Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Hata hivyo, habari ambazo tumeweza kuzipata sasa hivi ni kuwa watu waliomchukua wanadaiwa ni polisi na kuwa yuko kwenye kituo cha Bunju nje ya jiji la Dar kupita maeneo ya Mbezi. Sasa hivi wanasheria na vyombo vya haki za binadamu vinafuatilia kujua hali yake huko aliko kwani juhudi za kutaka kuzungumza naye kwa simu zimeshindikana.

Ni matumaini yangu - na bila ya shaka ya wengine - kuwa Dr. Ulimboka ambaye ameonekana kama kiongozi wa mgomo wa madaktari unaondelea nchini hatodhurika kwa namna yoyote ile na kuwa sheria zote zinafuatwa siyo na wale wanaotaka wengine wafuate sheria bali na wale wanaopaswa kufuata sheria.

Kwa niaba yangu na CCTI tunalaani vitendo hivi ambavyo vinaonekana kutaka kugeuza Tanzania kuwa police state hasa baada ya kushindwa kutafuta suluhisho la kawaida. Na zaidi kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa kinyume na sheria au haki au utawala wa sheria tunataka wahusika wote wawajibishwe mara moja.

Free Dr. Ulimboka Now!

Kwenda kuhojiwa polisi ndio mleta mada anasema k"atekwa"?

Adhuriwe nini huyo wakati tayari kisha dhurika? au hamjui gonjwa linalomsumbua?
 
Ulimboka ni mtu maarufu hivi hakuna mwanaJF ambaye ana mawasiliano naye???? tunatoka povu pasipo sababu kwa habari ambayo ni tetesi
 
Hili ni ombi kwa Rais wetu wa serikali chini ya chama
cha mapunduzi. Mh RAis tunakuomba utoe release order
ya kumuachia Dr Ulimboka maana hii italeta madhara
zaidi kwa watanzania...........................

Please free Dr Ulimboka

Kidumu chama cha mapinduzi
 
Kwenda kuhojiwa polisi ndio mleta mada anasema katekwa?

Adhuriwe nini huyo wakati tayari kisha dhurika? au hamjui gonjwa linalomsumbua?

Ni mgonjwa hata kabla hajatekwa kama una macho mwangalie vizuri utajua anaumwa nini? anataka kwenda na mwengi??

Gonjwa linalomsumbua linaweza kuwa limeharibu kichwa chake tukidhani anatetea wanyonge.
 
2013 Pinda 'NJE' 2015 CCM 'NJE'.
Wanakimbia wenyewe pasipo kufukuzwa.
 
Nadhani hii ni sera yao kwani yaonekana vitisho na ubabe ndo kanuni yao. Angalia yaliyotokea kule Igunga na Arumeru Mashariki mara tu baada ya Chaguzi ndogo, wakidhani kwa Kutesa/Kuua ndo wataungwa mkono, matokeo yake wanazidi kuchochea Chuki na Hasira toka kwa Watanzania.

I do support it, FREE DR. ULIMBOKA NOW.
 
wewe si ndio mdogo wake unayempelekea chakula gerezani!!! tuambie yuko gereza lipi?
mtolera na ulimboka wapi na wapi?

hapa ufumbuzi ni kutatua matatizo yao na si kukimbilia kushika watu,wakati pesa mingi yaenda mabank ya nje
 
Dr. Ulimboka inadaiwa amekamatwa na polisi usiku kwenye majira ya saa saba kasoro hivi akiwa na wenzake. Watu ambao hawakujitambulisha na wakiwa na mavazi ya kiraia lakini wakiwa na silaha walimchukua Dr. Ulimboka mkukumkuku kwenda kusikojulikana. JItihada za awali za kufuatilia zilionekana kugonga mwamba. Hata hivyo, habari ambazo tumeweza kuzipata sasa hivi ni kuwa watu waliomchukua wanadaiwa ni polisi na kuwa yuko kwenye kituo cha Bunju nje ya jiji la Dar kupita maeneo ya Mbezi. Sasa hivi wanasheria na vyombo vya haki za binadamu vinafuatilia kujua hali yake huko aliko kwani juhudi za kutaka kuzungumza naye kwa simu zimeshindikana.

Ni matumaini yangu - na bila ya shaka ya wengine - kuwa Dr. Ulimboka ambaye ameonekana kama kiongozi wa mgomo wa madaktari unaondelea nchini hatodhurika kwa namna yoyote ile na kuwa sheria zote zinafuatwa siyo na wale wanaotaka wengine wafuate sheria bali na wale wanaopaswa kufuata sheria.

Kwa niaba yangu na CCTI tunalaani vitendo hivi ambavyo vinaonekana kutaka kugeuza Tanzania kuwa police state hasa baada ya kushindwa kutafuta suluhisho la kawaida. Na zaidi kama kuna jambo lolote ambalo limefanywa kinyume na sheria au haki au utawala wa sheria tunataka wahusika wote wawajibishwe mara moja.

Free Dr. Ulimboka Now!

Kumkamata Dr. Ulimboka ni dhahiri kwamba serikali imeshindwa kuleta suluhu ya mgomo wa madaktari. Hii siyo njia ya kutatua mgogoro huu bali ni kuuchochea. Ni vema serikali ikamwachia haraka iwezekanavyo. Free Dr. Ulimboka Now! I support mgomo wa Madaktari!
 
Yaani nilikuwa nasubiria kitu kama hichi nipate sababu ya kuwaamsha watu mZuka! One mistake one winning GoaL!

Free DR. ULiMBOKA NOW!
 
Back
Top Bottom