Kinachotokea Afrika Kusini na Kenya inaweza kuwa sawa na Arab Spring kwa nyingine za Afrika

Kinachotokea Afrika Kusini na Kenya inaweza kuwa sawa na Arab Spring kwa nyingine za Afrika

Ukweli mchungu sana, ni vigumu kuendea ukiwa vijana wengi kama Mathanzua Showmax Bukyanagandi
Ni Kenya na South Africa ndiyo wanaweza fanya hivyo. Nchi zingine vijana wengi hawana maarifa, ushinda kwenye vijiwe vya kahawa na kusoma magazeti ya udaku na conspiracy.
Ni vipi, utamshawishi kijana anae amini maandamano ni kazi ya CIA?.
Maadamno yakifanyika ujeruman, Uingereza ama marekani ni sawa. Ila yakifanyika Ribya, Misri inakuwa wamedanganywa wamedanganywa na Marekani.

Uwa ninafurahi sana kusikia watanzania wananyimwa visa ya kwenda nje especially kutafuta maisha ama elimu.
Imejin unapiga kura ccm, Kisha hutaki kuiwajibisha serikali yako pindi inapovuruga na haileti maendeleo then baada ya uchaguzi unatufa visa kwenda ulaya ama marekani ambako wanajenga nchi zao kwa damu, maandamano, kuiwajibisha serikali zao etc.
Wapo tayari kufia barabarani then we ndiyo unataka ukale matunda ya damu yao kiulani.
Kuna majitu yanadhani chumi za Ulaya, Asia na Amerika zilishuka toka mbinguni kama Mana wakati wa Mussa.
 
Mlipuko wa Arab Spring ilianza kama masikhara nchini Tunisia baada kijana mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekosa kazi na kuamua kuuza matunda kwa kutumia toroli mitaani. Lakini alipokatiza mbele ya ofisi za Serikali kuuza matunda alizuiwa na kuadhibiwa kuwa anachafua mwonekano wa mtaa huo. Hasira ya kijana huyu alienda Petrol Station na kununua mafuta akarudi mbele ya ofisi ile ile na kujichoma hadharani.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima wakapandwa hasira na maandamano nchi nzima kumtaka Rais aondoke ofisini. Upepo huu ukaenea nchi nyingi za Kiarabu na mapinduzi mengi yakafanyika na mauaji pia. Wengi walipoteza maisha kudai mabadiliko.

Leo kuna maandamano makubwa nchini Afrika Kusini na Kenya. Afrika Kusini yanaongozwa na Julius Malems (Juma) wa EFF na Kenya ni Raila Odinga wa Azimio la Umoja. Hofu yangu ni kwamba madai ya waandamanaji SA na Kenya yanafanana. Kupanda kwa gharama za maisha na utawala mbaya wa kifisadi.

Swali ni je, ni nchi ipi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ni salama katika madai haya? Jakaya Kikwete ametoa clip kumtetea Rais Samia, "mafuta yamepanda hata Uingereza hata wanamlilia gharama kupanda wangefanya nini kama sio unafiki?" Kwangu mimi huu ni utetezi wa kijinga sana maana ni yeye huyo huyo Kikwete aliwahi kuulizwa Kwa nini Watanzania ni masikini? Alisema, "hata mimi sijui". Leo atajuaje Kwa ni gharama za maisha yamepanda? Ushauri wake Kwa Samia ni kuwalambisha asali wapinzani Ili biashara zao zisiathirike Kwa maandamano.

Ninaamini upepo huu ulipoanza kuvuma kutoka J'berg hadi Nairobi utafika Dar es salaam, Kampala, Maputo nakadhalika na watawala wataadhibiwa. Asali isiwapofushe. Teteeni haki na Hali ya wanyonge wasio na sauti. Naomba upepo huo uvume tu kuja Tanzania kuondosha pengo kubwa kati ya walalanjaa na washibenjaa. Nani asimame na umma? Let's count the days ahead!
Tatizo ni rushwa rushwa. We ona jinsi ambavyo Dkt Magufuli alikataa rushwa na ufisadi alivyowindwa kuuawa na wenye kupenda rushwa, leo hii hayupo ila kuna watu bado roho zao zinawauma kwa rushwa walioshindwa kula kipindi cha utawala wake ndiyo maana wanakula sasa hivi tena kwa msisitizo wa rais wa urefu wa kamba zao, africa kuendelea mpaka kizazi chetu kife chote na cha watoto wetu labda wajukuu, maana africa mtu akikamatwa na rushwa mpaka ndugu watakwenda kusali kumuombea kesi ashinde badala ya kumuacha
 
Kwanini wewe huingii kwenye siasa ukafanya mabadiliko?
Wenyee wanaotaka kuleta mabadiliko huwa wanafanyajwe tena? You know the story! Siasa zitabadilika, sio kwa maneno maneno mengi kama mnavyojibidiisha kuhubiri..Zinabadilika kama ilivyo Kenya na South Africa. Watu wengi wakiamua kubadili. Hata falme zimewahi kuangushwa.
Hakuna jeshi la mtu mmoja aisee
 
Serikali ya Kenya Bora ingeacha waandamane kwa Amani...saiv ni fully battle polisi na raia...naangalia hapa citizen kibao kimegeuka polisi Kuna mahali wamechezea kichapo Cha mbwa Koko ...

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wenyee wanaotaka kuleta mabadiliko huwa wanafanyajwe tena? You know the story! Siasa zitabadilika, sio kwa maneno maneno mengi kama mnavyojibidiisha kuhubiri..Zinabadilika kama ilivyo Kenya na South Africa. Watu wengi wakiamua kubadili. Hata falme zimewahi kuangushwa.
Hakuna jeshi la mtu mmoja aisee
Kwa hiyo wewe umeshindwa kuingia kwenye siasa kufanya mabadiliko kisiasa? unataka wengine wa uwane?

Unajuwa maana ya neno "siasa"?
 
mafuta yamepanda hata Uingereza hata wanamlilia gharama kupanda wangefanya nini kama sio unafiki?"
Mafuta yameshuka Bei saivi pipa kwenye soko la dunia Ni $70. Wakati uke Vita ya Ukraine imepamba Moto lilipanda Hadi $140 Ila kuanzia miezi kadhaa nyuma Ni mwendo wa kushuka tu. Sema wanatoa vibali kishwahiba badala ya kuwaambia kuwa mwenye uwezo wa kuagiza lete mafuta ushindani uwe mwingi. Sasa wakipeana wanahongana baadaye yanakuwa Bei juu mfanyabiashara anakamua masikini hela alizowapa.
Chakula ameruhusu kitoke nje mpaka 16march majuzi nimeenda kibondo nakutana na magari ya wanyarwanda yanatafuta chakula yaani yanapita kila Kijiji kukusanya.
Kama kilimo Ni biashara Kama biashara zingine mbona wanazuia sukari isitoke nje waruhusu sukari ya nje ije ili ipambane na wazalishaji wa ndani ama kisa Napo wanapata kitu kidogo na wenye viwanda.

Yaani masikini siku akiamka na ndio Mana ananyimwa elimu Bora ili asiamke tokea usingizini.

Askari nao wamelala wanatetewa wasiishi kwenye mbao na watt wao wasome shule nzima Kama wanaowalindwaa wanaposomesha watt wao sema Sasa Askari anajifanya hamnazo. Traffic anastaafu Ila bado anabana mahala kuwala vichwa wenye magari.
 
Mmarekani mshenzi sana kaona viongozi wa Afrika wanaenda Urusi kwenye mkutano kahonga viongozi wa upinzani wafanye maandamano the same day. Wapuuzi kabisa
 
Huna unachojua raila alikuwepo barabarani. Jitahidi uangalie hata tv kwa jirani
Aliandamana au ALIKWENDA na gari kuhutubia wajinga walioandamana for no reasons? Yaani Afrika unalalamika bei ya Unga? Huo ni uvivu uliopitiliza Afrika tunalima MAHINDI na tunasaga mashineni tunapata unga
 
Nimewahi kwenda Ivory Coast ya miaka hiyo wakati ikiitwa "Kisiwa Cha Amani Afrika". Wale watu walikuwa ni wapole kwa dola Yao. Yani upole wa kiwango Cha kuudhi maana ulipokodi teksi ikikufikisha hotelini, dereva anaongozana na wewe Hadi chumbani ahakikishe imefika na utalala salama ndipo unamlipa hela yake. Lakini siku walipochenjiana wenyewe kwa wenyewe kutaka kuondokana na ukondoo ndani ya siku moja mifereji ya Abdijan ilijaa damu kiasi kwamba wanaweza kusimulia tukio hilo ni wanajeshi kutoka Ufaransa waliokuja kutuliza Hali. Walikuwa ni kondoo kuliko Watanzania.
Watu wapole au jamii pole ni wabaya sana. Sii wajinga. Ila pia kila lenye mwanzo kina mwisho. Hii ni Hakika.
 
Mtanzania huyu anayepewa T-Shirt na kofia akapige kura.

Anayeuza kadi yake ya kupigia kura sababu ya njaa , aende akaandamane..?

Safari bado ni ndefu sana kwa Mtanzania huyu anyesombwa na lori ili aende kujaza mkutanoni kusikiliza sera.
 
Ingekuwa nimewaona Raila, Karua, na Wajakoya barabarani ningeamoni lakini ni waoga kinyama wamejifungia vyumbani wamewaacha wakala hoi akina Nuru OKANGA wakila gesi ya machozi na virungu vya polisi waliovalia kama wanajeshi
Unafikiri hao ni kama akina Lema na Mbowe na Zitto na Lipumba eeeh,
 
Aliandamana au ALIKWENDA na gari kuhutubia wajinga walioandamana for no reasons? Yaani Afrika unalalamika bei ya Unga? Huo ni uvivu uliopitiliza Afrika tunalima MAHINDI na tunasaga mashineni tunapata unga
Kama hakuandamana kwani msafara wake ulipigwa mabomu ya machozi?

Akili zako zitakuwa za kushikiwa wewe; sina mda wa kubishana na wewe.
 
Kama hakuandamana kwani msafara wake ulipigwa mabomu ya machozi?

Akili zako zitakuwa za kushikiwa wewe; sina mda wa kubishana na wewe.
Msafara gani tena kwani ilikuwa maandamano ya magari au watu, yaani maskini wa kibera wanatembea kwa miguu huku wakipigwa tear gass wao wamejifungia kwenye magari wakati wao ndio SINE QUA NON? Wangetembea kama wenzao ili kama mabomu ya machozi wale wote
 
Nchi zote za Afrika wataandamana isipokuwa Tanzania. Awamu ya 6 inafanya mambo makubwa Sana. Hayo ya mfumuko wa bei ni dunia nzima na Sisi Tanzania siyo kisiwa. Mikopo ni sehemu ya maendeleo Kwa nchi au MTU ambaye mtaji hautoshi. Hivi miradi yote inayojengwa Kodi za ndani zitatosha? Acha wakope waweke miundo mbinu Sawa na itachangia uzalishaji na madeni yatalipwa hata miaka 100 ijayo. Tatizo Mh. Rais Hana mtaalam mzuri wa kuelezea majukumu ya mikopo kwa undani. Pia awatumbue wapigaji wanaomwangusha bila kuwaonea huruma. KAZI Iendelee.
.....au basi...,daah!
 
Mtawala amefikia levo ya chini kabisa hadi kuamua kulipa milioni 5 kwa goli la Yanga na Simba. Umesikia wapi? Na anasema hela za magoli bado zipo nyingi. Hapa umeme umekata. Dar es Sallaam ilhali mito na mabonde imejaa maji kipindi hiki. Yupo bize na Simba na Yanga.
 
Mlipuko wa Arab Spring ilianza kama masikhara nchini Tunisia baada kijana mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekosa kazi na kuamua kuuza matunda kwa kutumia toroli mitaani. Lakini alipokatiza mbele ya ofisi za Serikali kuuza matunda alizuiwa na kuadhibiwa kuwa anachafua mwonekano wa mtaa huo. Hasira ya kijana huyu alienda Petrol Station na kununua mafuta akarudi mbele ya ofisi ile ile na kujichoma hadharani.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima wakapandwa hasira na maandamano nchi nzima kumtaka Rais aondoke ofisini. Upepo huu ukaenea nchi nyingi za Kiarabu na mapinduzi mengi yakafanyika na mauaji pia. Wengi walipoteza maisha kudai mabadiliko.

Leo kuna maandamano makubwa nchini Afrika Kusini na Kenya. Afrika Kusini yanaongozwa na Julius Malems (Juma) wa EFF na Kenya ni Raila Odinga wa Azimio la Umoja. Hofu yangu ni kwamba madai ya waandamanaji SA na Kenya yanafanana. Kupanda kwa gharama za maisha na utawala mbaya wa kifisadi.

Swali ni je, ni nchi ipi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ni salama katika madai haya? Jakaya Kikwete ametoa clip kumtetea Rais Samia, "mafuta yamepanda hata Uingereza hata wanamlilia gharama kupanda wangefanya nini kama sio unafiki?" Kwangu mimi huu ni utetezi wa kijinga sana maana ni yeye huyo huyo Kikwete aliwahi kuulizwa Kwa nini Watanzania ni masikini? Alisema, "hata mimi sijui". Leo atajuaje Kwa ni gharama za maisha yamepanda? Ushauri wake Kwa Samia ni kuwalambisha asali wapinzani Ili biashara zao zisiathirike Kwa maandamano.

Ninaamini upepo huu ulipoanza kuvuma kutoka J'berg hadi Nairobi utafika Dar es salaam, Kampala, Maputo nakadhalika na watawala wataadhibiwa. Asali isiwapofushe. Teteeni haki na Hali ya wanyonge wasio na sauti. Naomba upepo huo uvume tu kuja Tanzania kuondosha pengo kubwa kati ya walalanjaa na washibenjaa. Nani asimame na umma? Let's count the days ahead!
Wataanda manda mwisho wataishia kunywa maji na macho yao kuwasha kwa moshi wa mabomu

Ukweli ulivio kolona na vita ya ukereine na mvua kutonyesha kwa wakati ndio chanzo cha mambo haya

Hata huyo malema odinga hata wakapewa urais hakuna jipya watakalo kufanya katika kipindi kigumu kama hiki duniani nchi za wazungu nazo haziko salaama kwa sababu ya kolona na vita ya urusi

Wewe ulitaka Kikwete asemaje?ni kweli hata wazungu wako hoi baadhi yao wanalalama

Haya ngoja tuone hao wanao andamana kama hali itabadilika mfano kenya aridhi yote iko mikononi mwa hao wanasiasa dawa ya masikini ni kunyesha mvua za viwango vizuri watu wakalima vinginevyo watatoana roho bule
 
Back
Top Bottom