Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 1,015
- 2,493
Mlipuko wa Arab Spring ilianza kama masikhara nchini Tunisia baada kijana mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekosa kazi na kuamua kuuza matunda kwa kutumia toroli mitaani. Lakini alipokatiza mbele ya ofisi za Serikali kuuza matunda alizuiwa na kuadhibiwa kuwa anachafua mwonekano wa mtaa huo. Hasira ya kijana huyu alienda Petrol Station na kununua mafuta akarudi mbele ya ofisi ile ile na kujichoma hadharani.
Wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima wakapandwa hasira na maandamano nchi nzima kumtaka Rais aondoke ofisini. Upepo huu ukaenea nchi nyingi za Kiarabu na mapinduzi mengi yakafanyika na mauaji pia. Wengi walipoteza maisha kudai mabadiliko.
Leo kuna maandamano makubwa nchini Afrika Kusini na Kenya. Afrika Kusini yanaongozwa na Julius Malems (Juma) wa EFF na Kenya ni Raila Odinga wa Azimio la Umoja. Hofu yangu ni kwamba madai ya waandamanaji SA na Kenya yanafanana. Kupanda kwa gharama za maisha na utawala mbaya wa kifisadi.
Swali ni je, ni nchi ipi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ni salama katika madai haya? Jakaya Kikwete ametoa clip kumtetea Rais Samia, "mafuta yamepanda hata Uingereza hata wanamlilia gharama kupanda wangefanya nini kama sio unafiki?" Kwangu mimi huu ni utetezi wa kijinga sana maana ni yeye huyo huyo Kikwete aliwahi kuulizwa Kwa nini Watanzania ni masikini? Alisema, "hata mimi sijui". Leo atajuaje Kwa ni gharama za maisha yamepanda? Ushauri wake Kwa Samia ni kuwalambisha asali wapinzani Ili biashara zao zisiathirike Kwa maandamano.
Ninaamini upepo huu ulipoanza kuvuma kutoka J'berg hadi Nairobi utafika Dar es salaam, Kampala, Maputo nakadhalika na watawala wataadhibiwa. Asali isiwapofushe. Teteeni haki na Hali ya wanyonge wasio na sauti. Naomba upepo huo uvume tu kuja Tanzania kuondosha pengo kubwa kati ya walalanjaa na washibenjaa. Nani asimame na umma? Let's count the days ahead!