Kinyozi wa kike apandisha mashetani na kuzimia baada ya kugusa kichwa cha askofu Gwajima, aombewa na kuzinduka!

Kinyozi wa kike apandisha mashetani na kuzimia baada ya kugusa kichwa cha askofu Gwajima, aombewa na kuzinduka!

Hivi kweli kuna watu ni wajinga kiasi hiki mpaka umeamua kutunga story. Ukitaka kutanga story leta story hata inaenda na ukweli zaidi ili watu tuamini sio kwa upuuzi huu
 
Askofu Gwajima akihubiri kanisani kwake amesema leo asubuhi wakati anakwenda hapo ibadani alipitia saluni kusafisha kichwa chake.

Alipoingia saluni na kuketi dada mmoja alimjia kwa nyuma na kujaribu kugusa kichwa chake lakini ghafla akaanza kuweweseka kama amepigwa shoti ya umeme na kupandisha mashetani na ghafla akazimia.

Askofu Gwajima baada ya kumaliza kunyoa alimuombea dada huyo naye akazinduka, askofu akamuonya kwamba asirudie tena kutaka kugusa kichwa chake.

Saluni nzima wakaanza kuimba mbunge... mbunge.... mbunge.

Maendeleo hayana vyama!
Hili ni dude la mbinguni na watanzania tunatakiwa kumtumia kwa maendeleo kwa kwelii
Gwjima oyeee
 
Gwajima anaweza pande zote sishangai wale wanampiga hata Yesu alipokuja dunian walimkataa na sio wote walimkubali sembuse Gwajima kama Yesu tu walimfanyia vile je yeye hvyo Gwajima songa mbele usitishwe na maneno ya watu wala kelele za watu nenda kawatumikie wananchi wako wa kawe
 
Umeongea sana kumbuka sikuhizi watu tunaamini sio kwa maneno tu pia tutumie na video tuone ilivyokuwa maana tukio kubwa kama hilo sidhani kama halikuchukuliwa hata video.
 
Huyo dada alikuwa anamashetani yake tu ndiyo maana alipomgusa Askofu Gwajima akaanguka ila jambo zuri Gwajima hana ubaguzi na ndiyo maana akaamua kumuombea na huyo dada akaamka
 
Hivi Gwajima akiwa mbunge ndiyo atakuwa anatunga sheria yeye mwenyewe na ndiyo atakuwa anapitisha yeye mwenyewe ebu tujiongeze jamani..
 
Yan mmeacha kufanya kampen anapambana na mtu ambaye hamuwezi kumuangusha hata iweje mtapambana sana lakin hamtaweza kumshinda Gwajima oyeeee
 
Askofu Gwajima akihubiri kanisani kwake amesema leo asubuhi wakati anakwenda hapo ibadani alipitia saluni kusafisha kichwa chake.

Alipoingia saluni na kuketi dada mmoja alimjia kwa nyuma na kujaribu kugusa kichwa chake lakini ghafla akaanza kuweweseka kama amepigwa shoti ya umeme na kupandisha mashetani na ghafla akazimia.

Askofu Gwajima baada ya kumaliza kunyoa alimuombea dada huyo naye akazinduka, askofu akamuonya kwamba asirudie tena kutaka kugusa kichwa chake.

Saluni nzima wakaanza kuimba mbunge... mbunge.... mbunge.

Maendeleo hayana vyama!
huo ni uzushi
 
Back
Top Bottom