Kinga kwa Rais aliyeko madarakani na wastaafu ni kichocheo cha uvunjaji haki, Iangaliwe upya

Tatizo ni Katiba yetu Mkuu,tukipata Katiba Mpya yenye Meno na imani mambo yatakaa vizuri,pamoja na Raisi kuondolewa kinga kuna hili eti Tume ya Uchaguzi ikishamtangaza Raisi hakuna mamlaka inayoweza kuhoji hii imekaa vibaya sana ikumbukwe hakuna aliye juu ya sheria tunahitaji katiba mpya mkuu.
 
Katiba ya sasa ipo wazi kwenye hilo. Inaweza kupelekwa hoja ya kuondoa kinga ya Rais mstaafu ili ashitakiwe. Zambia walishawahi kufanya hivyo kwa short chassis Chiluba.
Hii kinga haina manufaa yoyote kwa nchi ila wabunge wetu wamekosa uzalendo na kuwaona hawa maraisi kama miungu watu wakati hii kazi waliomba wenyewe na baadae wakala kiapo cha uaminifu kwa Jamuhuri.
 
Bahati mbaya sana hata Katiba ya mzee Warioba na katiba inayopendekezwa zote zimebeba huu ujinga wa Kinga ya Raisi.
 
Mie napinga, nachosema watete mchakato mpya wa katiba mpya, vyote hivyo vitajibiwa humo. Kutoa kinga ya rais bado haijatatua tatizo la Dira la taifa letu i-wapi
hapo hujapinga ila umetoa tu the very easy and general solution ya hii issue
 


Naunga mkono hoja
 
Kuwatetea wajinga ni kazi kubwa mno. Nyerere alijua yote hayo ila akaona atuache tu
 
katiba ya warioba ilitaka hiyo kinga iondolewe ila mafisiem yakapinga
 
Hiyo kinga iondolewe ili nchi hii kila MTU awe na nidhamu,, naunga mkono hoja
 
Kama ulikuwepo kwenye kijiwe chetu cha jana mkuu! Hili suala tulilijadili sana kuwa wakati sasa umefika wa bunge kumwondolea kinga rais na kumpunguzia madaraka! Ifike wakati wabunge waweke vyama kando na kuungana katika mambo muhimu kama haya.
Kama wanavyoweka vyama kando na kuungana kwenye suala la posho?
 
Kinga isiondolewe......
Kuna umuhimu mkubwa wa Kinga kuwepo
 
Mimi ningekuwa Rais nisingetoa kinga
 
Katiba ya sasa ipo wazi kwenye hilo. Inaweza kupelekwa hoja ya kuondoa kinga ya Rais mstaafu ili ashitakiwe. Zambia walishawahi kufanya hivyo kwa short chassis Chiluba.
Kwa Tz hayawekani maana vyama vya siasa havipendi kuona mtu anayetoka chama chao anashitakiwa mf.rasimu ya katiba ya Warioba iliweka kila kitu lakini wabunge wa chama fulani wakatumia uwingi wao kuikataa nchi ya wajinga itabaki hivihivi hadi akili ziwarudie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…