Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Utawala wa demokrasia unaharakisha maendeleo.

Utaratibu tulijiwekea sasa haupelekei kuwepo kwa demokrasia. Kwanza kunatakiwa kuwe na itashi wa kisiasa kuwa ncho iwe ya demokrasia hata kabla ya kuangalia mifumo.
 
Daaa!!!aisee hii serikali ishaziba masikio nahawezi kubadilika kamwe kwani usizani hayo yanatendeka kwa kutokujua wanajua kabisa kilakitu nimakusudi ili kuitete ccm.
Over
 
Kwa haya yaliyotokea yameshaonesha kuwa hali ya kisiasa Tanzania ipo ICU.

Sasa hawa watu wameshaonja harufu ya damu. Wao kuuwa mtanzania mwenzao kisa madaraka ni kitu cha kawaida sana.

Sasa basi mi nashauri kama vipi achaneni na siasa. Tafteni kazi nyingine kama mtashindwa kuomba Tume huru ya uchaguzi.

Tunapoteza pesa, nguvu, na hata Watanzania wenzetu kwa chaguzi zisizokuwa zinazingatia haki na uhuru wa watanzania.

Acheni wajitawale wenyewe. Wafanye watakayo na tuone watafika wapi.
 
Hamna cha Tume Huru wala nini. Wapinzani hamkubaliki na siasa zenu za fujo na kususa susa. Jipangeni upya, ndio dawa.
 
Jamanii qweli hasa huu ni upuuzi kabisa katika siasa ya tz
 
Chama chochote makini cha siasa kitahakikisha panakuwepo na Tume huru ya uchaguzi katika nchi/ eneo wanalofanyia siasa. Hii ni tofauti kabisa hapa Tanzania, vyama vya siasa viko busy kugombea ruzuku na nyakati za uchaguzi wanasababisha machafuko kwa kisingizio cha kutotendewa haki na wasimamizi wa uchaguzi. Ndipo najiuliza Chadema kwa mfano hawajui kwama wakurugenzi wa wilaya ni makada?......na kama wanajua kwanini wanaingia uchaguzini? Hizi siasa za kula ruzuku zimepitwa na wakati na wala sishangai kuona vyama vya upinzani vikipukutika kila iitwapo leo!
 
Unataka chadema wapiganie
Tume huru ili iwejeee hapa tulipofikia panatoshaaa.

Tunachoomba vyama vingi vifutweeeee
 
sio kweli, jamaa waliwahi na wanalizungumziaga eneo hili, na bila katiba mpya wameona hawaliwezi eneo hili, na katiba mpya ndio suluhisho ya tume huru ya uchaguzi!
 
sio kweli, jamaa waliwahi na wanalizungumziaga eneo hili, na bila katiba mpya wameona hawaliwezi eneo hili, na katiba mpya ndio suluhisho ya tume huru ya uchaguzi!
Waliwahi lini?!......ile ya kwenye katiba mpya ilikuwa ni kazi ya kina Polepole siyo wapinzani. Nadhani kuna kitu kinaogopwa na wapinzani kuhusu Tume huru ya uchaguzi!
 
Waliwahi lini?!......ile ya kwenye katiba mpya ilikuwa ni kazi ya kina Polepole siyo wapinzani. Nadhani kuna kitu kinaogopwa na wapinzani kuhusu Tume huru ya uchaguzi!
Teh, hapana! tena hakuna kitu wanaogopa! wee unadhani wanaogopa nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…