Hope unamaanisha wewe ni mfano wa mungu unapozungumzia uumbaji, kwamba mwanadamu nae anaweza kuumba anapokutana na mwanadamu mwenzake [mke na mume].
Lakini ukumbuke, huu uumbaji wa mwanadamu, sio kama ule uumbaji wa Mungu, Mungu aliumba kwa kutumia neno, [alipomtuma malaika kumwambia Mariamu atapata ujauzito], wakati wanadamu wanaumba kwa kutumia miili.
Zaidi, unaposema Mungu alitupa mamlaka ya kuvitawala viumbe vyake, jiulize hayo ni mamlaka ya aina gani, matakatifu, au ya kishetani?
Kam kwa mfano, unapotaka kuchinja kuku. kwanza lazima umkimbize mpaka akichoka ndio umkamate ili umchinje, kama ungekuwa na mamlaka ya kitakatifu uliyopewa na Mungu kuku angekuheshimu ungemuita angekuja umchinje bila kumkimbiza, sasa iweje Mungu aseme kavitawale, halafu ukija huku mpaka umkimbize tena?
Kuna vitu hamvijui undani wake, mnachukulia mambo juu juu tu, na ndio mnadanganyana kwenye huu uzi, kwa kumuita mleta mada "genious"
Ndio maana nilikwambia you are still a learner.
U have got a very little and limited understanding about the ways of the God Almighty.
Maandiko yanapo sema dunia iliumbwa KWA neno la Mungu hayamaanishi kwamba Mungu alikuwa anatamka kisha vitu vinatokea kama mazingaombwe.
Hell No! Mungu sio mwana mazingaombwe mkuu.
Yana maanisha dunia iliumbwa KWA order kutoka kwa Mungu.
Yani Mungu ali design road map ya uumbaji na vile anavyo taka dunia, ulimwengu na vyote vilivyomo ndani yake viwe, kisha akatoa plan, instructions, permission na oda KWA viumbe wake( malaika) ambao tayari ndani yao alisha weka maarifa mbalimbali waka tekeleze huo mpango wa uumbaji.
Mfano aliposema na iwe mimea. Maana yake alitoa oda sasa tunatengeneza mimea, maana yake malaika wakusanye raw materials zote zinazo husika na.kutengeneza mimea kisha wafuate maelekezo KWA kufanya moja mbili tatu ili mimea itokee.
Nakadhalika nakadhalika.
Ni SAWA tunaposema Mkapa alijenga uwanja mpya wa taifa , hatumaanishi kwamba Mkapa ndio alienda kuchanganya cement pale taifa la hasha bali tunamaanisha Mkapa alitoa plan, oda, ruhusa na fund uwanja wa taifa ujenge.
Tunaposema Magufuli kajenga stendi ya Mbezi hatumaanishi Magufuli alienda Mbezi kumwaga zege nope Magufuli alitoa plan, fund oda na ruhusa stendi ya Mbezi ijengwe.
Vivyo hivyo kwa Mungu.
Mungu sio mwana mazingaombwe mkuu . Ni Mungu wa utaratibu kanuni na mipango.
Mwanadamu amekuwa designed and genetically engineered
Halafu Mungu ni Mfalme. He doesn't do things by himself he instruct his servants to do things for him