Kinachotokea kwenye mikutano mkuu wa mkoa Arusha kitufungue macho!

Anachofanyq makonda ni kujijenga kisiasa ana-uhakika hakuna kitakachotea ila jambo litekelezwe linahitaji mchakato wa kisheria wa kwenda mahakamani

Anachofanyq ni PR
Mfano hao wqnaotokea kwenye hiyo mikutano nani anathibitisha uhalali wao? Nani anathibitisha hayo madai? Nani anathibitisha ukweli wake? Hii nchi ina watu wa hovyo sana!
 
Mfano hao wqnaotokea kwenye hiyo mikutano nani anathibitisha uhalali wao? Nani anathibitisha hayo madai? Nani anathibitisha ukweli wake? Hii nchi ina watu wa hovyo sana!
Na huwezi sikiliza upande mmoja ukatoa maamuzi
Ndo maana mahakaman kila mmoja anapewa nafasi ya kujitetea kabla ya hukumu
Tanzania tuna safari ndefu sana
 
Ushauri mzuri sana. Serikali , nje ya mkuu wa mkoa, ina vyombo vyake vya kutatua matatizo mbalimbli kama vile mabaraza ya ardhi ya kata, mahakama nk.
 
Na huwezi sikiliza upande mmoja ukatoa maamuzi
Ndo maana mahakaman kila mmoja anapewa nafasi ya kujitetea kabla ya hukumu
Tanzania tuna safari ndefu sana
Ila kisaikolojia watu wasio na akili kichwani huwa na ujanja wa ku survive zana....

Na wabongo wengi hawajiulizi ile migogoro na madai alokua akishughulika nayo akiwa katibu mwenezi yaifa mwisho wake ulikuaje? Nani anafatilia hitimisho lake?
 
Mwarubaini wa matatizo ni kuwahamisha watendaji waliokaa muda mrefu, kuna taasisi kama mambo ya ndani, ualimu, afya, ujenzi, mawasiliano, mahakama wanaenda kuombewa sehemu za Ibada wasihame, kuna mwl chuo Kikuu hajawahi kuhama yaani ni full kutengeneza connection za madili, hili la Makonda kusema wahamishwe ni Sawa kabisa, Enzi za raisi Kikwete serikali ili control nidhamu kwa kuhamisha ajabu sasa hivi wanahamishwa wakuu wa wilaya, mikoa na labda mawaziri, mpaka sasa kuna taasisi zipo dar hazijahamia Dodoma na wale waliowahi kufika Dodoma hawahamishwi kabisa, hivyo kukaa na faili la MTU kwaajili ya ukiritimba ni rahisi Sana maana huhami mpaka unastaafu na kuajili watoto wako hapo hapo maana unageuka mwenye taasisi ya serikali.
 
Mimi nafikiri approach iwe tofauti. Sidhani watu wenye shida hasa wanaweza kupata hata nauli ya kusafiri na huenda hata kuweza kulala nyumba ya kulala wageni kwa sababu ya kwenda kumwona mkuu wa mkoa. Nadhani ni approach inayowalenga wenye shida nafuu au ambao maisha Bado yanawaendea vizuri. Chukulia mtu ambaye anashindwa hata kula Milo miwili kwa siku, je anaweza kusafiri kwenda mjini kuona na mkuu wa mkoa? Kwa nini kama lengo ni kuona na wananchi, hao wananchi wasifuatwe huko waliko (kwenye vijiji, vitongoji, kata)? Mimi naipna hii kama political strategy ya ku'win' public trust, lakini sioni kama njia sahihi ya kutatua kero za wananchi. Fikiria wazee au bibi ambao wanatembea kwa shida au pia hawawezi kutembea na almost always wako tu nyumbani, je wanaweza kusafiri kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa? Fikiria akina mama ambao ndio walinzi wa familia na watoto nyumbani, je wanaweza kusafiri kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa? Walemavu je? Wanaishi chini ya $2.50, je wanaweza kusafiri kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa? Jibu ni hapana! Then, kwa nini kusiwe na utaratibu wa kwenda kwa hao wasio na uwezo zaidi ili wasaidiwe huko waliko? Kwa uzosfu wangu, huyu mkuu huwa anaibua haya mambo ambayo huwa yanawavuta watu kwa kutegemea kama watasaidiwa lakini huwa ni short-term. Ni kama msemo wa 'mbio za sakafuni huishia ukingpni'. Njia nzuri ya kutatua kero za wananchi ni kuwatembelea huko waliko, kuwasikiliza na kuweka mfumo au utaratibu utakaorahisisha kero zao kutatuliwa kama wananchi wote na siyo kuchagua aina ya watu wa kusaidia. Hii ya 'nitakujengea nyumba ya vyumba viwili au vitatu' siyo utatuzi wa matatizo ya wananchi ni kuchagua nani wa kumsaidia na inaleta picha kwamba wengine wenye shida kama hiyo au hata zaidi ya hiyo hawana wa kuwasaidia. Do you get my point?
 
Nurdin babu amelala usingizi.
Anasubiri kwenda ATM mwisho wa mwezi
Huyu kweli Babu. Jana ameenda kule KINAPA kuna kijana ameuliwa na askari wa mali asili na ushahidi upo lakini hakuna la maana alilosema au kuamua.

Babu anasubiri tu tarehe za kutoboa ukuta wa Benki zifike basi. Kwanza hata hajulikani kama yuko Moshi.
 
Kwamba huyo PM ama walioko juu yake hawayajui hayo? Utakuwa mgeni hapa Tanganyika wewe.

Huyo dogo anaivua nguo serikali ya chama cha mafisadi na hapo watakacho kifanya saaana ni kuzuia aina hiyo ya mikutano isiendelee.

Lkn pia maigizo pia hayawezi kukosekana ijapo kidogo.
 
Mikutano kama hiyo alikuwa anafanya Jaji Warioba katika ziara zake akiwa PM, ila utawala huu hao maDAC RC wataifanyia maigizo ya kusifu na kuabudu kwasababu hawana ubunifu, huyo aliyefanikiwa ni mbunifu, waigizaji hawataifanya kwa kutafuta matokeo halisi.
 
Katiba Mpya inayojisimamia ni muhimu! Kila mtu ajue haki na wajibu kwa mujibu wa Katiba!
 
Unapata wapi muda wa kusimiliza mikutano,nyie ndio mnashinda vijiweni badala ya kwenda shamvani,pili unue hsyo ni maigizo tu
 
Dogo anamuumbua aliyemteua, ili amkomeshe! Hakumuheshimu awamu iliyopita, hamuheshimu sasa, sijui nini kilipelekea kuwekwa kwenye hizi nafasi?
 
Hivi unajua hayo yote yanatokea Chini ya Serikali ya CCM iliyoongoza kwa miongo mingi Sana? Unajua hao unaowasema wasikilize kero za wananchi ni Makada wa CCM??
Unajua kuwa hayo yote yanayolalamikiwa yako Chini ya Mbunge wa CCM? Nadhani Sasa unaelewa kuwa CCM ni janga
 
Dogo anamuumbua aliyemteua, ili amkomeshe! Hakumuheshimu awamu iliyopita, hamuheshimu sasa, sijui nini kilipelekea kuwekwa kwenye hizi nafasi?
Kwa hiyo unataka kusema,aliyemteuwa dogo ndiyo analinda Matapeli yanayoumbuliwa na dogo!?
 
Raisi wenu hapendi hayo mambo,iweje PM tena kuangushiwa jumba bovu
 
Mfano hao wqnaotokea kwenye hiyo mikutano nani anathibitisha uhalali wao? Nani anathibitisha hayo madai? Nani anathibitisha ukweli wake? Hii nchi ina watu wa hovyo sana!

Ujue Watanzania sio wajinga....hawazi mtu kwenda kwenye madai akiwa hajajiandaa...
Kama umefuatilia mikutano utakuwa umegundua kuwa; wengi wanaokuja wana data na refrence kibao (faili zima) pengine kushinda hata Mkurugenzi au pengine wanatakiwa kuwakilisha ushahidi wa madai yao siku inayofuata; na baadhi wamekuja na nyaraka za mahakama zilizodhibitisha kuwa wameshinda ila bado hawakupewa stahiki zao;
Kwa mtu mwenye maarifa anaweza kutambua madai Yenye uhalali inaeleweka na hata kabla ya watu kusomea madegree ya sheria Kesi zilikuwa zina amuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…