Kinachotokea Afrika Kusini na Kenya inaweza kuwa sawa na Arab Spring kwa nyingine za Afrika

Kinachotokea Afrika Kusini na Kenya inaweza kuwa sawa na Arab Spring kwa nyingine za Afrika

Mlipuko wa Arab Spring ilianza kama masikhara nchini Tunisia baada kijana mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekosa kazi na kuamua kuuza matunda kwa kutumia toroli mitaani. Lakini alipokatiza mbele ya ofisi za Serikali kuuza matunda alizuiwa na kuadhibiwa kuwa anachafua mwonekano wa mtaa huo. Hasira ya kijana huyu alienda Petrol Station na kununua mafuta akarudi mbele ya ofisi ile ile na kujichoma hadharani.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima wakapandwa hasira na maandamano nchi nzima kumtaka Rais aondoke ofisini. Upepo huu ukaenea nchi nyingi za Kiarabu na mapinduzi mengi yakafanyika na mauaji pia. Wengi walipoteza maisha kudai mabadiliko.

Leo kuna maandamano makubwa nchini Afrika Kusini na Kenya. Afrika Kusini yanaongozwa na Julius Malems (Juma) wa EFF na Kenya ni Raila Odinga wa Azimio la Umoja. Hofu yangu ni kwamba madai ya waandamanaji SA na Kenya yanafanana. Kupanda kwa gharama za maisha na utawala mbaya wa kifisadi.

Swali ni je, ni nchi ipi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ni salama katika madai haya? Jakaya Kikwete ametoa clip kumtetea Rais Samia, "mafuta yamepanda hata Uingereza hata wanamlilia gharama kupanda wangefanya nini kama sio unafiki?" Kwangu mimi huu ni utetezi wa kijinga sana maana ni yeye huyo huyo Kikwete aliwahi kuulizwa Kwa nini Watanzania ni masikini? Alisema, "hata mimi sijui". Leo atajuaje Kwa ni gharama za maisha yamepanda? Ushauri wake Kwa Samia ni kuwalambisha asali wapinzani Ili biashara zao zisiathirike Kwa maandamano.

Ninaamini upepo huu ulipoanza kuvuma kutoka J'berg hadi Nairobi utafika Dar es salaam, Kampala, Maputo nakadhalika na watawala wataadhibiwa. Asali isiwapofushe. Teteeni haki na Hali ya wanyonge wasio na sauti. Naomba upepo huo uvume tu kuja Tanzania kuondosha pengo kubwa kati ya walalanjaa na washibenjaa. Nani asimame na umma? Let's count the days ahead!
Wewe unajuwa kwannini Watanzania masikini?

Au ulitaka Kiwete ajibu ni walevi na wavivu wa kupindukia?
 
Waache kupamba na mfumoko wa bei wawe Bize na simba na Yanga sijui kufunga nchi watajijua hawa Watanzania wasionwe wanyonge siku wakiamua itakuwa shida sana.

USSR
Ushawahi kuona mjanja ambaye ana njaa? Mugabe baada ya kuwamaliza wazungu, akaanza kushughulikiwa yeye mwenyewe, tena na watu wale wale aliowapa mshamba ya wazungu.
Uongozi wa nchi za kiafrika ubadilike. Watu wanataka maendeleo. Watu wanataka accountability. Kinachoendelea sasa, kinaweza kutokea sehemu yoyote Africa
 
Tanzania mburura iko mingi, inadanganywa kidogo tu inakuwa mipooole ka kondoo! Hakuna wa kuandamana...Maisha ni magumu kweli, ila mitanzania iko tayari kula udongo ila watawala waendelee kula kuku!!
 
Haki ipi ambayo unaidai na hukuipata?
Kinachopambaniwa sio haki ya mtu...wanapambania ccountability. Wanataka wana siasa waache kula na kusaza kwa mgongo wa walala hoi. Wana siasa wa Africa, wengi wanatumia vibaya nafasi zao. Kujinufaisha wao, rafiki na familia zao
 
Mimi sijawahi kunyimwa Haki zangu.
Ila nazungumzia watanzania wengine.

Nenda viwandani Huko utajionea watanzania walivyo,
Sasa hizo ni porojo. Viwandani wanakosa hakinipi nina ni kiwanda kipi hicho?

Hao wa viwandani haki zao walikuja kudai kwako, au walikuletea wewe malamiko?

Hawajui wapi pa kwenda kudai haki zao?
 
Ingekuwa nimewaona Raila, Karua, na Wajakoya barabarani ningeamoni lakini ni waoga kinyama wamejifungia vyumbani wamewaacha wakala hoi akina Nuru OKANGA wakila gesi ya machozi na virungu vya polisi waliovalia kama wanajeshi
Angalia tena...wapo tele!
 
Ingekuwa nimewaona Raila, Karua, na Wajakoya barabarani ningeamoni lakini ni waoga kinyama wamejifungia vyumbani wamewaacha wakala hoi akina Nuru OKANGA wakila gesi ya machozi na virungu vya polisi waliovalia kama wanajeshi
Wewe unaishi Buza kwa mpalange umejuaje kama hawajajitokeza kwenye maandamano?
 
Ondoa Tanzania hapo.. Hii nchi kulala njaa ni uzembe wako tu ingali wenzetu huko mpaka ushike tonge la ugali ni umehanya sana. Hii nchi madalali wa viwanja wana magari na iPhone 13 unadhani kuna wa kuandamana hapo? Maisha ya mjini yakikushinda unarudi kijijini unakutana na bonge la msitu ni wewe na nguvu zako uanze kulima, wenzetu hawana hii. South Africa na Kenya ardhi yote imebebwa na elites. Maisha yao ni ya supermarket tu kwahiyo hujahanya lazima utalala njaa.

Narudia, Tanzania watu kuandamana labda itokee mageuzi makubwa sana kuliko tuliyonayo. We nchi mtu anavamia mahali anafanya usafi basi anaanza kuuza plots unadhani kuna maandamano hapo. Ukweli ni kwamba hapa kwetu njaa haipo.
 
Raila Odinga anapigania maslahi yake.
Hakuna Tajiri anayeweza kupigania maslahi ya maskini.

Wakenya ni wapumbavu sana wanadhani wakiumizana Kwa ajjili ya Maslahi ya Raila watakaoumia ni watawala au Bado ni maskini.?

Raila Ana Miaka ZAIDI ya Sabini Bado haoni kuwa siasa za kimfumo zimemkataa .

Alibebwa na Serikali ya Uhuru lakini akashindwa mwenyewe Kwa siasa zake zilizokosa será madhubuti akabaki na vichekesho majukwaani.
Sasa Raila baada ya kushindwa anataka nchi iingie kwenye machafuko. Inatakiwa kabla ya Wakenya hawajaamua kuuana wamuue yeye kwanza . Pumbavu kabisa!!!
 
Kinachopambaniwa sio haki ya mtu...wanapambania ccountability. Wanataka wana siasa waache kula na kusaza kwa mgongo wa walala hoi. Wana siasa wa Africa, wengi wanatumia vibaya nafasi zao. Kujinufaisha wao, rafiki na familia zao
Kwanini wewe huingii kwenye siasa ukafanya mabadiliko?
 
Ingekuwa nimewaona Raila, Karua, na Wajakoya barabarani ningeamoni lakini ni waoga kinyama wamejifungia vyumbani wamewaacha wakala hoi akina Nuru OKANGA wakila gesi ya machozi na virungu vya polisi waliovalia kama wanajeshi
Huna unachojua raila alikuwepo barabarani. Jitahidi uangalie hata tv kwa jirani
 
Raila Odinga anapigania maslahi yake.
Hakuna Tajiri anayeweza kupigania maslahi ya maskini.

Wakenya ni wapumbavu sana wanadhani wakiumizana Kwa ajjili ya Maslahi ya Raila watakaoumia ni watawala au Bado ni maskini.?

Raila Ana Miaka ZAIDI ya Sabini Bado haoni kuwa siasa za kimfumo zimemkataa .

Alibebwa na Serikali ya Uhuru lakini akashindwa mwenyewe Kwa siasa zake zilizokosa será madhubuti akabaki na vichekesho majukwaani.
Sasa Raila baada ya kushindwa anataka nchi iingie kwenye machafuko. Inatakiwa kabla ya Wakenya hawajaamua kuuana wamuue yeye kwanza . Pumbavu kabisa!!!
Sababu zao za kuandamana umezisikia au umeshiba magi, bi unaropoka tu
 
Back
Top Bottom