Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kinana anasema wabunge hawaendi bungeni kwa idadi ya watu Bali hoja! Kwa hiyo anamaanisha Wazanzibar na uchache wao wanahoja zaidi kuliko sisi wabara! Hapo ndio nimejua hoja ya Lisu itawamaliza ccm.
Huyu mzee anapotosha sana hili suala tena kwa kurudia rudia! Hakuna shida wazanzibari kuwa na Idadi yoyote wa wabunge wanaotaka kama wangekuwa wanaishia Zanzibar, tatizo linakuja wanapovuka na kuingia upande wa pili ambapo kodi za wote zinatumika kuhudumia hao wabunge.
 

Nadhani Kinana akili amechoka kama ulivyoka mwili wake. Hakuna cha maana alichokijibu.

Hawa ni watu wanaofikiria, hata vitu vinavyohitaji vitendo, vinaweza kujibiwa kwa hadithi. Mchakato wa katiba ulifikia hatua ya kupiga kura karibia miaka 10 iliyopita. Katiba pendekezwa ya Warioba ilihusisha maoni ya watu wengi wa kila makundi. Halafu Kinana kwenye porojo zake inasema inahitaji muda, haitakiwi kuwa ya vyama vya siasa tu! Huyu labda akili imekwishaanza kupoteza kumbukumbu. Hivi maoni kuhusiana na katiba mpya, ya jaji Warioba, walikuwa wanawahoji CHADEMA pekee yake? Kweli Kinana amechoka, aachwe apumzike.

Masuala ya Muungano, amepigapiga tu porojo, hakuna cha maana alichojibu. Anasema Muungano ni wa nchi 2, kuna mtu amekataa kuwa siyo wa nchi mbili? Kama anajua ni Muungano wa nchi 2, moja ina serikali yake, nyingine haina. Imeenda wapi?

Wasio na hoja tuwapuuze, madai ya msingi yamebakia pale pale:

1) Wananchi wanataka katiba mpya. Kazi aliimaliza Jaji Warioba na timu yake.

2) Tunataka Tume huru ya uchaguzi, siyo ya kimagumashi, iliyowekwa na mtu mmoja.

3) Tunataka Muungano wenye muundo mzuri wenye kulinda maslahi ya wabia wote wa Muungano.

Kama mtu hana majibu, kama alivyokosa majibu Mzee Kinana, asipoteze muda wa wananchi kwa kuleta hadithi, awaache wananchi waendelee na kuipigania nchi yao ya Tanganyika iliyopotezwa. Au la na Zanzibar ipotee, ibakie nchi moja tu.
 
Kwanini hawataki yaani ikizungumzwa katiba ccm wanakua mbogo hivi hawaoni hata wao itawasaidia pia hivi haya maisha wao wanaona ni sawa? Kawann wamekua wajinga kiasi hiki? Yaan 90 % tunaitaka katiba wao hata asilimia moja ya watanzania hawazidi mbona ni wajinga hivi?
 
Yule UVCCM wa Bukoba anayepanga kuwapoteza wapinzani unamuweka kundi lipi? Sabaya na Makonda ambao nao walisema watamaliza wapinzani nao unawaweka kundi gani ati! Mtu wa Tanganyika hawezi kumiliki ardhi visiwani Zanzibar, ila mtu wa Zanzibar anawexa kumiliki ardhi hapa Tanganyika. Huu sio ubaguzi?
 
Ukiongea huo ujinga mbele ya wakenya unaweza chapwa makofi mengi Sana
 
Tunataka mgombea binafsi. Wanaogopa nini?
Taifa linaingia gharama kubwa kufanya uchaguzi wa magirini kila baada ya miaka mitano. Ni heri usiwepo uchaguzi kuliko kutumia mabilioni ya shilingi kuhadaa ulimwengu kuwa tunafanya uchaguzi;

Kinana asikie tunataka mgombea binafsi.
 
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 

Hapo Kinana amebwabwaja ili kuwachanganya watu. Hata CCM hawakuonekana kuwa impressed.

Lissu hakuzungumzia idadi ya Wabunge au Waakirishi kwenye baraza lao la Wawalkirishi Zanzibar. Ameongelea Bunge la Jamhuri. Sasa Kinana anatuambia kuwa Zanzibar ni nchi ambayo wanajiamulia mambo yao. Sasa kesho wakiamua kutuletea Wabunge 100 sisi tutasema ni sawa tu ..... Vile vile Kinana anaitaja Zanzibar kama nchi lakini nchi ya pili inayounda Muungano kashindwa kuitaja hata mara moja.

Kwa ujumla Kinana kachochea kuni kwenye moto.
 
Kama hayo yaliyoandikwa ni kweli ameyasema Kinana basi amekosea katika baadhi ya majibu yake. Hapa nitazungumzia kuhusu idadi ya wabunge katika jimbo.
Kinana ametoa mfano wa nchi za Seychelles, Lesotho, Switzerland na Sweden kupinga hoja ya Lissu ya kulinganisha idadi ya wapiga kura na wabunge kutoka Zanzibar na hali ilivyo Tanzania ambako alitoa mfano wa Temeke. Kinana alitakiwa kutoa idadi ya wapiga kura na idadi ya wabunge katika majimbo ya uchaguzi ya nchi alizotaja na sio ya nchi nzima. Lissu hakulalamikia idadi ya wawakilishi katika Baraza la Mapinduzi bali idadi ya wapiga kura katika majimbo yanayotoa wabunge katika Bunge la JMT.
Kosa lingine ni kuwa ukiondoa Switzerland nchi nyingine ni Unitary States.

Tuzungumzie Switzerland. Switzerland ina Cantons 26 ambazo zinatofautiana idadi kutoka watu 16,003 hadi 1,487,969. Switzerland ina mabunge 2 ambayo yote yana nguvu sawa. Kuna National Councilambayo ina viti 200. Viti vinagawiwa kulingana na idadi ya wakazi katika eneo la uchaguzi. Hii ni kama House of Representatives Marekani. Bunge la pili ni Council of States ambapo kila Canton inatoa wawakilishi wawili. Hii ni kama Senate ya Marekani.

Mimi nitatoa mfano wa United Kingdom ambayo nadhani kidogo inafanana na mfumo wetu wa Muungano. UK ni muungano wa nchi nne ambazo ni England, Scotland, Wales na Ireland ya Kaskazini. Nchi zote hizo zina mabunge yao isipokuwa England. Bunge la UK linaitwa House of Commons ( kuna lingine linaloitwa House of Lords). Katika House of Commons yenye viti 650 England ina wabunge 543, Scotland 57, Wales 37 na Ireland ya Kaskazini 18. Jimbo la uchaguzi katika House of Commons linatakiwa kuwa na watu wasiopungua 69,724 na wasiozidi 77,062 isipokuwa kwenye visiwa vya Orkney na Shetland. Ni dhahiri kuwa idadi ya wabunge inatokana na idadi ya watu wanaoishi katika jimbo la uchaguzi na sio idadi ya watu wanaoishi katika nchi husika. Hii ni kwa sababu wabunge ni wawakilishi wa jimbo lao na sio nchi yao.

Tukiangalia mifano hii, idadi ya wabunge katika Bunge letu ilitakiwa kuendana na idadi ya watu wanaoishi katika jimbo bila kujali jimbo liko upande upi wa Muungano.

Kwa mantik hii wabunge kutoka Zanzibar ni wawakilishi wa majimbo yao na sio nchi ya Zanzibar katika Bunge la JMT. Kama tunataka uwakilishi wa Zanzibar basi liundwe Bunge lingine ambalo litakuwa na wawakilishi sawa sawa kutoka kila upande wa Muungano. Kwa mfano, Tanzania Bara inaweza kuwa na wawakilishi 20 na Zanzibar 20 ( Pemba 10 na Unguja 10).

Lissu hakukosea kwenye hili.

Amandla....

JokaKuu
 
We nae unaona eti umeandiiiika na halafu ukaridhika kabisa kwamba umemjibu sawa sawa mh Kinana!! Machagadema mkiambiwa akili zenu ni sawa na nyumbu mnakasirika!
Mimi nitakuwa refa wenu; kati yako na mleta mada.
Hadi hapa tulipo, mleta mada anayo akili safi kabisa mara mia ya hiyo yako, tukitazama tu uandishi wenu.

Watu wa aina yako, ndio mliojazana CCM siku hizi. Hamna uwezo kabisa juu ya jambo lolote. Kilichobaki ni kukaa madarakani kwa nguvu.
 
Umetoa maelezo na mifano mizuri kabisa, hasa hiyo la UK na US
Ireland ni ya Kaskazini.
 
Uko sahihi. Northern Ireland ni Ireland ya Kaskazini. Nimesahihisha nilicho andika.

Amandla...
Ninavyozidi kusoma yanayodaiwa yalisemwa na Kinana, nazidi kuwa na wasiwasi juu ya hawa watu wa CCM.

Hivi kweli Kinana anaweza kusema maneno kama haya yaliyowekwa kwenye kichwa cha mada; kwamba:"Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo sasa hivi; akisema kuanzia leo hakuna maandamano....ITAKUWA NIN"I?

Hajui kwamba watu wanaonyimwa uhuru wanayo haki ya kuutafuta uhuru huo? Kasahau kwamba mikutano na maandamano ni haki inayoruhusiwa na katiba ya nchi? Hajui kwamba ni ukiukwaji wa katiba kiongozi anapozuia uhuru wa watu unaotokana na katiba ambayo ndiyo imewaweka madarakani na kuapa kuilinda katiba hiyo?

Kwa mtu kama Kinana kuwa na mawazo ya aina hii, inaonyesha wazi huko ndani ya chama kuna matatizo makubwa zaidi
 
Nani ameleta uhuru nchini?? Hamuoni aibu mwanaume MZIMA unadai uhuru umeletewa na mwanamama toka nchi nyingine??
LISSU anachotuambia tunahitaji kuirekebisha katiba na tuunde muungano wetu vyema na kilanchi iwe na serikali au serikali iwe moja
 
Hata mimi ndio maana nina wasiwasi kama kweli kayasema. Ukisema Samia kaleta uhuru unamaanisha kuwa kabla yake hapakuwa na uhuru. Sasa kwa vile huo uhuru ni haki ya msingi ya kikatiba ya raia wa JMT ni kuwa anakiri kuwa chama chake (ambapo Rais wa sasa alikuwa Makamu wa Rais wa awamu iliyopita) kimekuwa kikikiuka Katiba katika awamu zote mpaka hii ya sasa! Na kwa vile Kinana amekuwa katika nafasi za juu katika Chama au serikali iliyoundwa na chama chake basi nae alishiriki katika ukiukwaji huo uliowanyima uhuru watanzania!

Amandla...
 
Kwanini hawataki kusema mifano ya nchi ya US, Canada na UK?! Wanaleta mifano ya nchi za ajabuajabu?; uchina?! Kenya?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…