Kiongozi makini na anayejali wananchi wake asingekubali zaidi ya bil 11 kutumika kutengeneza filamu ya namna hii badala ya kuboresha huduma za afya

Kiongozi makini na anayejali wananchi wake asingekubali zaidi ya bil 11 kutumika kutengeneza filamu ya namna hii badala ya kuboresha huduma za afya

Kiongozi MPUMBAVU tu ndiye anayedhani watanzania wote milioni 60 ni watumishi wa umma
Kwani watumishi wa Umma hawastahili kupandishiwa mishahara? Wamekaa miaka 6 bila kupandishiwa mishahara. Kwa taarifa yako ni Rais peke yake ndiye mwenye mamlaka ya kupandisha mishahara kwa watumishi wa Umma.
 
Masikini wapi sa hivi unainjoi barabara mtelezo na mnapokea tuzo kwa bashasha zilizopambaniwa na huyo masikini. Lamba asali tu na safari zisizo na kikomo kisa umekuta madege yapo.
We akiri ndogo unafikiri madege na barabara ndo maendeleo pekee? Maendeleo ni Uhuru wetu ambapo Sasa hivi hatuhofii Tena kusema chochote na kuikosoa serikali waziwazi na ajira zakumwaga private sector na pia kupandishwa mishahara na posho wafanyakazi ili mzunguko wa pes uwe mkubwa. Barabara kwanza zilisababisha mzunguko wa pesa kuwa mdogo Sana na nchi ilikuwa inaenda kukolapse kabisa.
 
Jibu hoja usikimbilie kujificha kwenye non issues!!
Issues are very clear. Wanaondaa Safari chanel ya Tbc walikuwa na uwezo mkubwa kuandaa documentary nzuri na ambayo ingeweza kutumika kupromote tourism. Hiyo bil 11 iliyotumika hovyo ingeboresha huduma za afya.
 
Ni usanii eti HV mnapata wapi muda was kucheki royal tour mwanzo nilipenda wazo ila baada tu kutoka Happ na kwenda kukah huko loss angles wik mbili na kuligarimu taifa mabilion ya shilingi bas nikapoteza msuka was royal tour
 
Ilikuwa ni jambo la kutumia kamera za Tbc taifa na kutengeneza filamu ambayo ingewekwa kwenye masoko mtandao ingeuzika na kuenea dunia nzima.

Hayo mabilioni yaliyotumika yangeimarisha huduma za afya huko vijijini maana vituo vya afya na Zahanati nyingi hazina madawa na vifaa tiba.

Hakuna kitu kipya hii filamu iliyogharimu pesa nyingi itabadili kwa sekta ya utalii. Mkuu wa nchi alipaswa kuwa na uchungu na taifa lake na wananchi wake.

Mkuu wa nchi anashiriki kutwanga vitu vizito kichwani raia wake!

Kinachokusumbua ni kuona mama ndiye Rais badala ya JPM.
Mipango ya Mungu sio mipango ya mwanadamu, unateseka sana ndugu yangu punguza chuki
 
Issues are very clear. Wanaondaa Safari chanel ya Tbc walikuwa na uwezo mkubwa kuandaa documentary nzuri na ambayo ingeweza kutumika kupromote tourism. Hiyo bil 11 iliyotumika hovyo ingeboresha huduma za afya.

Zile pesa za kununua wapinzani zingeweza kuboresha sekta ya afya pia.
Kaa kwa kutulia nchi ina Rais kamili mwanadiplomasia, msikivu na mwenye hofu ya Mungu.
 
Ilikuwa ni jambo la kutumia kamera za Tbc taifa na kutengeneza filamu ambayo ingewekwa kwenye masoko mtandao ingeuzika na kuenea dunia nzima.

Hayo mabilioni yaliyotumika yangeimarisha huduma za afya huko vijijini maana vituo vya afya na Zahanati nyingi hazina madawa na vifaa tiba.

Hakuna kitu kipya hii filamu iliyogharimu pesa nyingi itabadili kwa sekta ya utalii. Mkuu wa nchi alipaswa kuwa na uchungu na taifa lake na wananchi wake.

Mkuu wa nchi anashiriki kutwanga vitu vizito kichwani raia wake!

Sshiiiishh...!! 🐧🐧 Si ushaambiwa ukiniparura, nakupararua nakukata nakutoa damu, ukinikuna nakukuna na kukupapasaaa kabisa..!! Kimyaaa sshiiish
 
Issues are very clear. Wanaondaa Safari chanel ya Tbc walikuwa na uwezo mkubwa kuandaa documentary nzuri na ambayo ingeweza kutumika kupromote tourism. Hiyo bil 11 iliyotumika hovyo ingeboresha huduma za afya.
Mbona miaka yote hiyo hawakuwahi kuja na hiyo idea? Mawazo yanakuwa rahisi kwa mtu baada ya kufanyiwa kazi.
 
Wewe na watu wenye mtizamo kama wako, hawapaswi kulaumiwa maana tatizo lao ni uelewa na exposure. Kumlaumu mtu ambaye akili yake imefikia kimo cha kufikiri ni kumuonea bure.

Kwa lugha rahisi hiyo ni investment ambayo itazalisha. Kwa lugha rahisi zaidi ni mbegu ambayo itazalisha 1000x. .....

Sasa wewe ushauri wako ni kuwa ni bora tungekula mbegu. Mama alipaswa aongoze watoto kula mbegu ili aonekane anajali. Hahaahahah

Kuongoza nchi yenye watu wengi wenye uelewa wa namna hii, you must be very tricky! Vinginevo unaweza ukajikuta unaweka mbegu mezani kweli.

Tuambie n nchi gani Raisi anacheza movie na kuongeza pato la nchi???
Unataka kusema movie itatangaza zaidi ya safari tv??? movie moja au anaendelea kutoa series…..
Apa amebugi izo ela angewekeza kwene safari tv kuiongezea nguvu ifanye international broadcast
-UAE walijikunja kuiwezesha aljazeera saa izi imekua powerful n ni chombo chenye ushawishi mkubwa dunian nyie mmekaa kuupigia upatu movie… tena ya nchi ya tz??
 
Kiongozi makini na mpenda haki asingekubali kikokotoo kinachowanyonga watumishi wastaafu cha 33%
 
Nitoe mfano mmoja tu / muigizaji filamu wa kibongo akipata fursa ya kuigiza na Silvester Stalline ( Rambo) au aigize na wa hapa hapa.
Atapata milege (mafanikio ya kimataifa) na nani?
Mara nyingine unahitaji kugharamia ili utangaze na ufanye biashara.
Mfano tangaza biashara zako wakati wanacheza mpira kwenye Azam Tv Ihefu na Mbeya City au Simba na Yanga !!! Utasikika na kujulikana wapi zaidi???
Na je utangaze Kupitia mechi Ya Liverpool vs Man City.
Mifano mingi sana . Mafanikio ni gharama pia.

Tuamie iyo movie ina viewer wangap na imeingiza wangap??..

mngeiga hata rwanda ipeni timu inayowika ulaya andiken mabango ya vivutio au hamuoni Etihad wanafanya
 
Back
Top Bottom