Hiyo kitu ni hatari sana kwa afya, nimewahi fika kwenye kipub ninachopigaga gambe, wanasema K-vant na Konyagi villisha ndo wameagizia. Nikamwambia dogo anipe hiyo double Kick. Sema dogo anamfahamu wife na si mbali sana home (2.5 Km), wife kaitwa kaja kunichukua, imefika asubuhi ndio fahamu zinarudi na hapo nilikuwa nimepiga kama nusu na robo ya kitimoto na ugali wa wanaume wa mikoani. Sijawahi irudia tena. Yaani kina alcohol ya kawaida lakini kinaweza kukutoa roho, siku mbili hali si hali, tapika sana msosi haupandi tena, wakati nina uwezo wa kumaliza K-vant kubwa