Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh afariki baada ya kushambuliwa akiwa Iran

Kiongozi Mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh afariki baada ya kushambuliwa akiwa Iran

Siwezi kusupport hiyo mipumbavu mie.

Yaani tuliisupport vizuri kabisa back then ila cha ajabu ikawa upande wa Idi Amin kwenye vita vya Kagera. Juzi hapa imeua vijana wa Kitanzania waliokuwa masomoni Israel.

Wapambane na hali yao wajinga wale.

Huo ni mwono wako ndugu. Ila kina Mandela, Lissu na wengine wa namna hiyo nao wana miono yao.

Hao hapo juu CVs zao tunazijua na wengine hata wana hadi Nobeli vibindoni.

Labda ungetuwekea japo ka CV kako basi, ili tuone kama una merits zozote za kujimwambafai hivi kama wewe mbele za watu? Kama kakiwemo humo japo ka ukatibu kata, labda si inaweza ikapendeza zaidi?

Lakini kama kumbe ni kwa sababu tu nawe una domo ndugu?

Looh!

Kwa hakika huo si hata kuku anao?
 
Siwezi kusupport hiyo mipumbavu mie.

Yaani tuliisupport vizuri kabisa back then ila cha ajabu ikawa upande wa Idi Amin kwenye vita vya Kagera. Juzi hapa imeua vijana wa Kitanzania waliokuwa masomoni Israel.

Wapambane na hali yao wajinga wale.
Una ongea as if tuna cha kuwasaidia wakati na sisu tuna itaji misaada ..ayo machuma tunayo pitisha pale uwanja wa uhuru ndo uende nayo vitani
 
Jamaa kauzwa , Kaishi Qatar miaka kibao juzi tu hapa kaenda Iran ndio kauzwa ...Nasrallah aligoma kwenda hapa kutakuta kutokea vita hawa iran wanauza wenzao .

Nchi za salaama ni Qatar na saudia pale kati , hazina ufungamano wa makundi zaidi ya serikali
Sasa hivi unawakataa mashujaa wako Iran sio?
 
Hii dunia kuna binadamu wakikuamulia hata uende wapi hutoboi, Mossad ni hatari sana
 
yaani wewe hujafikia level ya kubishana vifungu vya Bible na mimi, kwasababu hauijui, kwa kukusaidia, amini tu kwamba alifufuka ili tuokoe muda.
Kwa hivyo Wale waliosemwa kwenye Marko 14;50 ni uongo?
 
Yaani, ninachojiuliza mimi ni kuwa ameuawa Iran.. siku ya kuapishwa Rais mpya wa Iran... ila sijui wamefanyaje; itakuwa ni bomu la kutega maana sidhani kama ni kombora au drone... ameletewa zawadi au kuna mtu kaingiza ndani zawadi... tena mtu wa kuaminika kabisa...
Yawezekana ni space laser weapon
 
Aisee Benjamin netanyahuu hacheki na kima jana usiku lebanon imekula mashambulizi ya kufa mtu mpaka beirut na tayari afisa mwandamizi wa hezbollah ameliwa kichwa
Watu wanakazania madrasa kuliko shule. wanakazana kuoa wake wanne, yaani unashinda kumbato wanawake kwa zamu halafu unatagemea kumpiga myahudi. Aisee wanahitaji reformation kubwa sana. Waaanze na kuwasomesha ma sheikh wao. Hawajui nini maana ya theology na philosophy na kila ijumaa wanatoa mawaidha. Wavaa makobazi ndugu zangu amkeni. Siwacheki wala kuwadharau lakini hakuna mtu atakayekuja kuwaokoa bali nyinyi wenyewe.
 
Kile kifo cha Rais wa Iran na aina ya Helicopter waliokuwa wanatumia na excuse za kwanini walikuwa wanatumia ile Helicopter ilitosha kabisa kuniambia Iran ni mwepesi mno.

Huwezi kutumia Helicopter aina ile halafu unaugomvi na USA na ISRAEL, maana mle kwenye helicopter Kuna electronics chips nyingi sana + control boxes ambazo mtu anaweza kufanya remote communication na kuchukua control.

Hili la Israeli kufanya mashambulio ya ndani ya Iran mara kwa mara limeonyesha pia how Iran is weak kwa sasa kuanzisha vita na adui alikuwa zaidi ya 1500km.

Iran anapaswa kubaki Low key, atafute technolojia na kutengeneza watu wenye akili na maarifa na sio kuendelea kutegemea wapiganaji mashujaa wanaoweza kutumia nguvu tu na sio akili, Dunia ya sasa inataka technolojia na watu wenye akili kila mahala kuanzia kwenye ujasusi na vita.
IMG_20240731_115251.jpg

Check vyuma vya North Korea hivyo.. Iran kelele nyingi kumbe raisi anatumia helicopter utumbo utumbo tu..
 
Kaisome vizuri Quran, inakwambia shetani alizaa, lakini haithibitishi ikiwa shetani anamke, mantiki hii tu, inatosha kusema, Ikiwa shetani wa Quran anauwezo wa kuzaa bila mke, maana yake mungu wa Quran anakuwa hana uwezo wa kumzidi shetani wa Qur'an ambaye alizaa bila mke

Lakini Mungu wa Biblia, yeye anauwezo wa kuzaa bila mke, na ukibisha hili, maana yake unampinga Mungu katika uweza wake

Unakuwa unamwamini kuwa anaweza yote ila si kuzaa bila mke!
Mungu wa biblia anaweza hata kukamatwa akiwa na kijana aliyeweka chupi begani pia anaweza hata akipata kibano kumlilia Mungu wake wa kweli Na machozi ya damu kumtoka au vipi?
 
Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh ameuawa nchini Iran, kundi hilo limesema.

Katika taarifa iliyotolewa leo siku ya Jumatano, Hamas imesema Haniyeh aliuawa kufuatia uvamizi wa Israel kwenye makazi yake mjini Tehran.

Kwa mujibu wa kundi hilo, Haniyeh alifariki baada ya kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian aliyeapishwa siku ya Jumanne.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Irani lilisema chanzo cha "tukio" hakijafahamika mara moja lakini "kinachunguzwa", shirika la habari la AFP liliripoti.


Usicheze na MOSSAD

=========

Ismail Haniyeh alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa Hamas kwa miongo miwili iliyopita, akiongoza shughuli za kisiasa za kundi hilo la kijeshi akiwa uhamishoni nchini Qatar katika miaka ya hivi karibuni.

Jumanne ya tarehe 30 Julai, 2024, Bw. Haniyeh alikuwa Iran na wanachama wengine wakuu wa "mhimili wa upinzani" wa Iran — ambao unajumuisha Hamas huko Gaza, Hezbollah nchini Lebanon na Wahouthi huko Yemen — kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa Iran.

Kama kiongozi wa kisiasa wa Hamas, alikuwa muhimu katika mazungumzo na diplomasia yenye hatari kubwa ya kundi hilo, ikiwemo mazungumzo yaliyokwama ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel.

Haya ndio tunayojua: Kiongozi wa Hamas huko Gaza

Bw. Haniyeh aliteuliwa kuwa kiongozi wa Hamas huko Gaza mwaka 2006. Mwaka huo, alihudumu kwa muda mfupi kama waziri mkuu wa serikali ya umoja wa Palestina, ambayo ilivunjwa baada ya miezi ya mvutano uliyojumuisha mapigano ya silaha kati ya makundi ya Palestina.

Mwaka 2017, aliteuliwa kuwa kiongozi wa ofisi ya kisiasa ya Hamas wakati ambapo walikuwa wakijaribu kupunguza taswira yao ya umma walipokuwa wakijaribu kushawishi Wapalestina na kimataifa.

Bw. Haniyeh aliongoza Hamas kutoka Qatar na Uturuki katika miaka ya hivi karibuni. Alikuwa miongoni mwa wajumbe wa mazungumzo yanayoendelea kati ya Israel na Hamas, yaliyosimamiwa na Misri, Qatar na Marekani, kumaliza vita vya Gaza kwa kubadilishana na mateka waliotekwa kwenye shambulio lililoongozwa na Hamas dhidi ya Israel.Kupanda kwa Madaraka

Alipozaliwa
Bw. Haniyeh alizaliwa mwaka 1962 katika kambi ya wakimbizi ya Shati kaskazini mwa Jiji la Gaza, kwa wazazi wa Kipalestina ambao mwaka 1948 walihamishwa kutoka nyumbani kwao katika eneo ambalo sasa ni Israel, huko Ashkelon. Alisoma katika shule zinazoendeshwa na shirika kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wapalestina, UNRWA, na kuendelea kusomea fasihi ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza.

Alikamatwa na jeshi la Israel na kuhudumia vifungo kadhaa katika magereza ya Israel miaka ya 1980 na 1990.

Kushika madaraka
Kupanda kwake madarakani huko Gaza kulisaidiwa na mshauri wake, kiongozi wa kiroho na mwanzilishi wa Hamas, Sheik Yassin, ambaye alimtumikia kama katibu binafsi. Wawili hao walikuwa malengo ya jaribio la mauaji ya Israel mwaka 2003; mwaka uliofuata, Bw. Yassin aliuawa na jeshi la Israel.

"Haupaswi kulia," Bw. Haniyeh aliwaambia umati uliojitokeza nje ya Hospitali ya Shifa huko Jiji la Gaza wakati huo. "Unapaswa kuwa imara, na unapaswa kuwa tayari kwa kulipiza kisasi."Anatafutwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu

Mwezi Mei, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu alisema atatafuta kibali cha kumkamata Bw. Haniyeh. Mwendesha mashtaka alimshutumu yeye na viongozi wengine wa Hamas kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu kuhusiana na shambulio la Oktoba 7 dhidi ya Israel, ikiwemo "kuteketeza, mauaji, kuteka mateka, ubakaji na unyanyasaji wa kingono katika kizuizi."

Familia yake kuuawa na Israeli
Mwezi Juni, Hamas ilisema kuwa dada wa Bw. Haniyeh na familia yake waliuawa katika shambulio la kijeshi la Israel kwenye nyumba ya familia ya Haniyeh huko Gaza, madai ambayo jeshi halikuthibitisha. Mwezi Aprili, watoto watatu wa kiume wa Bw. Haniyeh kati ya watoto wake 13 waliuawa na vikosi vya Israel katika operesheni nyingine ya kijeshi huko Gaza.

Alikuwa mkaidi mbele ya hasara hiyo, na jambo kuu katika maisha ya Bw. Haniyeh ilikuwa: "Hatutasalimu amri" Bw. Haniyeh alisema wakati huo, akibainisha kuwa tayari alipoteza jamaa kadhaa katika vita hivyo.
Special unit of Israel called Kidon.... Acha kabisa Dunia imesimama usiku. Wakati Israel wakiwa ktk moja ya operation ngumu kabisa kuwahi tokea. Iran lazima aseme poooo.. Hezbollah Naye lazima aseme poo sidhani kama atarusha mabomu tena. Maana wamesha ambiwa wanakitaka kichwa cha mkuu wao. Kuifuta Hamas nijambo linawezeka
 
Back
Top Bottom