Kingunge: Bila tume huru, wapinzani wasahau kuingia Ikulu

Una mawazo mazuri sana, lakini angalia na wakati tulionao. Wapinzani wanajitahidi kwa kadri ya uwezo wao, wanachokosa ni uungwaji mkono kutoka kwa wananchi, na hili ndio tatizo kubwa sana tulilo nalo.
Mtazamo wangu ni wao kwa umoja wao kuongeza mapambano ya kisheria kudai haki zao (haki zetu) kama wanavyofanya wadau wa matumizi ya mitandao katika kuipinge sheria ya mtandao na kanuni zake.
 
kuna mahali unaweza kuwalaumu na kuna mahali ,lazima tuweke uliganifu nao ni oama ifuatavyo:
1) Suala la kisheria kuhusru marekebisho ya katiba na sheria ,mahakana zetu hazina spidi hiyo unaweza anzisha kesi ikaisha uchaguzi mwingine umekwisha.Na hata ukishinra utekelezaji wake utahitaji marekebisho kupelekwa bungeni ;kule bumgeni inakuwaje,wabunge wengi ni wa ccm mabadiriko hayawezi kupatikana bungeni kupitia wabunge wa ccm.
2) Kupitia majukwa naharakati zingine ,uzoefu tumeuona hata mikutano ya ndani nayo n kosa imezuiliwa ,ukifqnya ni kesi ya mkuwanyiko usio halali au uchochezi.
3) Machapisho na mitandao je sheria zilizopo ni rafiki? ukifanya kesi mahakamani kosa la uchochezi.
kuna mahala siasa zatanzania ni taabani
 
Huwa tukiwaambia wapo kwaajili ya maslahi yao mnatubishia. Na swala la kubadili gia angani 2015 tuliwaambia litawagharimu miaka 50 ijayo, jamaa alikuja kuwafunga speed governor akawaambia hakuna haja ya uanaharakati.Ndo mnayoyaona Leo.. Kila mtu kimya kwenye chama.Mtamkumbuka Dr.Slaa ALWAYS.
 
Swali zuri sana na lenye jibu chungu.

Mkuu,mimi sioni haja ya wao kuendelea kushiriki uchaguzi ambao kila baada ya matokeo ni kulalamika tu.
Unaamini kutoshiriki/kususia uchaguzi ndio njia itakayosaidia kupatikana kwa Tume Huru?
 
kuna mahali unaweza kuwalaumu na kuna mahali ,lazima tuweke uliganifu nao ni oama ifuatavyo:
1) Suala la kisheria kuhusru marekebisho ya katiba na sheria ,mahakana zetu hazina spidi hiyo unaweza anzisha kesi ikaisha uchaguzi mwingine umekwisha.Na hata ukishinra utekelezaji wake utahitaji marekebisho kupelekwa bungeni ;kule bumgeni inakuwaje,wabunge wengi ni wa ccm mabadiriko hayawezi kupatikana bungeni kupitia wabunge wa ccm.
2) Kupitia majukwa naharakati zingine ,uzoefu tumeuona hata mikutano ya ndani nayo n kosa imezuiliwa ,ukifqnya ni kesi ya mkuwanyiko usio halali au uchochezi.
3) Machapisho na mitandao je sheria zilizopo ni rafiki? ukifanya kesi mahakamani kosa la uchochezi.
kuna mahala siasa zatanzania ni taabani
Umeongea vema. Nadhani watu waangalie kwanza hali halisi ya kisiasa iliyopo nchini kabla ya kulaumu.
 
Ukiwaambia hivi wanakuwa wakali sana.

Sasa wakae wakijua kuwa 2020 wabunge wa upinzani watakaorudi bungeni ni wale atakaoamua Jiwe.

Jimbo la sugu 'linachukuliwa' na Tulia.
Wewe huku sio dar labda sisi wananchi tuhamue
 
Unaamini kutoshiriki/kususia uchaguzi ndio njia itakayosaidia kupatikana kwa Tume Huru?
Tatizo la vyama hivi vya upinzani vipo kibiashara zaidi.

Wakijipanga wote wakasusia uchaguzi watapata tu.
Hawapati tume huru kwasababu wamekuwa wakilalamika tumeibiwa tumeibiwa huku wakiendelea kujipa moyo uchaguzi ujao tunashinda.

Hiyo ndio inawapa moyo watawala na kuendelea kuwaona wajinga.

Hivi vyama vinaendeshwa kama biashara,jicho likiwa kwenye kiasi cha ruzuku.
 
Wana JF,
Huu ni ushauri wa bure kwa Upinzani Tanzania.
Kwamba hapa tulipofikia kwa sasa hakuna haja tena ya kuweka wagombea kwenye chaguzi zote zinazokuja kuanzia hizi za marudio, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020

Sababu iko wazi kabisa kuwa kwa sasa hakuna kiti cha UDIWANI, UBUNGE au URAIS ambao upinzani wanaweza kushinda kwa mazingira tuliyo nayo. Uchaguzi mdogo uliopita juzi iwe ni benchmark, kwamba viti 77 Udiwani na 1 Ubunge CCM wameshinda kwa 100% kwa mbinu chafu. Nashauri Wapinzani warudi kwenye sanduku la kura pale tu Magufuli, CCM na Serikali yake watakapokubali kufanya mabadiliko ya Kikatiba kuhusu sheria ya Uchaguzi inayohusu TUME HURU YA UCHAGUZI kwa kuondoa WAKURUGENZI kuwa wasimamizi wa Uchaguzi na kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kuweka mkazo na msisitizo wa kubadili Katiba kwa kutumia media na Jumuia za Kimataifa kwa kuelezea bayana kwamba Tanzania hakuna Demokrasia tena na CCM wanatawala kibabe. Viongozi wa Upinzani nendeni kwenye Jumuia na Mataifa ya nje kuelezea hali halisi ilivyo Tanzania, vinginevyo mtaendelea kutwanga maji kwenye kinu huku CCM wakiendelea kutawala milele na milele!!!
 
Si mlitaka Rais Mbabe na sasa kapatikana hapa tunasema upele umemuota mwenye kucha kazi kwake sasa kuukuna.

JK alidharauliwa sana na yeye akaona isiwe taabu ngojeni niwafundishe maisha.
 
Wana JF,
Huu ni ushauri wa bure kwa Upinzani Tanzania.
Kwamba hapa tulipofikia kwa sasa hakuna haja tena ya kuweka wagombea kwenye chaguzi zote zinazokuja kuanzia hizi za marudio, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020

Sababu iko wazi kabisa kuwa kwa sasa hakuna kiti cha UDIWANI, UBUNGE au URAIS ambao upinzani wanaweza kushinda kwa mazingira tuliyo nayo. Uchaguzi mdogo uliopita juzi iwe ni benchmark, kwamba viti 77 Udiwani na 1 Ubunge CCM wameshinda kwa 100% kwa mbinu chafu. Nashauri Wapinzani warudi kwenye sanduku la kura pale tu Magufuli, CCM na Serikali yake watakapokubali kufanya mabadiliko ya Kikatiba kuhusu sheria ya Uchaguzi inayohusu TUME HURU YA UCHAGUZI kwa kuondoa WAKURUGENZI kuwa wasimamizi wa Uchaguzi na kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kuweka mkazo na msisitizo wa kubadili Katiba kwa kutumia media na Jumuia za Kimataifa kwa kuelezea bayana kwamba Tanzania hakuna Demokrasia tena na CCM wanatawala kibabe. Viongozi wa Upinzani nendeni kwenye Jumuia na Mataifa ya nje kuelezea hali halisi ilivyo Tanzania, vinginevyo mtaendelea kutwanga maji kwenye kinu huku CCM wakiendelea kutawala milele na milele!!!
Kuna tatizo kubwa Tz la vyama mamluki, kama tlp ya mrema; na kile cha dovutwa; na vingine vingi vidogvidogo. Usishangae vikashiriki uchaguzi na kushindishwa katika baadhi ya maeneo.
Halafu ccm ikautangazia ulimwengu kwamba Tanzania kuna demokrasia; na kuna uchaguzi huru na wa haki.
 
Mkuu uko sawa... hakuna haja ya kutoana macho na kukosa viungo vya mwili, kwa sasa kura haiamui nani awe kiongozi.

Nasizitiza kutafuta KATIBA mpya ndiyo kipawo mbele kwa sasa.
 
Hilo hawawezi kulifanya kamwe kwani Mbowe anahitaji ruzuku kuliko chochote Dunia hii, hivyo wataendelea tu kuwazuga na kuwadanganya lkn ukweli ni kwamba Mbowe na Uongozi Mkuu wa chadema haujali chochote isipokuwa fedha yetu tu, na ndiyo maana pmj na malalamiko yao yote hawawezi kususia uchaguzi kwani Tume yetu pia haitawapa fedha yetu!
 
Wakisusia kuna wapinzani kina Cheyo et al watagombea na utaitwa uchaguzi ulioshirikisha wapinzani,we unadani mchezo?
 
Hilo hawawezi kulifanya kamwe kwani Mbowe anahitaji ruzuku yetu kuliko chochote Dunia hii, hivyo wataendelea tu kuwazuga na kuwadanganya lkn ukweli ni kwamba Mbowe na Uongozi Mkuu wa chadema haujali chochote isipokuwa ruzuku yetu tu, na ndiyo maana pmj na malalamiko yao yote hawawezi kususia uchaguzi kwani Tume yetu pia haitawapa ruzuku yetu!

Hapo nachoona mnajito akili tu. Hawa wanaoongelea CDM kujitoa ndio waliotupa mawe mengi CDM walipogomea uchaguzi hapo nyuma sasa hivi wanageuza kauli as if wame format vichwa. Kama CCM wangekuwa na akili wangesikitika Upinzani kujitoa. Angali yaliyotokea ZNZ baada ya Seif kujitoa. Halafu useme tena CDM wagomee uchaguzi.
 
Wapinzani wa Tanzania hawatakubari kuacha pesa wanazopewa kwa ajili ya chaguzi. Hawako kwa ajili ya kishinda mkuu. Ndiyo sababu malalamiko yaleyale ya 1995 hadi leo wanayarudiarudia tu
 
Naunga mkono hoja. Hakuna tume ya uchaguzi huru hakuna kushiriki uchaguzi.
 
Wana JF,
Huu ni ushauri wa bure kwa Upinzani Tanzania.
Kwamba hapa tulipofikia kwa sasa hakuna haja tena ya kuweka wagombea kwenye chaguzi zote zinazokuja kuanzia hizi za marudio, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020

Sababu iko wazi kabisa kuwa kwa sasa hakuna kiti cha UDIWANI, UBUNGE au URAIS ambao upinzani wanaweza kushinda kwa mazingira tuliyo nayo. Uchaguzi mdogo uliopita juzi iwe ni benchmark, kwamba viti 77 Udiwani na 1 Ubunge CCM wameshinda kwa 100% kwa mbinu chafu. Nashauri Wapinzani warudi kwenye sanduku la kura pale tu Magufuli, CCM na Serikali yake watakapokubali kufanya mabadiliko ya Kikatiba kuhusu sheria ya Uchaguzi inayohusu TUME HURU YA UCHAGUZI kwa kuondoa WAKURUGENZI kuwa wasimamizi wa Uchaguzi na kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani.

Kinachotakiwa kwa sasa ni kuweka mkazo na msisitizo wa kubadili Katiba kwa kutumia media na Jumuia za Kimataifa kwa kuelezea bayana kwamba Tanzania hakuna Demokrasia tena na CCM wanatawala kibabe. Viongozi wa Upinzani nendeni kwenye Jumuia na Mataifa ya nje kuelezea hali halisi ilivyo Tanzania, vinginevyo mtaendelea kutwanga maji kwenye kinu huku CCM wakiendelea kutawala milele na milele!!!
Kuvuja kwa pakacha........, na bado, maji mtayaita mmah !
 
Mkishindwa kwenye kura mnaeneza propaganda,mbona maneno hayo mmesema siku zote na kuziomba taasisi za kimataifa kutoipa misaada Tanzania lkn ndo kwanza pesa inamwagwa na kuusifia utawala wa Magufuli,mnachotaka hatujui ni kitu gani. Upinzani umekuwa dhaifu sana maana hakuna hoja za msingi wanazojadili bali ni kulalamika tu kama mazezeta. Huku mitaani kila Mwananchi hamalizi siku bila kumtaja Magufuli kama shujaa wa nchi hii. Heshima imerudi kwa kiwango cha hali ya juu kwa watumishi wa Serikali wanapowahudumia Watanzania kitu ambacho kimeongeza tija kwa kiwango kikubwa na mengine mengi tu
 
Hilo hawawezi kulifanya kamwe kwani Mbowe anahitaji ruzuku yetu kuliko chochote Dunia hii, hivyo wataendelea tu kuwazuga na kuwadanganya lkn ukweli ni kwamba Mbowe na Uongozi Mkuu wa chadema haujali chochote isipokuwa ruzuku yetu tu, na ndiyo maana pmj na malalamiko yao yote hawawezi kususia uchaguzi kwani Tume yetu pia haitawapa ruzuku yetu!

Barbarosa,
Acha porojo za ki-Abunuwasi baali unatakiwa kuongea kitu chenye mashiko.
Unachoongea ni umbeya ambao huwezi kuuthibitisha.Mbowe hana njaa ya ruzuku kama unavodai. Ruzuku iko kisheria kulingana na idadi ya Madiwani na Wabunge kilio nao chama. CHADEMA hata isipoingia kwenye Uchaguzi wa marudio ruzuku yake ipo palepale mpaka 2020 labda huo mpango wenu wa CCM kununua Madiwani na Wabunge wote watakapohamia CCM ndipo CHADEMA WATAKOSA RUZUKU...!!
 
Back
Top Bottom