Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Hapa nimekuelewa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukataa kuhojiwa wameonesha kuwa hawana hoja za kujibu
Ccm hatujawahi kuyumbishwa na viongozi hata siku moja
Jumbe alivuliwa nyadhifa zake zote,zaidi ya nne,Maalim sefu na genge lake walitimuliwa itakua hao wastaafu
Kwani wao wamesema wanataka nyadhifa wameshatumikia sana chama kwa miaka na walishastaafu siasa za kila siku muda tu sasa Jumbe alikuwa kiongozi na wakati huo chama kimoja ilikuwa kuna nguvu kubwa ya chama na hakukuwa na platform za kuongelea nje ya chama na serikali ila leo maoni yako utayatolea nyumbani tu tena vyombo vya habari vitakuomba wewe. waacheni wazee wapumzike inatosha heshima ni kitu cha bure nadhani wazee waliobaki wanajitafakari maana leo ni kama kutishwa ila bora ufe ukiwa na heshima yako kuliko kudhalilishwa na watoto.
 
Ni vema wameamua kuondoka mapema kwani CCM inahitaji mabadiliko Makubwa Sana.
Uzee na Uzoefu usioenda na Uadilifu Ni hewa tu na hauna maslahi kwa Taifa letu.

Kama Wana Tuhuma zozote za Kijinai Basi nashauri Mamlaka Husika ziingie kazini.
 
Hawa Ma- Komredi, lazima waumie. Ilikuwa badala ya kusikilizwa malalamiko yao, wao ndio wakaonekana ndio wakosaji, na kutakiwa kufikishwa KIZIMBANI huko Dodoma.
 
Kukataa kuhojiwa wameonesha kuwa hawana hoja za kujibu
Ccm hatujawahi kuyumbishwa na viongozi hata siku moja
Jumbe alivuliwa nyadhifa zake zote,zaidi ya nne,Maalim sefu na genge lake walitimuliwa itakua hao wastaafu
Pole Mkuu ndio upeo wako ulipoishia,unatolea mfano usioijua ..hoja za Jumbe na Maalim kuhusu Zanzibar+Muungano zitaitesa CCM milele,na Si ajabu zitakuwa Msingi wa kubadilisha Historia ya Tanzania ...Ni suala la muda tu!
Kwa wanaCCM Kama wewe mnaomshabikia Musiba hili kwako Ni Elimu ya Nuklia!
 
Kuna meli yenye nyara za serikali ilikamatwa ughaibuni, Hivi ni nani alikuwa mmiliki?
 
Ni vema wameamua kuondoka mapema kwani CCM inahitaji mabadiliko Makubwa Sana.
Uzee na Uzoefu usioenda na Uadilifu Ni hewa tu na hauna maslahi kwa Taifa letu.

Kama Wana Tuhuma zozote za Kijinai Basi nashauri Mamlaka Husika ziingie kazini.
Akili mkojo hizi
 
Mkuu kuna watu ni mazezeta sana humu. Musiba kawakalia kwenye ubongo wao hawatafakali tena
 
Bahati mbaya wazee wetu walipokuwa njiani walipata matatizo ya usafiri kutokana na mvua kubwa zinazonyesha kuvunja madaraja mkoani Tanga na Arusha hivyo magari yao kushindwa kuendelea na safari. Hata hivyo wamefurahishwa na maamuzi ya chama kuwahoji ili kujenga umoja wetu watanzania aliotuachia baba wa taifa.
Samahani nilisema madaraja hapana, ni kwamba walipata mafua kutokana na vumbi wakati huu wa mvua nyingi zinazosababisha tope barabarani, lakini wote walifika salama Dar es Salaam na wiki ijayo wataanza safari ya kuja makao makuu ya chama Dodoma.
 
Ni afadhali CCM ife izikwe kabisa kuliko kurudi kwenye CCM ya Makamba na Kinana; kuvaa jezi ya Yanga mtaani ilikuwa taabu sana enzi hizo. Siku hizi naziona nyingi tu.
Ungeeleza kinachoitofautisha CCM ya Magufuli na hiyo ya akina Makamba na Kinana ingesaidia sana kukuelewa.

Tofauti inayoonekana sasa hivi ni kuwa CCM ya Magufuli ni yake. Anaimiliki. Kama unapenda anayofanya mwenye mali yake, bila shaka hata mali utaipenda.

Lakini inashangaza pia kwamba ile CCM ya akina Makamba na Kinana, pamoja na ubovu wake, ndiyo iliyomweka Magufuli alipo na kumkabidhi hiyo mali anayoihodhi.

Hao wawili, Makamba na Kinana kazi kubwa waliyofanya na CCM yao mbovu kumnadi Magufuli sio kazi inayoweza kubezwa kirahisi hapa leo.
 
Ila dada hawa walisema watatubatiza kwa moto wao, hata wamogopa kuweka kidole chao,ukichimba shimo utadumbukia mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hao maccm wamesahau ule msemo wa wahenga unaosema, usisahau mbachao kwa msala upitao........
 
Ukiona hivyo jua musiba alishapuuzwa na wao hawaitwi kwa hizo tuhuma za musiba bali maneno walioongea wao kwenye simu.
Chama kina taratibu zake na lazima zifuatwe ili kukilinda chama na mwisho iwe taasisi imara.
Chama kutokuwa na misimamo na kuwa na double standards imeigharimu chadema kila kona ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umbea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…