Wakuu habari....
Kwa jinsi serikali ya awamu ya nne ilivyovurunda hasa kwenye matumizi mabovu ya fedha na rasilimali za wananchi, natamani Rais kama mkuu wa nchi, kiongozi mkuu wa serikali ashitakiwe mahakamani.
Lakini nimesoma katiba yetu ibara ya 46 kifungu cha kwanza hadi cha tatu vinasema nimarufuku kumshitaki rais akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu kutokana na makosa aliyotenda akiwa madarakani.
vifungu vyenyewe ni kama kama vifuatavyo...
46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.
(2) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, haitaruhusiwa kufungua mahakamani shauri kuhusu jambo lolote alilolitenda au alilokosa kulitenda yeye binafsi kama raia wa kawaida ama kabla au baada ya kushika madaraka ya Rais, ila tu kama angalau siku thelathini kabla ya shauri kufunguliwa mahakamani, Rais atapewa au ametumiwa kwamba taarifa ya madai kwa maandishi kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na taarifa hiyo ikiwa inatoa maelezo kuhusu chanzo cha shauri hilo, kiini cha madai yenyewe, jina lake na anwani ya mahali anapoishi huyo mdai na jambo hasa analodai.
(3) Isipokuwa kama ataacha kushika madaraka ya Rais kutokana na masharti ya ibara ya 46A(10), itakuwa ni marufuku kumshtaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.
Sasa nauliza je bunge linaweza muondolea Rais mstaafu kinga ya kutokushtakiwa mahakamani??
Naomba ufafanuzi wa kisheria tafadhali....