let the caged bird sings
JF-Expert Member
- Sep 19, 2020
- 3,699
- 8,857
8:54 "Anayenipa heshima ni Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnamwita Mungu wenu".Katika Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina hilo.
Katika Mathayo 27.43 yanatajwa maneno ya wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu.
Walikuwa wakimzulia kuwa anadai uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli.
Mara nyingi waliokuwa wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani.
Ama mwenyewe Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrani, lugha yake, Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu.
Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80.
Mahasimu zake wa Kiyahudi walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa Mayahudi.
hicho ni kinywa cha Nani?.