Kinachotokea Afrika Kusini na Kenya inaweza kuwa sawa na Arab Spring kwa nyingine za Afrika

Kinachotokea Afrika Kusini na Kenya inaweza kuwa sawa na Arab Spring kwa nyingine za Afrika

Watanzania tuunganishe hapo hapo tudai katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na kuondolewa mlolongo wa tozo na maisha magumu. Wiki hii hii sio wiki ijayo.
Kenya afirika kusini ndio nchi zenye katiba bora dunia lakini Madudu kila kona mtu mweusi hana uwezo wa kusimamia katiba bhana
 
Nimewahi kwenda Ivory Coast ya miaka hiyo wakati ikiitwa "Kisiwa Cha Amani Afrika". Wale watu walikuwa ni wapole kwa dola Yao. Yani upole wa kiwango Cha kuudhi maana ulipokodi teksi ikikufikisha hotelini, dereva anaongozana na wewe Hadi chumbani ahakikishe imefika na utalala salama ndipo unamlipa hela yake. Lakini siku walipochenjiana wenyewe kwa wenyewe kutaka kuondokana na ukondoo ndani ya siku moja mifereji ya Abdijan ilijaa damu kiasi kwamba wanaweza kusimulia tukio hilo ni wanajeshi kutoka Ufaransa waliokuja kutuliza Hali. Walikuwa ni kondoo kuliko Watanzania.
Faida ya maandamano ni kuuana na kuwafanya watu kuwa masikini na vilema fatilia afirika kusini kenya tangu wameanza kuandamana wamepata nini cha maana
 
Mlipuko wa Arab Spring ilianza kama masikhara nchini Tunisia baada kijana mmoja mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekosa kazi na kuamua kuuza matunda kwa kutumia toroli mitaani. Lakini alipokatiza mbele ya ofisi za Serikali kuuza matunda alizuiwa na kuadhibiwa kuwa anachafua mwonekano wa mtaa huo. Hasira ya kijana huyu alienda Petrol Station na kununua mafuta akarudi mbele ya ofisi ile ile na kujichoma hadharani.

Wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima wakapandwa hasira na maandamano nchi nzima kumtaka Rais aondoke ofisini. Upepo huu ukaenea nchi nyingi za Kiarabu na mapinduzi mengi yakafanyika na mauaji pia. Wengi walipoteza maisha kudai mabadiliko.

Leo kuna maandamano makubwa nchini Afrika Kusini na Kenya. Afrika Kusini yanaongozwa na Julius Malems (Juma) wa EFF na Kenya ni Raila Odinga wa Azimio la Umoja. Hofu yangu ni kwamba madai ya waandamanaji SA na Kenya yanafanana. Kupanda kwa gharama za maisha na utawala mbaya wa kifisadi.

Swali ni je, ni nchi ipi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ni salama katika madai haya? Jakaya Kikwete ametoa clip kumtetea Rais Samia, "mafuta yamepanda hata Uingereza hata wanamlilia gharama kupanda wangefanya nini kama sio unafiki?" Kwangu mimi huu ni utetezi wa kijinga sana maana ni yeye huyo huyo Kikwete aliwahi kuulizwa Kwa nini Watanzania ni masikini? Alisema, "hata mimi sijui". Leo atajuaje Kwa ni gharama za maisha yamepanda? Ushauri wake Kwa Samia ni kuwalambisha asali wapinzani Ili biashara zao zisiathirike Kwa maandamano.

Ninaamini upepo huu ulipoanza kuvuma kutoka J'berg hadi Nairobi utafika Dar es salaam, Kampala, Maputo nakadhalika na watawala wataadhibiwa. Asali isiwapofushe. Teteeni haki na Hali ya wanyonge wasio na sauti. Naomba upepo huo uvume tu kuja Tanzania kuondosha pengo kubwa kati ya walalanjaa na washibenjaa. Nani asimame na umma? Let's count the days ahead!
Tafuta pesa ndugu...!hakuna maisha rahisi dunia nzima...!utanishukuru.
 
Ingekuwa nimewaona Raila, Karua, na Wajakoya barabarani ningeamoni lakini ni waoga kinyama wamejifungia vyumbani wamewaacha wakala hoi akina Nuru OKANGA wakila gesi ya machozi na virungu vya polisi waliovalia kama wanajeshi
Unamawazo mgando sana
 
mfumko ya Bei ni tatizo la Ulimwengu mzima, sasa munapoandamana sijui munakitafuta nini, Unless muwe na ajenda zenu nyengine behind scene.
 
Sisi hapa Mbowe na Zitto Kabwe yameshakula bahasha ya kaki yamekazana MAMA MAMA MAMA MAMA kama mabwege vile. Badala ya kutumia hii opportunity kuanzisha upya lile vuguvugu la mabadiliko ambalo lilizimwa na Magufuri yanalaza damu saa hii tundulissu hata sijui yupo eneo gani la Dunia hii amebakia kuwa mzururaji tu.
 
Back
Top Bottom