Kwa akili za kikulima, asa ukiwa mkulima unajua kama chakula kipo kingi ama chakula hakuna Kila mkulima anajua hilo swala, tuje kwenye uhalisia kwa sasa chakula kipo chini sana kwa bei, hapa nazungumzia jikoni (shambani), hii bei inamuumiza sana mkulima ndio mana nasema(naunga mkono) hoja ya mheshimiwa raisi kuwa bei zipande na wakulima wapate faida, kwa Tanzania ata iweje kwenye suala la chakula haliwezi kupanda bei mpaka wananchi wakashindwa kununua masokoni ni suala ambalo haliwezekani, nasema hivi sababu najua, nimelima na nimeuza mazao sokoni mwenyewe, Kuna watu wana stock ya miaka miwili nyuma na bado wanaingiza mpya, ata wakisema tuuze nchi jirani chakula kupanda mpaka kufikia bei ya kutisha ni hapana.
NB: hapa nazungumzia mazao ya chakula ambayo wanalima watanzania kwa wingi mf. Mahindi na mchele .....etcetera etcetera
Sent using Jamii Forums mobile app
NB: hapa nazungumzia mazao ya chakula ambayo wanalima watanzania kwa wingi mf. Mahindi na mchele .....etcetera etcetera
Sent using Jamii Forums mobile app