Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Kinachomsumbua Dkt. Slaa ni udini na chuki binafsi kwa Rais Samia

Huo ni mtazomo wako wa kichawa na pia kutokana na uduni wa akili,yaani Samia atumie mabilioni ya kodi zetu kumfadhili Sultan Mbowe halafu watu wake kimya tu.
Huo ushahidi wa hayo Mabilioni upo wapi ewe Mropokaji? Kazi yako ukurupukaji tu na Uropokaji kama mlevi wa gongo
 
Sahihi kabisa, kipindi cha Mwendazake hakuwahi kuwa na chuki kiasi hichi..picha lilianza kwenye sakata la DP world nadhani iligusa maslai ya kanisa mzee hakupendwezwa!
 
Kwa hiyo kama alikuwa hakosoi kipindi cha magu basi aendelee kukausha au sio?

Hivi nyie maccm akili zenu huwa mna muachia mwenyekiti au mbona hamna mwenye ahueni pamoja na huyo mwenyekiti wenu.
Unaweza kuweka ushahidi wa uzushi na uongo anaozungumza?
 
Ndugu zangu Watanzania,

Napenda kuwaambieni ya Kuwa Dkt. Slaa siku zote na wakati wote tangia kuingia kwa Rais Samia madarakani amekuwa na chuki kubwa sana na Rais wetu.

Amekuwa na hasira kubwa sana kifua pake kusema ni vile tu hana uwezo wa kikatiba wala kisheria wala nguvu ya aina yoyote ile ya kuweza kumtoa Rais wetu madarakani.

lakini kama angekuwa na Uwezo basi asingependa pengine hata kuona Rais Samia akiapishwa kuwa Rais wetu tangia siku ile ya tarehe 19-3-2021.

Na msingi wake mkubwa wa kumchukia RAIS wetu ni chuki binafsi pamoja na Udini tu uliomjaa kifuani pake. Muangalie na kumfuatilia dkt slaa wa wakati wa hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Dkt slaa wa wakati huu.

Je, Mumewahi kuona dkt slaa akifungua mdomo wake kukemea au kukosoa chochote kile wakati wa awamu ya Tano? Mnafikiri kwanini?

Jibu ni Udini tu ndio msingi wake Mkuu hasa kwa kuzingatia historia yake ya wapi ametokea na kuhudumu ndani ya kanisa kwa muda mrefu.

Dkt slaa Kwa chuki zake binafsi kwa Rais wetu na udini wake umempelekea kuwa Muongo, Mzushi, mfitini na mtu wa kuzusha na kuleta taharuki tu kwa watu.

Amekuwa ni mtu anayetamani mabaya tu yatokee na kutamalaki katika utawala huu wa awamu ya sita ili moyo wake ufurahie na apate cha kuongea.

Amekuwa ni mtu wa kuongea na kuzusha uongo usio na ushahidi wa aina yoyote ile zaidi ya kujiongelea tu. Ni huyu huyu Dkt Slaa akiwa kwenye mkutano mkoani Mbeya amewahi kuzusha uongo na uzushi kuwa kuna gari linaingiza maboksi ya kura feki lakini baadaye ikaja kufahamika kuwa aliongea uongo na uzushi mkubwa sana wenye kuleta tu taharuki kwa umma.

Dkt slaa amekuwa na hasira kubwa sana na chuki kubwa sana kila inapotokea utawala uliopo madarakani ni wa upande wa pili ambao siyo wa dini yake. Ni wakati wa kumkemea hadharani na kumwambia kamwe watanzania hatutakubali wala kumuunga Mkono uzushi na uongo wake usio na ushahidi wa aina yoyote ile. kwa sababu tunatambua anaongozwa na Udini na chuki binafsi tu katika kauli zake dhidi ya RAIS wetu.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Slaa hapendi Rais asiyekuwa wa Dini yake
 
Dkt slaa ni daktari wa nini?
Wewe darasa la 7 ulifaulu?

Samia ni Dr wa nini?

Hii hapa CV ya Dr Slaa kasome uone ni Dr wa kitu gani.

 
Back
Top Bottom