Wana JF,
Huu ni ushauri wa bure kwa Upinzani Tanzania.
Kwamba hapa tulipofikia kwa sasa hakuna haja tena ya kuweka wagombea kwenye chaguzi zote zinazokuja kuanzia hizi za marudio, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020
Sababu iko wazi kabisa kuwa kwa sasa hakuna kiti cha UDIWANI, UBUNGE au URAIS ambao upinzani wanaweza kushinda kwa mazingira tuliyo nayo. Uchaguzi mdogo uliopita juzi iwe ni benchmark, kwamba viti 77 Udiwani na 1 Ubunge CCM wameshinda kwa 100% kwa mbinu chafu. Nashauri Wapinzani warudi kwenye sanduku la kura pale tu Magufuli, CCM na Serikali yake watakapokubali kufanya mabadiliko ya Kikatiba kuhusu sheria ya Uchaguzi inayohusu TUME HURU YA UCHAGUZI kwa kuondoa WAKURUGENZI kuwa wasimamizi wa Uchaguzi na kuhoji Matokeo ya Urais Mahakamani.
Kinachotakiwa kwa sasa ni kuweka mkazo na msisitizo wa kubadili Katiba kwa kutumia media na Jumuia za Kimataifa kwa kuelezea bayana kwamba Tanzania hakuna Demokrasia tena na CCM wanatawala kibabe. Viongozi wa Upinzani nendeni kwenye Jumuia na Mataifa ya nje kuelezea hali halisi ilivyo Tanzania, vinginevyo mtaendelea kutwanga maji kwenye kinu huku CCM wakiendelea kutawala milele na milele!!!