umeniuliza kuhusu yohana,Marko,Luka ama umeniuliza kauli ya yesu?.
wewe umeshavuta bangi ya dini,hakuna utakachokubali hata kama kitafunuliwa katika framework yoyote.
I'M OUT
Tulia tueleweshane kistaarabu
wewe umeniwekea nambari tu bila kuandika umetoa wapi , mimi ndio nikakuuliza vile
Tukiendelea
Francis Young, Mwalimu wa mafunzo ya Agano Jipya katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, akiandika katika kitabu kinachoitwa
The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) anasema:
"Isipokuwa katika Injili ya Yohana, ambako maneno ya maelezo yamewekwa kwenye mdomo wa Yesu, injili zote nyengine zinaeleza kuwa wenye kutumia maneno kama 'Mtakatifu wa Mungu', au 'Mwana wa Daudi', au 'Mwana wa Mungu' si Yesu bali wengineo.
Jina pekee alilokuwa mwenyewe Yesu daima akilitumia ni 'Mwana wa Adamu'... "
Yafaa pia tukumbuke kuwa katika zama za Yesu ilikuwa ni jambo lililoenea kuwabandikiza ungu viumbe vya hadithini na hata wanaadamu wa kweli kweli walio hai.
Mwandishi wa kipagani Laertu alieandika kitabu kiitwacho Lives of the Philosophers (Maisha ya Mafailasufi), ameandika kuwa mafailasufi kadhaa wa kadhaa walikuwa wana wa Mungu.
Plato amesimuliwa kuwa wazee wake ni miungu; hali kadhaalika Paithagoras akiaminiwa kuwa ni mwana mungu aliyekuwa mwanaadamu na mzazi wake ni mungu aitwae Hermes.
Empedokles pia alidaiwa kuwa ni mungu wa milele aliyekuwa akiponyesha wagonjwa, na wafwasi wake wakimuabudu na kumsalia.
Plutarch, mwandishi mwengine wa zama hizo, alikuwa anaamini kuwa bila ya shaka yo yote Alexander (Iskandar) Mkubwa ni mwana wa mungu, na Romulus, huyo anayedhaniwa kuwa ndiye baba wa Warumi, alikuwa ni Mwana wa Mars (Marrikh), mungu wa vita.
Yeye akiaminiwa kuwa alipaa mbinguni katika kiwingu.
Yapo maandishi ya mwaka 48 K.K. (Kabla ya Yesu) yaliyomweleza Juliasi Kaisari, Mtawala maarfu wa Warumi, kuwa ni 'mungu wa kweli, mwana wa Ares na Aphrodites, mwokozi wa wote wa maisha ya wanaadamu.' Maandishi mengine yanamtaja Agosti Kaisari, aliyerithi utawala wa Juliasi, kuwa 'Mfalme wa wafalme, Kaisari, Mwana wa Mungu, mungu Agosti, mwaangalizi wa ardhi na bahari'.
Majina haya, basi, ya "mungu", "mwana wa mungu" na "Bwana" kwa kuwa yalikuwa yameenea na maarufu katika nchi za bahari ya Kati (
Mediterranean) katika zama za Yesu haiwezi kukosa kuathiri mawazo ya watu ambao bado haijawavaa imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja kama ilivyokuwa ikifunza dini ya Kiyahudi.
Majina kama hayo yalikuwa yakitumiliwa ovyo na kila mtu takriban.