Ili kuleta uwajibikaji kuanzia Ikulu mpaka ofisi ya serikali mtaa, nawashauri wabunge wa CCM na wale wa UKAWA kuungana pamoja na kuifutilia mbali kinga ya Raisi.
Marekebisho hayo pia yaruhusu hata maraisi waliostaafu huku wakiwa na hii kinga nao waweze kushitakiwa iwapo kutakuwa na tuhuma zinazowahusu na zinazostahili wao kufikishwa mahakamani.
Ni matumaini yangu kuwa Magufli atakuwa wa kwanza kuunga mkono hoja/hatua hii kama kweli anaamini katika usawa na anataka kuridisha nidhamu serikalini.
Tujifunze kutoka Afrika kusini kwani inawezekana watu aina ya Zuma waliwahi ishi pale magogoni au wakaja kuishi siku zijazo.
NB:Nimeleta habari kuunga mkono wazo la mwandishi,Prudence Karugendo katika makala yae katika gazeti la Mwanahalisi la leo iliyoko katika ukurasa wa 14 wa gazeti hilo.Makala hiyo mwandishi ameipa kichwa cha habari kinachosomeka: "JPM atumbue kinga ya maraisi wastaafu."
Tofauti na alivyopendekeza mwandishi Karugendo,mimi nimeona ni vizuri hoja hii ianzie Bungeni moja kwa moja badala ya kusubri serikali ndio ipeleke hoja hiyo Bungeni ili kumtomjenga raisi uadui unaoweza kujitokeza baina yake na watangulizi wake.