Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Pre GE2025 Kinana: Rais Samia wanayemsema ndio ameleta uhuru uliopo nchini sasa hivi, akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
anachokifanya lisu ni mkakati wa chadema kuligawa taifa

uzuri watanzania si wajinga kwa hilo
 
Mwalimu Nyerere alituasa kuwa makini sana na wanasiasa wanaoutumia dini , kabila na rangi katika kutafuta uongozi. Wanasiasa waliokosa hoja hukimbilia mambo hayo ili kuwahadaa wananchi.
Tundu lissu wa chadema ni mfano Hai wa ambacho alikielezea Mwalimu Nyerere. Watanzania mpuuzeni maana hajui analoongea lina athari gani kwa jamii yetu.
Nyerere ndio alituachia hii katiba ya umungu mtu, na ndio muasisi wa huu muungano wa shuruti. Tunamuelewa vizuri Tundu kuliko huyo Nyerere mnayedhani tulimkubali kihivyo.
 
Mwalimu Nyerere alituasa kuwa makini sana na wanasiasa wanaoutumia dini , kabila na rangi katika kutafuta uongozi. Wanasiasa waliokosa hoja hukimbilia mambo hayo ili kuwahadaa wananchi.
Tundu lissu wa chadema ni mfano Hai wa ambacho alikielezea Mwalimu Nyerere. Watanzania mpuuzeni maana hajui analoongea lina athari gani kwa jamii yetu.
Pole naona mshale umepenya kunako. Milio mnayotoa ni ya kila aina. Tumetoka pia kusikiliza mlio wa babu yako Kinana muda sio mrefu.
Safafi hii mtatoa mikio yote aisee.
 
Bora wangekuwa wanamsema,Sasa wanamtukana.Hata Sasa akiamua kupiga marufuku maandamano hakuna wa kunyanyua mdomo.
Anapewa ukweli wake, anaweza kupiga marufuku tu hata usiku huu. Alipiga marufuku mikutano dhalimu Magu, na bado ilipofika wakati wa uchaguzi aliupora, itakuwa Hawa? Ccm sio chama Cha kizazi hiki, haya mambo ya kulazimisha kwenye kizazi hiki ni kupoteza muda.
 
Lucas mwashamba
1.Kwanini Wabunge wa Zanzibar huwa wanajadili bajeti za Wizara zisizo za Muungano, Kama Wizara ya Kilimo?

2. Kwanini kwenye Baraza la Wawakilishi hakuna Wabunge toka Tanganyika kulinda Maslahi ya Tanganyika?

3.Kwanini Wazanzibar wanakuwa Wakuu wa Wilaya Tanganyika ilihali Watanganyika hawawezi kuwa Znz,assumption kwamba TAMISeMI ipo nchi ya Rais?

4.Kwanini Rais wa Jamhuri akitaka kugawa eneo labda Mkoa au Wilaya,Tanganyika anagawa tu,ila Kwa Zanzaibar ni lazima ashauriane na rais wa Zanzibar?
5.Idadi kamili ya wapiga kura ilikupata Jimbo la Mbunge wa bunge la JMT ni ngapi?

6.Kwanini Sukari bei chini Znz?

7.Kwanini Leseni ya udereva ya Tanzania haikubaliki Znz?

8.Kwanini Mh Rais hakubinafsisha bandari za Znz?..Znz hawataki Ufanisi?

9.Kwanini Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hatambuliki Znz ilihali ni wa Tanzania nzima?

10.Kwanini Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halijawahi kuwa na Spika wala Naibu Spika toka Zanzibar?
 
Anapewa ukweli wake, anaweza kupiga marufuku tu hata usiku huu. Alipiga marufuku mikutano dhalimu Magu, na bado ilipofika wakati wa uchaguzi aliupora, itakuwa Hawa? Ccm sio chama Cha kizazi hiki, haya mambo ya kulazimisha kwenye kizazi hiki ni kupoteza muda.
Mumemkuta Samia analeta huruma za kimama,Makonda alishawaambia angewakomesha ingekuwa awamu ya chuma ,mungesaga meno mara 2.
 
lisu atakuwa anasikilizwa sana na wana ccm kuliko hata chadema wenyewe.....hata akienda chooni kujisaidia ccm watajuzana jamaa kaingia toilet ndicho kinachoendelea sasa....hata kama jamaa anaenda kanisani bado ccm itakuwa na wasiwasi sana. na 2025 haifiki leo mbona watakonda sana mbwa waele
 
Anatafuta fedheha tu, kwa umri wake na alichokula na kuwaibia watanzania angejipumzisha tu ili alinde heshima ila anachokitafuta atakipata tu.
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana amezungumza na waandishi wa habari na wanaCCM katika Dodoma akiangazia masuala mbalimbali ikiwemo hoja mbalimbali zilizoshika kasi hivi karibuni kutoka upande CHADEMA na hasa Lissu. Nilichokiona ni kwamba Kinana kajichanganya na kukoroga zaidi badala ya kupangua hoja, tujadili aliyosema Kinana kwa kurejea kauli zake

1. Katiba na Sheria
Kinana anaposema mambo ya katiba mpya yanahitaji muda na tafakuri, Je ni Muda gani? Miaka mingapi?
Kinana anapaswa kufahamu raia wengi hawataki "blank cheque", wanataka kujua ni wakati gani hasa umepangwa kuipata hiyo katiba mpya. Hapa hatajazungumzia rasimu ya katiba ya Warioba.

Kinana Anasema Katiba yetu imepokea mabadiliko mara 14, na ukitazama madailiko hayo mara nyingi yalilenga siasa, madaraka na uchaguzi, hata msukumo wa sasa wa CHADEMA lengo lake ni uchaguzi.!
Kwa nini Kinana anafikiri haya ni mambo madogo na sio ya muhimu au kipaumbele?
Kinana anayesifiwa ni mmojwapo wa magwiji wa siasa nchini hafahamu siasa, madaraka na uchaguzi amabavyo kwa pamoja vinaunda muundombinu wa utawala wa nchi ndio injini yenyewe ya nchi ?! Hajui mambo hayo ndivyo dhima kuu ya katiba zote duniani?! Au anataka tuweke barabara, madaraja,umeme, maji n.k katika katiba?



Tume ya Uchaguzi na Mamlaka ya Rais
Kinana anasema hajaona nchi ambayo Rais hahusishwi kwenye maamuzi ya Uchaguzi na kwamba hakuna tume ya Uchaguzi Duniani ambayo Rais hana Mamlaka. Kinana afahamishwe zipo nchi za aina hiyo na US ni mojawapo. Hata hivyo hoja ya msingi ni tume huru, Kenya wana tume inayoundwa na Rais laikini ni huru na Wakenya karibia wote hawana malalamiko kwamba tume yao ya uchaguzi sio huru.

Kinana anasema Katiba na Sheria ya Uchaguzi siyo njia pekee ya kushinda uchaguzi, Sera nzuri, Kukubalika kwa chama chako, Kukubalika wagombea wako na kujipanga ipasavyo kwenye uchaguzi kuna mchango mkubwa sana kwenye ushindi! Kinana hafahamu kwamba wapinzani wakati mwingine huwa hawapati hata hiyo fursa au nafasi ya kuingia katika sanduku la kura?!


2. Muungano
Kinana anasema CHADEMA wamekuja na hoja kwamba Zanzibar ni ndogo wakati ina wabunge wengi, Kinana anapotosha kwa makusudi au haelewi hii hoja?
Hoja sio wingi au uchache, hoja ni uwiano sahihi na hili Lisu amesemea hata kwa kulinganisha mkoa wa Lindi na Dar es Salaam katika kukosekana uwaino sahihi.

Kinana anasema wabunge hawaendi bungeni sababu ya idadi ya watu, wanaenda kwa uzito wa hoja!
Kinana katika hili amepotoka vibaya sana, usahihi na inavyopaswa kuwa ni wabunge wanaenda bungeni kwa sababu ya idadi ya watu. Rai wanaweza kumchagua hata mjinga kabisa akawawakilishe bungeni na katika demokrasia maamuzi hayo yanaheshimiwa pia.

Kinana anasema CHADEMA Wanasahau muungano wetu ni wa nchi huru, tumeunganisha nchi mbili, na huu Tunakubali na kukiri hizi ni nchi mbili tofauti zilizoamua kuungana kwa hiyari, zikiwa na ukubwa ardhi tofauti, ukubwa wa uchumi tofauti na ukubwa wa watu tofauti, tukiungana lazima tukubali kuwe na uwakilishi wa kutoka pande zote mbili. Usipime watu kwa udogo wao na ukubwa wao, wapime kwa walivyo, walikuwa huru tukaungana nao anasema Nchi ya Seychelles wako 100,007 wana wabunge 35, Lesotho ina watu 2,300,000 wana wabunge 130, Switzerland ina watu 1,700,000 wabunge wa 246 sawa na Tanzania ambapo sisi ni milini 60 na wabunge 300 , Sweden 10,500,000 wana wabunge 349 kwanini hatuwaulizi? Anasema hoja hii ya CHADEMA haina maana, ni hoja ya kuzua, kukorooga vichwa vya watu, kuchanganya watu, kuleta, uhasama, uchochezi. Aansema Haya yote wanayoongea hayaondoi umasikini wala kuleta maendeleo, basi tu tuvurugane!
Kinana afahamishwe hoja kuu ni UWIANO wa uwakilishi, ikiwa tumeamua kuwa na wabunge 50, 100, 400, 1,000 au hata 3,000 n.k, hoja kuu ni UWIANO wa hao wabunge. Sio sahihi mbunge mmoja anawakilisha raia 5000 halafu mbunge mwingine anawakilisha raia 500,000 katika bunge hilo hilo moja.
Swala la kwmba Zanzibara ina sheria zake hata haikufaa alizungumzie kwa sababu litazua mjadala zaidi hasa katika jambo hili ambalo lina athari na maslahi makubwa kwa upande wa pili pia.


3. Kuligawa taifa katika majimbo
Kinana anasema Duniani nchi nyingi hazina majimbo zina mfumo wa umoja, inaitwa unitary system of government, mfumo wa serikari ya umoja.
Suala sio nchi nyingi, suala ni je mfumo tulio nao unatufaa na kukidhi haja yetu. Hata hivyo nchi nyingi kubwa kama Marekani, India, Russia, Brazil n.k zina mfumo wa majimbo au ni unitary system lakini raia ndio wanachagua viongozi wa mikoa na wilaya zao na sio Rais anachagua kila mtu katika kila nafasi.


Rais Samia ameleta uhuru nchini
Kinana anasema Rais huyu wanayemsema, Rais Samia na mtakubaliana na mimi ndiye aliyeleta uhuru ulioko sasa hivi nchini, uhuru wa kusema, kushutumu, kuandamana, uhuru wa mikutano ya hadhara, nina hakika watajibu watasema lakini ipo kwenye katiba, kwani huko nyuma waliponyimwa katiba haikuwepo? Walikwenda barabarani? Katiba ilikuwepo, uhuru huo ulikuwepo lakini ulipigwa marufuku na hawakwenda barabarani. Sasa amekuja kiongozi muungwana amesema katiba inaruhusu na mimi naondoa kifungo kile mlichokuwa mmefungwa kuzuiwa kutumia uhuru wenu halafu wanasema hapana, unajua hii ipo kwenye katiba siyo kwamba ameturuhusu. Leo hii akisema kuanzia leo hakuna maandamano itakuwa nini?
Kinana hafahamu haya anayojivunia ndio chanzo hasa cha watu kutaka katiba mpya?! Rais kuweza kuzuia haki zilizoko ndani ya katiba ndio udhaifu hasa wa katiba yenyewe, sababu zake zinaweza kuwa nyingi ikiwemo na Rais kuteua wakuu wa polisi bila check yeyote, mahakama kutoweza kumshughulikia Rais n.k
Kinana afahamu kwamba tungekuwa na katiba imara ingempa hata yeye fursa ya kushitaki makampuni ya simu yaliyowafanyia udukuzi katika maongezi yao binafsi yeye, Yusuph Makamba na Nape wakipiga soga tu.
 
Honestly, amekoroga mambo zaidi badala ya kuyatuliza. Hajajibu hoja hata Moja.

Kinana na CCM yake kama kawaida yao, kaja na utaratibu wao uleule wa miaka nenda rudi........... kupiga propaganda uchwara ktk mambo ambayo Watanganganyika wanataka majibu!

Huku ni kukimbia hoja na kuahirisha matatizo tu.

Shame on them!!

Very sad kuwa, Kinana na CCM yake anadhani Watanganganyika bado ni wajinga kama walivyo wao.

Nadhani hapa ni kama tu ndo kamchokoza Tundu Lissu na CHADEMA na sisi wengine tunaotaka katiba mpya!!.

Atajibiwa na kuwashiwa moto mkali zaidi
 
Huyu mzee yuko overrated sana katika siasa za CCM lakini hana credibility yoyote katika ustawi wa Tanzania.
Ni aibu kubwa kumtegemea mtu wa aina hii kwa karne hii... Mzee Kinana kaingizwq 'chaka' na wajanja ..hapa atakapotokea Lissu ,akazichambua hoja mfu kwa mapana ..tutaambiwa kawakosea heshima ..natamani kusikia kauli za kisheria toka Serikalini.
 
Hatuhutaji huruma ya mtu yoyote, tunataka katiba iheshimiwe. Huyo Makonda ni mlevi wa madaraka, wala sio sehemu ya mifano ya siasa za ushindani.
Siasa za ushindani si ndio? Subiria Samia atoke mtakoma ,nasubiria Kwa hamu sana kusikia vilio nitawakumbusha tuu
 
Back
Top Bottom