Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana

pole sana dr.ulimboka. Naangalia upande wapili wa shilingi ni huu,unaweza kufanya kitu usijue itakuwaje kesho,lakini naamini sana walichofanya serilaki yetu sikivu ni kumpandisha chati zaidi aonekane ni mkombozi wa wanyonge.

kwenye hii muvi ya mgomo wa ma doctor wanyonge ni akina nani? Madokta waliogoma au wagonjwa wanaokufa kwa kukosa huduma?
 
pia Pinda ataenda naye....ningekuwa daktari wa zamu nawadunga sindano ya sumu! na potelea mbali kuhusu mustakabali wangu
 
Tumeingiliwa na viwavi jeshi badala ya kuomba wote wakae mezani wasikilizane wewe unaleta crapp!! zako hapo.Wote wanaumuhimu wagonjwa na serekali .Swali mbona enzi za Mkapa hatukusikia vitu vya kijinga jinga kama sasa!!Serekali na wananchi wajihoji
 
bora kuishi na vvu utatumia arv kuliko kuwa na serikali ya kipuuzi,dhaifu,mafia ,majambazi,kama hii.

pole kwa dr ulimboka na familia yake.Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

hivi sheria inasemaje kuhusu hili, mahakama imetoa hukumu , huku nyuma mhukumiwa anapigwa karibu na kifo.
 
Swali langu mi nahoji kwann madaktari wameudumie yeye wakati wamegoma? Mwacheni naye aonje machungu wanayopata wagonjwa hapo hapo Muhimbili kwa kuendeleza mgomo wao, Mkuki kwa Nguruwe sio?

Acha kuropoka pumba wewe kijana, kama hujui uchuna. Weka UNYINYIEM WAKO KUSHOTO.
 
Nikweli kabisa naungana na wewe pia. Ila umeruka moja.
SERIKALI
Inawezekana kabisa watumishi wa serikali (wanausalama/polisi) wakayafanya haya hata kama hawajaagizwa hilo. Tumekuwa tukishuudia watu wa usalama wakifanya mambo kinyume cha haki za binadamu/Katiba yetu na bado hakuna mkono unaoweza kuwagusa. Ni mapema sana kuhukumu kwasasa, tuombe Mungu Dr.Ulimboka apate nafuu upesi ili asaidie kupatikana kwa taarifa kamili kuhusiana na tukio hili.

Ni Usalama wa Taifa wamekosa akili inaelekea walishindwa namna nyingine ya kumuuwa zaidi ya kumteka mbele ya wenzake kama hawana akili kiasi hiki hii nchi tuko salama kweli
 
Kwani dr ulimboka nae ni msanii? Mukulu anatembeleaga wasanii wenzie tu!
 
Napata shida kidogo kwamba nikupe pole wewe au wale wagonjwa ambao kwa lengo lenu la kugoma na kuiwajibisha serikali wengi wanateseka,wengine wanakufa,mama zetu wanajifungua kwa uchungu bila ya kua na msaada wowote,haya ni mateso makubwa,
Hemu tujiulize vipi kama ulimboka na yeye kama akitelekezwa aachwe bila ya huduma yoyote?
ni vyema madaktari watafute njia tofauti yakuibana serikali kwani watanzania wasio na hatia wanakufa kwa kosa la serikali


Watafue njia ipi hebu tijulishe, sio lazima uandike hapa JF.
 
Kampe pole mama yako ambaye hata kansa ya shingo inayotibika wameshindwa kuigundua mapema kwa sababu tuu Jakaya kawauzia wazungu migodi

jitahidi kujenga hoja acha ushabiki,
ulimboka ni nani awe na thamani kuliko ma elfu ya watanzani wanaoteseka kwa mgomo?
madaktari walipo goma sijaona mtu hata mmoja akiwaita wanyama kwa mateso wanayopata watanzania wasio na hatia kwani wao sio serikali.
 
Kwa hili ndo madakari mnatakiwa kuonesha msimamo wenu na hata ikibidi mgome mwaka mzima maana haki haiji ila kwa ncha ya upanga.
 
kama polisi na wanasiasa wanadhani wao ni bora...!

NAWAASI MA DOCTOR WOTE... ASKARI YEYOTE NA MWANASIASA AKIJA HOI HAPO MUHIMBILI MKIMBIENI KAMA UKOMA..!

mbona watanyooka wenyewe..!
 
Katika mazingira ya namna hiii, umakini kwa pande zote ni kitu cha muhimu sana. Kumuumiza Ulimboka kwa sasa, hata kama anawaongoza madaktari ambao watu wanahisia tofauti kuhusu kinachotokea, ni vyema busara za hali ya juu zikatumika kutatua matatizo yanayotukabili.

Mgomo unajadilika.Serikali haitakiwi kujiona ina nguvu kwa kila kitu na kutumia mahakama zake kutoa maamuzi, maana pasipo haki hata maamuzi yakitolewa na mahakama ya namna gani hayatatekeleawa.

Tunahitaji kukaa chini Watanzania wa kada zote na kukubaliana tunakotaka twende na tuavyopaswa kuendesha nchi ili kila mmoja wetu aishi kwa furaha na amani.

Serikali ichukue hatua kwa waliohusika na kitendo cha kumdhuru huyu Dr. ulimboka, hata kama ni watu wao wachukuliwe hatua za kinidhamu maana hili litaendeleza ugomvi na hasira na mwisho wataumia waliomo na wasiokuwemo.

Sisi wakulima ambao ni wa hali ya chini tutaathirika sana.

Ninasikitika sana.
 
Huu ni unafiki usiopimika! Kwa hakika hata Kubenea alifanyiwa mambo ya aina hii na maswahibu wake na yeye akijua hivyo, akawa wa kwanza kumtembelea Kubenea! Inauma sana!
 
Duh huu Si Ubinadam Ingawa Binafsi Siungi Mkono Mgomo Wa Madaktari But huu Ni UNYAMA kumfanyia Binaadam Jambo Kama Hili

It's Important Serekali Ifanye Uchunguzi Nimeona Picha za Huyu Brother Ameng'olewa Kucha Za Mkononi kwa Plaizi Serekali yetu inawajibu Wa Kulinda Usalama Wa RAIA uchunguzi ufanyike alotenda hili ajulikane Si sawa kabisa Na Serekali Inawajubu wakutafuta wahalifu Hawa sitaki kuamini jambo hili linamahusiano Na Mgomo Na Kama mtu huyu kaumizwa hivi kwa ajili ya Mgomo we cnt solve Matatizo ya Jamii yetu kwa njia ya Kuumiza watu walofanya hivi Si Binaadam
 
Back
Top Bottom