Ni bahati mbaya nimekuwa busy sijaweza kuchangia wala kupitia maoni ya wachangiaji wengine na pia kutokana na ujinga unaoendelea kujitokeza jukwaani kuona wenye mawazo tofauti kuwa wametumwa na nape nk naomba nisichangie....ila nakumbuka jumamosi iliyopita nilimuuliza mchangiaji mmoja kuwa just imagine unasafiri then yanakukuta ya kukukuta njiani halafu mgomo unaoushabikia unaendelea...fumba macho then uone hiyo picha..
At the end tulikubaliana kutokuelewana... Nachotaka kusema hapa ni kuwa bila kujali ulimboka kafanya/kafanywa nini pengine na nani bali yuko kama tunavyomuona kwenye picha...(mimi si mmojawapo wa wanaoshabikia mabaya) lakini bila huduma za madaktari (pamoja na ukweli kuwa yeye ni daktari) asilimia za kumkosa ni kubwa...je ni wangapi kuanzia kule Kintinku, Misenyi, Nguruka, Lituhi, Namanyere, Karumeli, Mbambabay Nyachabakeni, Muhoro, nk nk wanaopatwa na masahibu kama haya na wanaathirika na mgomo alouasisi yeye na hatimaye kufa kwa kukosa huduma?
Hivi maisha ya mtu yana mbadala?? serekali wanayoigomea inaathirika vipi na hili? yanini tunamalizana wenyewe kwa kudhani kuna tunayemkomoa serekalini? ...acha niwe kilaza katika hili ila bado sielewi madaktari na wanaowaunga mkono... wangetenganisha madai ya mshahara na madai ya mazingira bora ya kufanyia kazi wangeeleweka vizuri sana na tungewaunga mkono saana tu...lakini madai ya mshahara wa millioni 3 kufichwa ndani ya madai ya kuboresha huduma ...nitakuwa wa mwisho kuelewa...
Hakuna aliyelazimishwa kuwa daktari ila ukeshakuwa daktari una kiapo cha kutumikia wagonjwa...leo mzima kesho nani anajua UTAKUWA KAMA ULIMBOKA?? Alijua kuwa atakutana na alokutana nayo? Hasha...sitaki na wala sitaingika kwenye mjadala wa ama ameshughulikiwa na serekali, amefumaniwa amepata ajali...what ever the case lakini wapo watanzania wangapi ambao hawajiwezi (kama yeye) na sasa wanavuta pumzi za mwisho bila msaada kutokana na mgomo alouasisi?
Mbona wenzie hawakugoma kwake?? wamelipwa millioni 3? Nakaribisha matusi kama ilivyo kawaida ya JF nowadays ....kwamba lazima tuwaze yanayofanana.
kwa upande mkubwa nakuunga mkono kwa point 2. kwanza wana JF wao wanataka mawazo yote yaendane na kuichafua Serikali ama CCM.
Pili ni kwamba, pengine vifo na mahangaiko ya watu walioadhirika na mgomo aliouasisis unamgeukia!
Cha msingi tusikimbilie ku conclude kwamba serikali ndio imefanya hivyo, Uwezekano ni pamoja na
1. ndugu wa mmojawapo wa aliyefariki kwa adhari ya mgomo kafanya hivyo kwa hasira
2. Watendaji walionyanganywa kitumbua chao wakaamua kufanya hivyo kwa hasira
3. Serikali ikaona usalama wa taifa unayumba kwa sababu ya msimamo wao naye kama kiongozi.
4. wanasiasa wanataka umaarufu au kuichafua seriakli kwa kutumia loop hio
5. sababu za kijamii ikiwemo madai, mapenzi, chuki etc
6. sababu tofauti na hayo
kumbuka Ulimboka ni Dr ambaye hata hatibu ila ndio kakomaa na wakati serikali inaona uwezekano ni hakuna kwani hata walimu wanahitaji chaki, madawati na kahawa kurekebisha mazingira ya kazi, nao pia wanahitahi 3M na malupulupu so 9M hapo ameanza tu kazi, je Dr bingwa inakuwaje, like-wise police, makarani, mahakimu, na wafanyakazi wote wanahitaji hata laki4 tu. why so special wakati uspecial walishapewa?
ndugu, tusikimbilie ushabiki wa kisiasa, chuki na kuharibu amani zaidi