Tetesi: Kinana agoma kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM

Status
Not open for further replies.
Mkuu vita ya Musiba unaiweza?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimkashifu kitu gani? Maana sijaona kashifa
 
Ni vema wameamua kuondoka mapema kwani CCM inahitaji mabadiliko Makubwa Sana.
Uzee na Uzoefu usioenda na Uadilifu Ni hewa tu na hauna maslahi kwa Taifa letu.

Kama Wana Tuhuma zozote za Kijinai Basi nashauri Mamlaka Husika ziingie kazini.
Wewe hauijui CCM, kwanza chama huwa akina mbadhirifu kama mfikirivyo, haina auditing ya mnayo fikiria, mambo yake upangwa na kamati za siasa na ukaguzi ujifanyia zenyewa taarifa upeleka tu kwenye vikao vya halmashauri kuu, na wajumbe wake ni pamoja na wa kamati ya siasa, hivyo vyote waamuavyo ni halali. Na hawana bajeti kukiwa na jambo. Kumbuka lengo kuu la cha cha siasa ni kushika Dola, mengine baadae, hivyo wewe kama unaona mali na pesa vina dhamani si kwa siasa.
 
Kila zana na kitabu chake baba.

CCM ya Nyerere haikuwa sawa na CCM ya Mwinyi, na haikuwa sawa na CCM ya Mkapa, na vile vile haikuwa sawa na CCM ya Kikwete na haitakuwa sawa na CCM ya Magufuli, na haitakuwa sawa na CCM ya atakayemfuata Magufuli.

It is a simple fact! Tuliambiwa kuwa ya Kaizari mpe Kaizari; usitafute mwingine wa kumpa.

Wazee hawa sijawasikia wakilalamika kuwa serikali haitekelezi Ilani ya CCM, wanacholalamikia kuwa wamesahahuliwa na serikali !!. Hata wakiondoka CCM sidhani kama wana political impact yoyote tena. Ni afadhali wangenyamaza tu; kuna methali inasema ukila na kipofu usimguse mkono, wao walianza kuvuta kabisa mkono wa kipofu huyo wakaiona
 
Zitto kabwe umeibuka na vioja vyako!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa Ma- Komredi, lazima waumie. Ilikuwa badala ya kusikilizwa malalamiko yao, wao ndio wakaonekana ndio wakosaji, na kutakiwa kufikishwa KIZIMBANI huko Dodoma.
Ina maana msingi wa mashitaka ni kudukuliwa, kwanza ashitakiwe mdukuwaji!
 
CCM CHAMA LAO....MANYUMBU WAMESAHAU WANACHOPIGANIA SASA WOTE TUMEWAGEUZISHA WAMEHAMIA KWENYE MJADALA WA KINANA NA MAKAMBA MKIJA KUSANUKA UCHAGUZI HUU.....


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kumbe yule bwana ni kinyangarika,
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mimi ningekua makamba au kinana nisingeenda
 
Mara nyingi niwaonapo wazee hawa huwa naikumbuka vita ya Kagera iliyomng'oa dikteta nduli fashisti Iddi Amini Dada pale Uganda.

Wakati huo nilikuwa nafanya kazi pale TRC Mwanza station......hakika niliwashuhudia wapiganaji wetu WAZALENDO wengi wakielekea vitani. Nasi tulitoa kila aina ya msaada uliohitajika ili kuwawezesha wapiganaji hawa.

Ndio maana siku mzee Lowassa alipotangaza kujiuzulu uwaziri mkuu sikushangaa kabisa.

Na hata nikisikia mzee Kinana na mwenzie Makamba wamestaafu siasa na kurudisha kadi za chama cha siasa kwa wamiliki wa kadi sitashangaa.

Kuchukua maamuzi magumu ni sehemu ya maisha ya mjeda popote pale duniani.

Nawatakia Dominika yenye Baraka!
 
Kinana na makamba Wana heshima zao.hawawezi kukubali kuburuzwa vikamati "uchwara" ili tuu kumsujudia magufuli.
Kukataa kuhojiwa wameonesha kuwa hawana hoja za kujibu
Ccm hatujawahi kuyumbishwa na viongozi hata siku moja
Jumbe alivuliwa nyadhifa zake zote,zaidi ya nne,Maalim sefu na genge lake walitimuliwa itakua hao wastaafu
 
Hawana tuhuma zozote magufuli anataka kuiendesha CCM kwa mkono wa chuma.wazee wamegoma
Ni vema wameamua kuondoka mapema kwani CCM inahitaji mabadiliko Makubwa Sana.
Uzee na Uzoefu usioenda na Uadilifu Ni hewa tu na hauna maslahi kwa Taifa letu.

Kama Wana Tuhuma zozote za Kijinai Basi nashauri Mamlaka Husika ziingie kazini.
 
Watu Kama nyie humu nchini tunawaita wasindikizaji.hujui ulikotokaa,ulipo, naunapokwenda.
CCM CHAMA LAO....MANYUMBU WAMESAHAU WANACHOPIGANIA SASA WOTE TUMEWAGEUZISHA WAMEHAMIA KWENYE MJADALA WA KINANA NA MAKAMBA MKIJA KUSANUKA UCHAGUZI HUU.....


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…