Kinachopelekea wanaookoka au kusilimu na kuwa swala tano kufeli kimaisha

Hivi unadhani Mungu hafurahi kuona kiumbe alichokiumba kinamsifu,kina mshukuru, kumtukuza na kumwabudu? Ikiwa tu wafalme wa duniani wanafurahi wanaposifiwa na kutukuzwa, vpi kwa MUNGU ambaye ni mmiliki wa ulimwengu mzima??

Sisi viumbe ni watumwa wa Mungu, Mungu ndiye Bwana wetu, so ni lazima tunyenyekee kwake
 
Ur very right mkuu. Ibada inayo kubalika mbele za Mungu ni ibada ya shukrani. Una mshukuru kwa kukuumba kwa mfano wake
 
Ukitaka kumjua Mungu toka nje ya "kifungo cha dini" ndani ya kifungo cha dini huwezi kumjua Mungu wa ukweli hata siku moja..
 
Eti mtumwa wa Mungu. So Mungu na yeye ana watumwa?
 
Ukitaka kumjua Mungu toka nje ya "kifungo cha dini" ndani ya kifungo cha dini huwezi kumjua Mungu wa ukweli hata siku moja..
Ukimtoa Mungu katika sphere ya maisha yako ina maana wewe sio muumini wa MUNGU ila unaamini katika matamanio ya nafsi yako!

Uzuri Quran haijaacha kitu...Mungu anasema hivi

Quran 45:23

Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?
 
Maisha ya dunia si lolote... SASA unafanya kazi ili iweje kama maisha ya dunia si lolote. Kunywa sumu jiue ndo tujue upo serious una maanisha.


Yani Mungu ame design maisha ya mwanadamu for a period of one thousand years. Ameitengeneza dunia nzuri yenye kuvutia amekuleta kiumbe wake uje ufurahie maisha then malipo YAKO kwake ni kusema maisha si lolote. Are you serious?

Mimi nayapenda maisha na kika SIKU namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa maisha na kunileta duniani.


" Dunia tupo kujaribiwa" ni sentensi inayo mkufuru Mungu kwa kiwango cha stifler gorge. Ukisema duniani umekuja kujaribiwa tafsiri yake ni kwamba anae kujaribu hajui hutafanya nini endapo atakujaribu. Kwamba hajui mambo yajayo. Ndio unacho maanisha hiki.

Mungu hana interest yoyote na kukujaribu wewe kiumbe wake. And he cannot do such a stupid mission.

Hiyo kumjaribu mtu ni human character na sio divine character.
 

KWA hiyo unataka kusema nje ya Qur'aan binadamu hawezi kumjua Mungu ?
 
LIKUD wewe humuabudu Mungu bali unayaabudu matamanio ya nafsi yako. Unapokiri kuwa unamuamini Mungu lazima u-acknowlwdge his absolute will and power over you.

Mungu ameweka sets of laws and guidance kama unahitaji kuwa upande wake ni lazima uzifate na uzitii. Kama unafanya biashara basi ifanye biashara katika msingi ambao Mungu anautaka na kuuridhia! Usifanye biashara za haramu licha ya kuwa zinaweza kukuingizia pesa nyingi kwa muda mfupi, Usidhulumu watu katika vipimo na haki zao, Usile riba, usimdidimize mfanyabiashara mwenzio ili tu wewe uwe juu n.k

Ukisema unafuata akili yako tuu ni wazi kuwa maagizo ya Mungu utayaweka kando.
 
Jamaa haeleweki mara aseme yeye hana dini mara mfuasi wa mwanga halafu anaendaga msikitini kuswali ,inashangaza sana..

Yes masjid naenda kusocialize a jamaa zangu.

Kuwa mfuasi wa Mwanga sio dini. Naufuata Mwanga. Dini ni utumwa. Wewe endelea kuwa mtumwa wa dini. Mimi nimesha toka kwenye huo utumwa mkuu.
 
KWA hiyo unataka kusema nje ya Qur'aan binadamu hawezi kumjua Mungu ?
Kuna kumjua na kumuamini. 100% ya viumbe wote wanamjua Mungu. Hata hao atheists wanamkanusha midomoni tu ila deep down nyoyo zao zinajua kuwa yupo aliyeumba huu ulimwengu. Tunapokuja kwenye suala la wananaomuamini huwa ni la wachache tu. Kuamini maana yake ,you hear and obey!! Unajisalimisha (unaslimu) kuwa chini ya mamlaka na sheria za Mungu. So yes bila ya kupitia vitabu vitakatibu huwezi kumjua Mungu ukweli wa kumjua. Utaishia tu kutambua uwepo wake ila kujua anapenda na anachukia nini , hutoweza kujua mpaka usome habari zake kupitia maandiko matukufu.
 
Mimi sijajiumba mwenyewe mkuu. Nimeumbwa na Mungu. Hayo matamanio ya nafsi yangu ameniumbia Mungu. Kutafuta matamanio ya nafsi yangu sio jambo baya ni jambo zuri KWA sababu ndivyo Mungu alivyo niumba. Hata mfalme Suleiman anasema " Sikuyanyima macho yangu chochote yalichotaka waka Siku unyima mwili wangu chochote ulicho taka".

Bila " matamanio ya mwili" wewe usingekuwa una andika hapa. Ni matamanio ya mwili ndio yali mfanya baba ako akamjua mama ako kisha wewe ukazaliwa. Yaheshimu matamanio ya mwili mkuu
 
Yes masjid naenda kusocialize a jamaa zangu.

Kuwa mfuasi wa Mwanga sio dini. Naufuata Mwanga. Dini ni utumwa. Wewe endelea kuwa mtumwa wa dini. Mimi nimesha toka kwenye huo utumwa mkuu.
Wewe unaabudu matamanio ya nafsi yako as i said earlier!!

Mungu mwenyewe anatambua uwepo wa Dini, wewe ni nani useme huamini kuhusu dini?

Quran 3:19

Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na walio pewa Kitabu hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ujuzi, kwa sababu ya uhasidi ulio kuwa baina yao. Na anaye zikataa Ishara za Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhisabu
 

Binadamu ameishi duniani KWA miaka milioni saba. Qur'aan imeletwa miaka 1500 iliyopita. Hao watu walio ishi kabla ya Qur'aan walikuwa hawamjui Mungu?
 
Kati ya Mungu aliye niumba akanipa matamanio ya mwili na mimi mwanadamu ninae yatumia matamanio ya mwili kuifurahisha nafsi yangu nani mwenye makosa?
 
Kwa kweli una hoja ila heading umekosea ila main body na conclusion iko vzr

Hi la kuwa na nguvu za kiungu ndani yangu nililiona Hilo kitambo ila sijalifanyiaa kazi

Je sas kwa andiko hili unatka kutukataza kwenda kanisa na kushikiri katk sikuu za mafuno ianenda kuazimishwa October 31
 
" Ukisema unafuata akili yako tu ni wazi maagizo ya Mungu unayaweza kando" Maagizo ya Mungu yapi hayo? Na nani alikwambia hayo ni Maagizo ya Mungu?
 
Binadamu ameishi duniani KWA miaka milioni saba. Qur'aan imeletwa miaka 1500 iliyopita. Hao watu walio ishi kabla ya Qur'aan walikuwa hawamjui Mungu?
Quran 35:24


"Hakika Sisi tumekutuma wewe (Muhammad) kwa Haki, kuwa ni mbashiri na mwonyaji. Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao"


Kabla ya Quran vipo vitabu vilitangulia kama Taurati, Zaburi na Injili na hakuna umma wowote isipokuwa Mungu alipeleka muonyaji kati yao. Hakuna excuse kuwa Mungu hakupeleka Muonyaji ila alipopeleka muonyaji nini watu walifanya??

Quran 35:25

Na wakikukanusha basi walikwisha wakanusha walio kuwa kabla yao. Mitume wao waliwajia kwa dalili wazi wazi na kwa maandiko na Kitabu chenye nuru.
 
Kanisani nenda kwa ajili ya kusocialize na waamini wenzako lakini ukweli ukae nao kwenye nafsi YAKO kwamba Mungu amekupa kila unacho kihitaji. Nguvu za Mungu zipo ndani YAKO. Ukiamini katika hilo BASI utafanya kitu chochote unacho hitaji kukifanya hapa duniani. Hakuna jini wala mchawi wala sijui pepo atakae kubabaisha.
 
Mkuu wewe ni mlevi ujue? Wewe unanitajia vitabu vya juzi hivyo miaka 2000 iliyopita. Mimi nimekwambia watu walio ishi duniani miaka milioni saba iliyo pita...

Acha ulevi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…