Kinywaji "Double Kick" kinamaliza vijana

Vijana chukueni tahadhari
 
Hizi pombe nyeupe za bei ndogo sitaki kusikia.
Kuna siku nimetoka mishemishe nikanywa bia safari nne pale ubungo then nikawahi sehemu nyingine.

Nilipofika kama saa kumi jioni, nikawa na mzuka wa kuendelea kunywa ila kuna watu kama 6 wakawa wananisubiria niwafanyie kazi zao na deadline ilibakia siku mbili.

Kwa hiyo nikawa nafanya kazi huku nakunywa smart gin (wenyewe wazoefu wanaita sungura).
Mzuka ulivyopanda nikawa nakunywa tu kama maji.

Mwisho nikashituka kama saa kumi na mbili asubuhi nimekaa vilevile kwenye computer ikiwa ON, smartgin zangu zipo, simu zipo ila nilijigonga damu zilikuwa zimekaukiana hapa juu ya jicho.

Nataka kutoka, nakuta mlango umefungwa. Kucheki nje bahati nzuri nikamkuta mnywaji mmoja katoka kulewa, ndio nikamwagiza akanichukulie funguo nyingine mahali fulani aje anifungulie.

Baadaye saa mbili ndio wakafika wale clients wangu wakanambia bwana tulivyoona huwezi tena kufanya kazi, kwa usalama tukakufungia na funguo tukaweka dukani kwa Mangi ili akufungulie asubuhi.

ULEVI NOMA
 
Smart gin nayo ni kali me ilinishinda Kama ilivyonishinda k vant, konyagi, double kik, rovella. alafu wewe ulichanganya sasa.!!!

Pombe kali ninayoweza kunywa hata chupa ndogo 2 bila shida ni bongo don na han'sons choice baaas.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri wa Bongo Don asubuhi unaamka vizuri kabisa bila gang over. Ubaya bei, chupa ndogo ujazo wa double kick 3000 ingawa kubwa ni bei ya kawaida 9000.
 
Na mimi sasa naenda mwezi wa pili sijagusa, nilikuwa nikiangalia TV hata kama ni Channel ya kiingereza nasikia wanaongea kiswahili. Picha naona kama ni vitu vya kutisha sana mpaka mwili unasisimka, nikilala naona vitu vya ajabu inabidi nikeshe hadi asubuhi. Ikabidi nitandike daruga kwanza ili nijitafakari upya
 
Hiki kinywaji ukiwa na 2,000 TZS unazima mazima. Vijana mtaani wanazoa kinywaji hiki kwa kushindana.
NB: Vijana wanapoteza utu bila kupenda
Hiki kinywaji inabidi kipigwe marufuku mapema sana na Mamlaka za Serekali kabla hatujapoteza vijana wengi zaidi ambao ndio nguvu kazi ya Taifa
 
Wateja wako wastaarabu Sana. Wangekuwa wengine wangeweza kujiongeza kukutatua marinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…