Gangongine
JF-Expert Member
- Dec 31, 2015
- 3,854
- 1,776
Hata kuwe na Tume Huru hawana Wagombea zaidi ya kuokoteza makapi ya CCM!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe unaweza kujua mama ako kalala vipi chmbani kama si babako Kuamka na kusema kama mamaako anaumwa ndaniHuyu mzee si alikuwa kwenye bunge la katiba, wanazingua, waongee wengine si hawa
Mkuu wkt mwingine kauli ya JPM ya wazee ndo wametufikisha hapa, huwa INA mashiko!Ni mwanzilishi, mlezi, mtetezi, chief strategist & propagandist na think tank iliyozaa mfumo huu huu anaoulalamikia sasa. Amekula wee na kufaudu mumo kwa mumo wakampa ulaji pale stendi ya Ubungo yeye na wanae. Walipomnyang'anya tu huyooo akalamba hela za Eddo akageuza gia angani. Bunge la katiba JK anaichakachua katiba mpya laivu yuko kimyaaa leo hii ati ndiye mwanaharakati.
Wanasiasa wa Tanzania hawa wachumia tumbo tu na ni wachache sana ambao wameweka matakwa ya taifa mbele. Haiwezekani mtu utumikie mfumo ule ule kwa miaka 70 na jioni kabisa huku ndo ujifanye mwanaharakati. Hopeless kabisa!!!
Exactly pal!!I think, he would be best legendary if he would retire from this youth politics gentleman [emoji124]
Namuona huyo anaekoroga hapo begi lake alilokuwa kalivaa mgongoni kalitupa chini ili apate kuisikilizia chai ya ikulu bila usumbufu...Chai ya ikulu tamu wewe. Hebu muone Prof. alivyo makini utafikiri hajawahi kunywa chai maishani. Badala ya kusubiri mwenyeji aionje kwanza ili kuhakikisha haina sumu, wenyewe hata wafe sawa tu.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na Katiba Mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Kauli ya Kingunge imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.
Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.
Mbali na mwenyekiti kuteuliwa na Rais, wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ni wakurugenzi wa wilaya ambao pia huteuliwa na Rais kwa kuwa NEC haina wafanyakazi wake kote nchini.
Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.
Kingunge, aliyetumia muda mrefu kueleza historia ya maisha yake katika siasa na jinsi alivyopambana katika harakati za kudai uhuru, alisema hali ya sasa ni mbaya kuliko wakati wa wakoloni wa Kiingereza ambao walikujwa wakali, kwa sababu CCM haifuati Katiba wala sheria.
“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977. Tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema.
Kingunge ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya waziri anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na mkuu wa mkoa alisema, “(Pia) Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana.”
Alisema pamoja na kwamba Chadema inapendwa na wananchi wengi na Edward Lowasa aliyegombea urais kwa tiketi chama hicho, anapendwa, bado ni vigumu kushinda kwa sababu mfumo uliopo sasa.
“Tufanye yoyote, lakini tuhakikishe, ama tunapata Katiba Mpya au vipengele hivi vya sheria vinafanyiwa marekebisho. Kwa maoni yangu, kundi hili lililo madarakani bila shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi, halitataka mabadiliko,” alisema.
Alisema enzi zao walifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitolea kwa nguvu na wengine, na yeye akiwamo, waliacha kazi za mishahara mikubwa na kujiunga na Tanu kupigania uhuru.
“Tulifanikiwa kupata uhuru kwa sababu walijitoa mhanga. Wengi tu waliacha kazi, mtu anamaliza chuo kikuu anasema sitaki kazi anaingia Tanu kusaidia. Kwa hiyo tukawa na jeshi kubwa la vijana waliohakikisha nchi inapata uhuru,” alisema.
“Ninyi mnapambana katika mazingira magumu na wazee wenzenu walipambana katika mazingira hayo. Haikuwa rahisi. Wapo wengi walitusaliti, wengine hawakufanya lolote. Baba yangu tuligombana, nilipoacha kazi kwenda kuitumikia Tanu. Miezi sita hatukuzungumza.”
Akizungumza mkutano huo, Lowassa, ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, aliwatia moyo vijana walioshtakiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, akisema bado jeshi kubwa la vijana linahitajika.
“Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo na yajayo. Si haki kusema unakwenda mahali pengine, mwenzako amepasafisha, safisha pa kwako. Nimefurahia moyo huo. Kama alivyosema Ngombale, tunataka jeshi kubwa zaidi, watu wengi zaidi,” alisema Lowassa.
View attachment 449805
Wamejenga uwanja wa ndege Chato? wamejigawia nyumba za serikali? wameitia hasara serikali kiasi gani ukilinganisha na hasara alizoitia nchi huyu mhe sana ?.... Nenda shule ...Kinguge na Lowasa mmeshiriki kufilisi nchi ni bora mkae kimya kupisha wengine.
Hata sisi tulikuwa kwa age hiyo na vimitazamo vya ukawa ila inafika sehem unaona kwa usahihi, ndo maana ni muhimu NEC ikawa na back up, tusije tukajikuta tunachaguliwa raisi na minors.CCM wenzangu angalieni, fanyeni tafiti kujua ktk vijana wenye age ya 13, 14, 15, 16 na 17 kwa asilimia wangapi wanaunga mkono CCM na wangapi wako upinzani. Mwaka 2020 ndio wataamua nani awe rais wa Tanzania.
Mkuu asante, changamoto kubwa ambayo ipo, haitowezekana kupata watu wenye sifa hzo, na ikitokea tutakuwa hatuna rais maaana itakuwa tunashinda mahakamani,Tume huru ni tume ambayo haiwezi kuingiliwa kwa vyovyote na mtu yeyote.Ni tume ambayo mwenyekiti wa tume anaajiriwa na kufanya interview na kuidhinishwa na bunge na kukubalika na pande zote na asiwe ni mwanachama wa chama chochote na asiwe mteule wa rais(Je waweza kwenda kinyume na mteule wako).Muundo wa tume iwe na wajumbe toka vyama vyote!!.Zanzibar pamoja na figisu zote tume yao kwa kiasi kikubwa ilikuwa huru!!!. Nafikiri umenipata vema!! Happy exmas and ny!!!!😉😉😉😉😉😀😀😀😀
Yaah hata kama ameshakufa.uumbaji unaendelea ila sijui kama matunda yanakuwepo pia!!!!mwanadamu uendelea kuumbwa kila siku
Better vote because if you don't vote is the worst decision, sensitise as many people as possible to voteBila tume huru ya uchaguzi! I will never vote again!
... Ni kweli alikuwa mjumbe wa BMK kutoka kundi la waganga wa kienyeji. Mchango wake Nakumbuka haukusaidia kupata Katiba yenye kuzingatia maoni ya wananchi. Hata hivyo hiki alichokisema leo ndiyo ukweli halisi na Natumaini atakuwa anajutia kutoitumia vizuri fursa ile aliyoipata kwenye lile bunge...Huyu mzee si alikuwa kwenye bunge la katiba, wanazingua, waongee wengine si hawa
... Bila ku quote the whole text you will still never vote again?Bila tume huru ya uchaguzi! I will never vote again!
No free and fair election in africa except Ghana! I will never vote again without free and fair election comitee…Better vote because if you don't vote is the worst decision, sensitise as many people as possible to vote
Mwalimu Nyerere alisema mpinzani wa kweli atatoka CCM, hata hivyo Mwalimu Nyerere ndie aliyefuta mfumo wa vyama vingi baada ya Uhuru na pia ndie aliyependekeza na kuurudisha mfumo wa vyama vingi miaka ya 90 kiasi kwamba kila mtu anamsifu Mwalimu Nyerere hadi leo ,sasa iweje tumbeze Kingunge?
Hapo kwenye mfia chama umekosea. Tena umekosea sana.Mkuu najua wewe ni mfia chama ila tuweke uzalendo kidogo. Hawa akina Kingunge hawa? Umesahau hasira zake zilianzia wapi? Akina Mahanga? Umemsahau mkuu? Masha? Muulize Wenje! Mmekatisha wengi tamaa! Wengi wasiojua muda utaongea tu. Tatizo si kukosea ...bali baada ya makosa mnafanya nini! Ukisoma historia ya kanisa unakumbuka hakuna mtikisiko mkubwa uliopasua kanisa kama ule wa Martin Luther ....pamoja na Kanisa kuamini Luther alikosea lakini walijitathimini na kufanya marekebisho pale walipoona kulikuwa na hoja. Chadema inapaswa kufanya marekebisho makubwa yatakayorudisha mwamko upya. Tuache kutetea kila kitu tuseme ukweli chama kipone...