Kinywaji "Double Kick" kinamaliza vijana

Kuna hii nyingine “Shimhwa” (Sijui ndivyo inavyoandikwa) inawaumiza sana vijana pasipo wao kujua.
 
Hiki kinywaji ukiwa na 2,000 TZS unazima mazima. Vijana mtaani wanazoa kinywaji hiki kwa kushindana.
Dah!...hivi vinywaji vikali vyote tu vinaharibu vijana kuanzia hiyo double kick, Diamond, Konyagi na vingine vingi.

Hata matumizi makubwa ya 'energy drinks' kwa vijana ni hatari kubwa kwa siku za mbeleni.

Nadhani vijana wenyewe ndio wanaopaswa kulinda afya zao, wakizembea watajitesa wao wenyewe na familia zao hapo baadae.
 
Tafuta pesa
 
Sasa hiko ni kinywaji ama sumu?!
Na kwanini ujitese hivi wakati fedha unatafuta kwa shida na kutumia tena iwe shida.
 
Analeta masikhara na double kick, huku mtaani wanauza cha kupima, kidogo tu ila ukimuona mtu katoka kukipiga aisee, kile kilevi sijui wanaweka nini, dah
 
Yaan kichupa cha 200mls lazima uzime baadhi ya walevi wamepoteza ubikira
Inasikitisha sana, na ni wengi tu hawana ubikira kisa hii kitu, weka mbali kabisa kama mwili wako ni unga unga mwana [emoji23]
 
Daaah pombe inaitwa "Double Kick"?! Jina lake tu limekaa kihuni huni, mwonekano wa chupa yake nao unatia mashaka...iyo ni gongo iliyochangamka[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kwa eneo nilipo wanywaji wamehamia kwenye smart gin, wanasema ukinywa double kick ikifika asubuhi unasikia harufu ya nyama unapohema yaani hapo ujue maini yameiva huko tumboni.
Hahahaha hahahaha
 
Analeta masikhara na double kick, huku mtaani wanauza cha kupima, kidogo tu ila ukimuona mtu katoka kukipiga aisee, kile kilevi sijui wanaweka nini, dah
Nakwambia nakunywaga jipaba peke yanguu nalewa ndio

Ila kuna siku nilipiga dabo kiki chupa moja ile chaap kwa haraka yan chini ya nusu saa nishakamaliza asee sikuamini nilijua nakata moto...

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…