zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Hata hivyo, habari ambazo tumeweza kuzipata sasa hivi ni kuwa watu waliomchukua wanadaiwa ni polisi na kuwa yuko kwenye kituo cha Bunju nje ya jiji la Dar kupita maeneo ya Mbezi. Sasa hivi wanasheria na vyombo vya haki za binadamu vinafuatilia kujua hali yake huko aliko kwani juhudi za kutaka kuzungumza naye kwa simu zimeshindikana.
Ni matumaini yangu - na bila ya shaka ya wengine - kuwa Dr. Ulimboka ambaye ameonekana kama kiongozi wa mgomo wa madaktari unaondelea nchini hatodhurika kwa namna yoyote ile na kuwa sheria zote zinafuatwa siyo na wale wanaotaka wengine wafuate sheria bali na wale wanaopaswa kufuata sheria.
Kwa niaba yangu na CCTI tunalaani vitendo hivi ambavyo vinaonekana kutaka kugeuza Tanzania kuwa police state hasa baada ya kushindwa kutafuta suluhisho la kawaida. Na zaidi kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa kinyume na sheria au haki au utawala wa sheria tunataka wahusika wote wawajibishwe mara moja.
Free Dr. Ulimboka Now!
Kwenda kuhojiwa polisi ndio mleta mada anasema k"atekwa"?
Adhuriwe nini huyo wakati tayari kisha dhurika? au hamjui gonjwa linalomsumbua?