi ya kichwa sio kabati la kutunzia meno
Mshaurini dkt Slaa aache Udini na chuki binafsi kwa Mheshimiwa Rais. Embu nikuulize swali hilo. Je umewahi kumsikia Dkt Slaa akikosoa chochote kile katika utawala uliopita?
 
Wazazi waliuza ng'ombe ili wapeleke ng'ombe ingine shule. Sad story
Tunahitaji mtu wa kukosoa mambo kwa hoja na ushahidi na siyo mtu anayeonekana kuongozwa na Udini pamoja na chuki binafsi. Dkt Slaa amekuwa mtu wa kusukumwa chuki binafsi na Udini.ndio maana hajawahi kuonekana akikosoa chochote kile katika utawala uliopita.
 
Acha ujinga mama kizimkazi ndo mdini.
Mheshimiwa Rais hajawahi kuwa mdini wala kumbagua mtu kwa misingi ya aina yoyote ile. Lakini dkt Slaa amekuwa na chuki kubwa sana na utawala huu tangia uingie madarakani. Kinachomsumbua ni Udini na chuki binafsi tu ndio maana amekuwa akizusha vitu vya uongo na uchonganisha kwa lengo la kumchafua Mheshimiwa Rais
 
Mheshimiwa Rais hajawahi kuwa mdini wala kumbagua mtu kwa misingi ya aina yoyote ile.lakini dkt Slaa amekuwa na chuki kubwa sana na utawala huu tangia uingie madarakani.kinachomsumbua ni Udini na chuki binafsi tu.ndio maana amekuwa akizusha vitu vya uongo na uchonganisha kwa lengo la kumchafua Mheshimiwa Rais
Alafu usikute wewe ni mwalimu 😂😂😂
 
😂 😂 😂
Nguvu ya buku 7 za Lumumba mbona atajuta na alishakula kiapo cha uaminifu yaani jamaa kashakuwa mtumwa wa fikra zake. Unamdhalilisha sana muumba wako aliyekuwa akili timamu
Lucas Mwashambwa
Watanzania hatuwezi kuunga mkono na kumfumbia macho mtu anayeleta habari za Udini na chuki binafsi kwa kuzusha vitu vya uongo na uchonganisha kwa maslahi yake binafsi na genge lake.
 
Back
Top Bottom