Kiongozi makini na anayejali wananchi wake asingekubali zaidi ya bil 11 kutumika kutengeneza filamu ya namna hii badala ya kuboresha huduma za afya

Kiongozi anayejali wananchi wake asingekubali kukaa miaka 6 madarakani bila nyongeza ya mishahara au kupandisha madaraja.
Kwa kazi ya kuingia saa mbili na kusoma magazeti, kisha chai saa tatu hadi saa tano, kisha lunch saa saba hadi kesho yake tena.?
 
Si bora hata hiyo billion 11 sasa billion zaidi ya 50 zilizopotea bure .kujenga uwanja wa chato unazungumziaje
 
aisee we ndo mbulula kabisa ,kilaza wa mwisho
 
Hadi ifike 2030 mtakuwa mumenyooka..

Kama wewe ni jobless ingia website ya utumishi mama kamwaga ajira kama 600 hivi..

Kuandika ujinga humu haitondoa njaa zako
 
Kuna kichaa alijenga uwanja wa billion 50 kijijini kwake kwa kutumia kampuni yake. Saiv ule uwanja wanaanikia dagaa.
 
Halafu waTz tumekuwa kama wote ni watoto wadogo 'malaika' tusiotambua jema na baya!

Kila lifanywalo na serikali lazima kuli compere na jambo fulani jingine!

Hivi huu ni ugonjwa ama laana sijui!

Hospitali na vituo vya afya vinajengwa, kwa hiyo mambo mengine yasianzishwe ama kutekelezwa hadi hapo vituo vya afya na mahospitali yatakapokamilika?

Hayo mahospitali walishakwambia ni mangapi wanatarajia kuwepo ndiyo iwe idadi tosha itakayokuridhisha wewe?

Kwa hiyo miradi yote ya maendeleo hupimwa kwa kujenga zahanati!

Ununuzi wa ndege, ujenzi wa Sgr na miradi mingine ya kimkakati kama hiyo haikufaa kutekelezwa ili kwanza yajengwe mazahanati!

Raia Tztuna safari ndefu sana kufikia kujitambua.
 
Reactions: Tui
Awamu hii kukosolewa inaitwa Chuki.

It tells alot about a person who is in charge.
Chawa wa awamu mna matatizo makubwa sana ya kiakili.
Aliyekuwa mtetezi mkubwa wa awamu iliyopita,leo akikosoa tu awamu iliyopo,anaitwa mwenye chuki.
Aliyekuwa anakosoa awamu iliyopita aliitwa mpinzani.
 
Mbona alinunua ndege kw matrilioni na mpaka sasa zinatengeneza hasara tu.
 
Akili ya kimaskini hizi ulizorith kitoka kwa mskini mwenzio jpm
 
Ni kweli mkuu, umewahi tizama account za Peter zina followers wangapi au likes tu
 
Umeandika UPUMBAVU mtupu sijui kama unajielewa. Mbegu ambayo ingewezekana ikizidi sana bilioni 1 tena ingefanyika kwa ufanisi hata hapo TBC 1 wewe unazungumzia mbegu bilioni 11? Una akili kweli? Watu wanakufa kwa kukosa huduma bora za afya wewe unaongelea uwekezaji ambao ni wa kubahatisha wala haujafanikiwa tafiti yoyote kama utarejesha manufaa? Watu wajinga kama nyie ni aibu kwa taifa
 
Kiongozi anayejali wananchi wake asingekubali kukaa miaka 6 madarakani bila nyongeza ya mishahara au kupandisha madaraja.
Unawaza tu mishahara badala ya kuwaza kutoka kazini kwako hadi kwa wazee wako kunafikika na barabara zenye usalama wa maisha yako? Waliopandisha wenyewe wamekuta angalau tanzania imeungana kutoka mkoa mmoja hadi mwingine. Kila zama na matukio yake na vipaimbele vyake.
 
Akili ya kimaskini hizi ulizorith kitoka kwa mskini mwenzio jpm
Masikini wapi sa hivi unainjoi barabara mtelezo na mnapokea tuzo kwa bashasha zilizopambaniwa na huyo masikini. Lamba asali tu na safari zisizo na kikomo kisa umekuta madege yapo.
 
Mimi nilidhani ungemjibu kwa hoja ingekuwa vizuri zaidi kuliko kujipaisha mwenyewe na kujiona una akili sana. Kuna kitu gani kipya kilichopo kwenye hiyo filamu ambacho kilikuwa hakijulikani kabla? Kwenye Internet kuna documentaries nyingi kabisa tena zenye kuvutia na kutangaza utalii zaidi kuliko hiyo Royal tour. Hakuna anayepinga matangazo ila watu wanahoji njia na gharama zilizotumika: kwa nini hatukuchagua njia nzuri zaidi; na muhimu zaidi, tutangaze vivutio ambavyo havijulikani kuliko kurudia yale yanayojulikana tena kwa njia inferiour zaidi? Ukweli ni kwamba rais alipekeleshwa na watu wasio na weledi wowote bali wanaongozwa na ushabiki maandaazi! Hii inanikumbusha vituko alivyokuwa anafanya Kikwete mara baada ya kuchaguliwa urais mara ya kwanza. Mara sijui anakimbilia kuwaalika Real Madrid waje Bongo, eti wataitangaza nchi , yaani vitu vya kilimbukeni visivyotakiwa kufanywa na rais!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…